True love....
Am praying for true loveeeeeeeeeeeeee!!!
mhhh wenye bakhti zao
Thanks Mkuu, you touched my heart. Kuna ndugu mmoja alioa mke na wakabarikiwa wakawa matajiri kwa kiasi chao, lots of investments and money.
Bwana yule akawa na hawara nje ambaye alimthamini na kusahau jinsi walivyohangaika na mke wa ndoa. Kwa bahati mbaya mke wa ndoa akaugua, na ilitokana na mawazo mengi hivyo akapata strock.
Hebu shangaa jinsi ambavyo yule Bwana alikimbilia kufunga ndoa nyingine ya kiserikali na yule hawara kabla mke hajafa!!! Na akawa anaenda kumtembelea mkewe huku akiwa na mke mpya ambaea fika mkewe alimfahamu na pengine was a cause for her illiness.
Sadly, yule mke wa ndoa passed away, huku akilia kwa uchungu sana na kumuita Mungu. Haikupita miezi sita mumewe ghafla alidondoka na kufa papo hapo.
Tuepuke laana za wake wa ujana wetu, ni mbaya. Hata kama umechana naye kwa kuwa umepata chombo kipya, but mheshimu. Ndoa ni ndoana kama hutaigharamia katika kuikuza kwa heshima na upendo!
Ukhti Nilham, umepotelea wapi wewe uonekani siku hizi, vipi hali yako kiafya mara ya mwisho nakumbuka ulisema upo Hospitali.x paster wallah katika siku ulizonifurahisha leo ya kwanza sasa signature yangu ishapanda chati hehehhe dat's true,,,(true love never die),,,nice storry,,,
Muelekee Muumba wako, hakukutanishe na mtu atakaye kupenda maisha na wewe kumpenda.nielekeze kunakotengenezwa bakhti nikatoe hili gundu!
shost hii kauli yako... ina story moja ndefu sana behind!.. pole
Muelekee Muumba wako, hakukutanishe na mtu atakaye kupenda maisha na wewe kumpenda.
Tatizo kubwa ambalo vijana wengi wa kileo linawakuta, ni kushindwa kudumisha upendo dhidi yao wapendanao, wanafikiria kila kitu kinakuja tu, bila jitihada ya kuvumiliana na kuaminiana na kuthaminiana.
Wengi wanashindwa kujiepusha na vitendo vinavyopelekea wenza wao kuwatilia mashaka. Na saa nyingine wakisha zoea ile hali ya kupendwa, basi ujiona kuwa chochote atakachofanya kwa kuwa anapendwa basi akita athri upendo wa mweza wake. Na matokeo yake ni kujuta na kukosa kile alichokizoea kukipata kutoka kwa mwenza wake.
Bahri ya mapenzi ni pana sana, ni bahri yenye mawimbi mazito yanayo ambatana na dhoruba za hapa na pale, dhoruba zinazo ambatana na mapapa na manyangumi. Inataka muogeleaji stadi alie mahiri na mvumilivu. Na haswa subra na kuto kata tamaa mapema.