A statesman is madly needed,tumepotoka tutaangamia kwa kukosa maarifa

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,695
31,480
Amani ya bwana iwe nanyi wana JF

Katika kipindi hiki cha kwaresma nimeona ni vyema tukafanya tafakari ya muenendo wa kisiasa katika Taifa letu. Tafakari yangu haitaongozwa na Waraka pendwa wa TEC bali na mwenendo mzima wa siasa-chuki zinazoendelea nyumbani Tanzania. Vyombo vya habari vinaripoti matukio yaletayo simanzi ikiwa ni pamoja na mali za viongozi wa upinzani kuharibiwa, viongozi wa kiserikali kubagua wanachama wa vyama pinzani na kuuwawa kwa mfuasi ambaye ni kiongozi wa kitongozi wa chama cha upinzani. Hali kadhalika inaonekana bayana vyombo vyetu vya usalama vimeegemea upande mmoja wa mizani jambo ambalo mwenye macho aambiwi tazama. Haya yote yanatokea ili hali bado taifa halijapata majibu ya kitendo cha kifedhuli cha kupigwa risasi Mbunge na Raisi wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika. Matukio hayo yote yametokea ili hali viongozi wa kuu wa kisiasa wakiwa wamekaa kimya bila kutoa kauli thabiti, na zenye kuonesha uthabiti kwenye kulaani na kuyapinga matendo-ovu yanayoendelea kwa sasa.

Kinachoonekana ni kwamba upinzani hauvumiliki tena na shughuli za siasa za upinzani ni shughuli hatari kwa usalama, uhai, ustawi na maendeleo ya mtanzania wa kawaida. Je mustakabali wa mtanzania wa kawaida ni upi? Kuacha siasa za upinzani? kuhamia chama tawala? Haya ni mambo ambayo mtanzania wa kawaida anapaswa kujiuliza na kuyafanyia maamuzi kwa wakati uliopo. Kimsingi siasa za upinzani shughuli halali zilizo halalishwa na Katiba na Sheria za nchi yetu. Siasa za upinzani zipo kwaajili ya kuleta fikra mbadala ili kusaidia Taifa kufikia malengo yake kwa kutumia njia sahii na kwa gharama nafuu. Mazingira yanayojengwa sasa ni ya kuua mawazo mbadala. Je mawazo mbadala yakifa ni faida gani Taifa litapata? Wapo watu wenye namna ya ajabu ya kufikiri (strange way of thinking) wakiamini wanayoyaaamua au wanayoyafanya ni sahii wakati wote na hasiwepo mtu wa kuyapinga. Namna hii ya kufikiri ni ya hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu. Lazima ileweke kwamba Taifa hili ni la kwetu sote. Hakuna mtu mwenye hati miliki ya mawazo (namnukuu Comrade Kinana).

Taifa letu limepotoka kwa sasa na hakuna mtu jasiri wakusema hayo maneno hadharani. Tunahitaji statesman, mtu jasiri akemee haya mambo hadharani bila ya uoga na afikishe huo ujumbe kwa viongozi wetu wajue kwamba wanachokifanya leo kitawarudia kesho. Dunia yetu ina mifano hai na yakutosha kwa aina ya viongozi na uongozi kama huu. Tunahitaji kuachana na siasa zinazojenga chuki kwa wananchi wetu. Kama ni lazima maendeleo yaje kwa kuwagawa wanachi basi maendeleo hayo yasubiri. Wananchi wetu kwanza maendeleo baadae. Zipo nchi ambazo zilikimbilia maendeleo na kugawa watu wake kilichotokea hao watu hawawezi kufaidi mabaki ya maendeleo baada ya mataifa hayo kusambaratika. Ni wakati wetu kutafakari maneno na matendo yetu. Tujenge taifa letu kwa maneno na matendo yetu.
 
Back
Top Bottom