A Missing Soldier

A Missing Soldier

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,190
Reaction score
34,526
RIWAYA: C.O.D.EX 4
(A Missing Soldier)
MTUNZI: Frank Masai
MAWASILIANO: 0717 738973

SEHEMU YA KWANZA.

“Tulikuwa ni watu kama watu wengine. Tuliwapenda wazazi wetu kama watoto wengine. Tuliishi na kufurahi kama watu wengine. Na tukapata malezi bora kama watoto wengine. Lakini mambo yalikuja kubadilika baada ya kuingia mikononi mwa Wanasayansi. Watu ambao hawajali uwepo wa nyama miili mwetu na mzunguko wa damu katika mishipa ya damu. Wakapandikiza kemikali zao kwenye damu zetu, wakatengeneza miili yao kwa kutumia nyama zetu. Na hatimaye tukaitwa wanajeshi. Na tena wanajeshi wenye uwezo wa kipekee duniani. Maisha ni kama upepo, ukiamua kubadilika, hubadilika bila kuambiwa ubadilike. Maisha yetu yakabadilikia hapo, na sasa tukaitwa wanajeshi hatari.”

NEW YORK, MAREKANI.

Kulikuwa ndani ya jengo kubwa na lenye mwanga mkali kila mahali. Watu mbalimbali walioenekana ndani ya mavazi ya kitabibu huku wamekamata Ipad za gharama ambazo walionekana wakizichezea chezea na wakati huohuo wakiangalia miili ya watu iliyokuwepo ndani ya majokofu yenye matirio ya kioo na ndani yake kulikuwa na maji yaliyojaa. Binadamu waliokuwepo humo, waliingiziwa mipira midomoni na puani na walibandikwa vitu fulani vifuani mwao kwa ajili ya kupima mapigo yao ya moyo.

“We called them, New Generation Soldiers, Sir (Tunawaita Wanajeshi wa Kizazi Kipya, Mkuu)” Aliongea bwana mmoja ambaye alikuwa nje ya maabara ile lakini aliweza kuona kila kinachoendelea kupitia kioo kikubwa kilichokuwa ndani ya jengo lile.

“Are you sure about your generation? (Unahakika na kizazi chako)” Bwana mmoja mwenye suti na mwenye asili ya Kimarekani, alimuuliza yule tabibu aliyekuwa kasimama pembeni yake akijinadi juu ya wale wanajeshi waliokuwa ndani ya majokofu zaidi ya hamsini.

“Yes Prime Minister. These are the best soldiers we ever created before. They can fight for so long without tired. (Ndio Waziri Mkuu. Hawa ni wanajeshi bora kuliko tuliyowahi kuwatengeneza hapo kabla. Wanaweza kupigana kwa muda mrefu bila kuchoka)” Akajibu yule tabibu ambaye alivaa kitambulisho kilichoonesha sura yake, jina na cheo chake. Bwana mmoja aliyekuwa na asili ya Kimarekani, na ilionekana kuwa kaongozana na Waziri Mkuu, aliangalia kitambulisho hicho kabla hajaongea.

“Tutegemee nini katika wanajeshi wako Dokta Ice Mujo.” Akauliza yule bwana aliyeongozana na Waziri Mkuu kwa lugha ya Kiingereza.

“Maajabu ya dunia. Wanajeshi watano pekee, wanaweza kuingamiza Urusi yote ndani ya saa moja. Tumewapachika uwezo wa kipekee na silaha nzito wanazo vichwani mwao.” Alijibu Dokta Ice.

“Silaha gani hiyo Dokta?” Akauliza tena bwana aliyeongozana na Waziri Mkuu.

“Nyuklia bombs. Kila mwanajeshi hapo, kabla hajaenda mapambanoni, tunampandikiza chip ndogo ambayo inaweza kuruhusu mabomu ya nyuklia yalipuke mahali ambapo yatapandikizwa. Kati ya wanajeshi watano tunaoweza kuwatuma, wawili ni lazima wawe na mabomu ya Nyuklia. Hawa ndio wanauwezo wa kipekee.” Alijibu Daktari.

“Wanauwezo gani?” Akauliza Waziri Mkuu.

“Angalia hii.” Akamsogezea Ipad. Kisha akabonyeza sehemu ya video na hapo wakaanza kuonekana wanajeshi wakifanyiwa majaribio. Picha ambayo iliwafanya wale mabwana waliokuja pale kushangaa, ni mlipuko mkubwa uliotoka kwenye mwili wa mwanajeshi mmoja, halafu baada ya mlipuko huo, yule mwanajeshi alitoka ndani ya moto akiwa anawaka lakini akitembea bila wasiwasi… Baadae moto huo unazima, na mwanajeshi anaoekana hana makovu yoyote ya moto licha ya nguo zake zote kuungua.

“Hatari sana hii.” Aliongea waziri mkuu huku katabasamu.

“Hiyo ndio C.O.D.EX improved chemical.” Daktari alijigamba kwa mbwembwe.

