A Special message to single mothers

A Special message to single mothers

Lusungo

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
29,524
Reaction score
42,677
Mwisho wa siku Single mother nae ni mwanamke kama wanawake wengine, anayo kila sababu ya kuhitaji kupendwa, kuolewa, na kuwa na mwanaume ampendae.

Yeye kuwa na mtoto hakumfanyi asivutie, asipendwe au aonekane disperate na kufanywa kama chombo cha starehe na wanaume wakware. Ndio, yeye ni mama na ni mwanamke pia, tena mwanamke mzuri ambaye ana a lot of things to offer!

Black bro, mpende kama wanawake wengine na usimuone kama yuko dillema ukatumia huo udhaifu wake. Usimuone kama anatafuta mwanaume wa kumsaidia kulea mtoto wake. Licha ya aliyopitia bado Hajavunjika moyo, she is not a mess!

Ni mwanamke mzuri, anayepambana na hali yake na wala hatafuti huruma. Anampenda mtoto wake kwa moyo wote, na anao upendo wa hali ya juu kwa mtu ambae ataonesha kumthamini. Mpende, na jaribu kuelewa mazingira yaliyomfanya mpaka akawa single mother, ukielewa hilo utajikuta ukimheshimu kwa yale aliyopitia!

Uhisi uzuri wake, muone namna anavyopenda it is beyond her motherhood, mtazame namna anavyomkuza mtoto wake, namna anavyomlea mwanae, inaonesha namna yeye binafsi alivyo. Ni rahisi mno kumpenda, ni rahisi mno kumpenda mtoto wake.

Single mother, ninyi ni wazuri. Mna moyo wa kulea; naamini siku moja mtakuja kuwa wake wazuri kwa mwanaume atakaetambua namna mlivyo!!

Let us Stand ovation to all single mums [emoji817][emoji817]

NB: Natoa zawadi ya iphone 7 Space gray 128GB kwa single mother atakaetoa ushuhuda mzuri kupita wote....
 
Hivi single mother's nini mpk mtu ajihisi ni inferior?!!
Mbona ni vitu vya kawaida sana ktk maisha!!

Mimi niseme ukweli wangu sehemu pekee niliyoona single mothers wanadharaulika ni jf!!ila katka maisha ni vitu vidogo mnoo!na wanaolewa kama wengine tu!mifano ipo hai mingi tu!

Mungu ndo anajua mwenza wa mtu ktk haya maisha
 
Kasome uzi wa Mama sabrina unasema " wanaume sasa mtuacheni jamani".
 
Binam asante kusema hayo lakini mimi wala huwa sijali kabisa nashangaa wanaoumiaga maana nikimuona mwanangu napata raha sana
Kuweni na mioyo migumu msitishwe na wanaume wenye masimango na wabinafsi,tena kama mwanaume hataki mwanao piga chini
 
Sijui Cha Kuandika,siku nkiamua nitaandika,single moms Mungu awape moyo na msijione mko tofauti,nyinyi ni wa thamani zaidi,usikubali kuyumbushwa hao wanaowanyanyapaa kimoyomoyo wanawakubali
 
Sijui Cha Kuandika,siku nkiamua nitaandika,single moms Mungu awape moyo na msijione mko tofauti,nyinyi ni wa thamani zaidi,usikubali kuyumbushwa hao wanaowanyanyapaa kimoyomoyo wanawakubali

Tunawapenda Single mothers ila kiukweli wengi wao wanashida. Mifano tunayo yaani kwenye kauli tu utajua she is hell of a problem no man can bear.
 
Back
Top Bottom