“Kwa hiyo ni ile C.O.D.EX ya wale wanajeshi wengine?” Aliuliza bwana yule aliyeongozana na Waziri Mkuu.
“Ndio Waziri wangu wa Ulinzi.” Kwa tabasamu pana alijibu Dokta Ice.

“C.O.D.EX ni nini?” Akauliza Waziri Mkuu.

“Ni kifupisho cha maneno haya, CINDREX OLTIVIASO DECA ENDROLINE X. Ni chemikali zilizobuniwa miaka kumi nyuma na walitengenezwa wanajeshi kadhaa ambao walisumbua sana CIA na FBI. Baada ya kujua kemikali hizi, CIA waliweza kuharibu maabara yote ya kutengenezea wanajeshi hawa. Sasa hivi ndio tumepewa kibali cha kutengeneza silaha kupitia kemikali hizi.” Alijibu Daktari.

“Kuna tofauti gani kati ya wanajeshi hawa na wale wa miaka kumi iliyopita? Hawawezi kuleta madhara kama yale?” Aliuliza Waziri wa Ulinzi.

“Hapana. Hawawezi fanya hivyo. Tatizo kubwa la wale waliyopita, hawakuwatoa kumbukumbu wale waliowatengeneza, hivyo ilikuwa rahisi kwa zile kemikali kurudisha kumbukumbu baada ya kuanza kuisha. Hilo likaleta tatizo kwa baadhi ya wanajeshi ambao kumbukumbu ziliwarudia.” Akajibiwa.

“Okay. Kwa hiyo hawa hawana kumbukumbu?” Akauliza tena Waziri wa Ulinzi.

“Ndio. Kabla hatujawaingizia C.O.D.EX, tulihakikisha kwanza tunafuta kumbukumbu zao zote za maisha yaliyopita. Tuna uhakika tumefanikiwa katika hilo.” Alijibiwa na daktari.
Waziri wa Ulinzi akaangaliana na Waziri Mkuu kisha kwa ishara fulani walipeana kuonesha kuwa wamekubaliana na ile kazi ya C.O.D.EX.

“Sawa Dokta. Ila kwanza ni lazima tufanye majaribio na silaha zako.” Waziri wa Ulinzi aliongea na kumpa nafasi dokta naye aongeze jambo kama analo.

“Mmepanga wapi kufanya majaribio yenu?” Akauliza Dokta.

“Iraq na Iran.” Akajibiwa na dokta akaonesha kukubaliana na majibu hayo.

“Ila kuna jambo moja ambalo tumelipandikiza kwenye miili yao.” Akakumbusha daktari.

“Lipi hilo?” Akaulizwa.

“Hawana huruma hata kidogo. Kitendo cha huruma kwao kimepita kushoto. Kwa hiyo hayo majaribio, tujaribu kuyafanya mbali na raia.” Akaongea dokta.

“Hamna shida.” Akajibiwa na Waziri wa Ulinzi kwa kifupi.
Baada ya maongezi hayo marefu, wale viongozi wa serikali ya Marekani, walianza kuondoka eneo lile huku nyuma wakifuatiwa na walinzi wao muhimu kabisa.
****
BAADA YA WIKI MBILI.

Vyombo vya habari duniani vilikuwa vinatangaza kuhusu Iran kuvamiwa na mitambo yake ya nyuklia kuharibiwa vibaya na wakati huo mateka wa Iraq walisemekana kuwa wamekombolewa na wanajeshi wa jeshi la Marekani lakini hawatambuliki ni wapi walipo. Habari zilikuwa zimezagaa na kuzusha maswali kadhaa kwenye vichwa vya habari na watu wote kwa ujumla.

Vyombo vya habari viliuliza kuhusu wanajeshi hao na Waziri Wa Ulinzi alithibitisha uwepo wa wanajeshi hao na kuahidi kuwa, Marekani itakuwa na nguvu kubwa kuliko nchi yoyote duniani.

Wakati hayo yanaendelea, daktari mkuu wa ile maabara alikuwa anatazama na kusikiliza vyombo vya habari kila kukicha. Jambo ambalo hakuwaambia wale viongozi, ni uwezo wa wale wanajeshi kuchukua matukio yote kwenye chipu iliyokuwa imepandikizwa vichwani mwao kwa ajili ya kuwatuma wafanye mambo fulani.

“Wajinga sana hawa. Niliwaambia wasifanye majaribio kwenye makazi ya raia wema. Matokeo yake wamewaua mateka wote. Washenzi sana. Natakiwa kufanya jambo moja muhimu sana kabla sijaondoka hapa.” Alijiwazia Dokta Ice na hapohapo akaifata kompyuta yake iliyokuwa katika ofisi ndogo kwenye chumba chake na kuanza kusoma mambo kadhaa kwenye mafaili yaliyokuwepo kwenye kompyuta hiyo.

Kesho yake ilikuwa Asubuhi ya Jumapili yenye bashasha nyingi sana. Dokta akiwa anajua wazi kabisa kuwa siku hiyo ni ya mapumziko kwake, alitoka ndani ya nyumba yake akiwa kakamata mkoba wenye makaratasi kadhaa, kisha akapanda gari lake la gharama na kuelekea zilipo ofisi zao.

Huko aliamrisha baadhi ya wafanyakazi waondoke kwa sababu alikuwa na kazi nyeti ya kufanya bila wao kuijua. Alipofanikiwa kuwatoa, akafungua jokofu moja ambalo lilikuwa tofauti na yale mengine. Lenyewe lilikuwa halioneshi na lilifanana na lile la kuhifadhia maiti. Alipolifungua, akaonekana muafrika mmoja aliyekuwa kafumba macho yake kama marehemu na mvuke ukimtoka kwa sababu ya kuganda kwa mwili wake.

Ice Mujo, akabofya vitufe kadhaa kwenye lile jokofu nalo likaanza kuvia maji ambayo yalikuwa ya moto. Maji hayo yakayayusha barafu iliyopo mwilini mwa muafrika yule na kumfanya awe laini na mwenye hali ya umoto.

Akabofya tena vitufe kadhaa kwenye ipad yake. Vitu fulani vikatokea angani na kisha vikashuka hadi kwenye lile jokofu. Vikazama ndani ya maji na kumkamata yule bwana, kisha vikatoka naye na kumuweka kwenye lile jokofu lingine ambalo lilikuwa linauwezo wa kujazwa maji pamoja mitambo ya kumuwezesha binadamu kupumua.

Dokta Ice, akambandika vile vifaa vya mapigo ya moyo pamoja na mipira maalumu kwa ajili ya kupumulia. Alipomaliza, akafunga lile jokofu na kufungulia maji yaliyoanza kujaa ndani yake.

Akasogea kwenye kompyuta inayoonesha hali ya yule binadamu muafrika. Akaanza kuruhusu kemikali aina ya C.O.D.EX ianze kuingia mwilini mwa yule bwana. Kilikuwa ni kitendo cha dakika kumi pekee kukamilisha tendo lile na lilifanikiwa kwa sababu muafrika yule alianza kupumua akiwa ndani ya jokofu lile.

Kwa haraka, akabonyeza tena vitufe kwenye kompyuta na hapohapo maji yakaanza kupungua na baada ya kuisha yote, yule bwana alijikuta akisogezwa nyuma kwa kasi na kisogo chake kikagota nyuma ya kidirisha kidogo ambacho kilifunguka na hapohapo mwanga fulani mwekundu ukaanza kupitia sehem hiyo ya kisogoni. Kisogo cha yule bwana kikafunuliwa kidogo kwa kutumia ule mwanga ambao ulitumika kukata sehemu hiyo.

Kiasi kidogo cha ubongo kikatolewa, na baada ya hapo, Dokta Ice alifungua mkoba wake na kutoa Diskette na kuchomeka kwenye sehemu maalumu ya kwenye komyuta aliyokuwa anaitumia. Ikaanza kusoma harakahara na baadaye ikaandika ‘loading succefully, 100%’. Dokta akashusha pumzi na kisha akabofya kitufe cha Enter. Hapo kule kwenye kisogo cha yule bwana, ikapandikizwa chipu na kisha ile ngozi iliyotolewa kisogoni, ikapachikwa na kupitiwa na mwanga ule mwekundu. Pakarudi vilevile.

Yule muafrika akatoka kule alipobananishwa na kusogezwa katikati ya lile jokofu. Dokta akabonyeza tena vitufe kadhaa kwenye kompyuta yake, yule bwana akaanza kuzunguka taratibu kwenye lile jokofu kw a dakika zipazo kumi. Aliposimama, kompyuta ikaongea kwa sauti ya kike, ‘upgrade complete’. Kisha maji yakajazwa ndani ya jokofu na dokta akawa kamaliza kazi ambayo alipanga kuifanya jana yake.

Dakika ishirini mbele, akamtoa mtu yule kwenye jokofu na kumuingiza kwenye mashine nyingine iliyoanza kuupembua mwili wa muafrika yule hadi ikaridhika na kutamka maneno mengine ya kiingereza, ‘Scan Complete’.

Dokta Ice akatabasamu baada ya kufungua mashine ile na yule muafrika kusimama mwenyewe na kumtazama Dokta.

“Nipo tayari kukutumikia mkuu.” Aliongea bwana yule kwa Kiingereza na kumfanya Dokta kuzidi kutabasamu.

ITAENDELEA.
 
Hii simulizi imeruka baadhi ya sehem msome hivo hivo eeeh kuanzia sehem ya saba ndio mtiriiko unaenda sawa
 
RIWAYA: C.O.D.EX 4
(A Missing Soldier)
MTUNZI: Frank Masai
MAWASILIANO: 0717 738973

SEHEMU YA TATU

Idris alipomuangalia Soldier One, alimuona akijivaa vaa taratibu ili asimame na hilo likawa kosa lake kwani Idris alimchota mtama mzito na jamaa yule alirudi chini akidondokea kisogo na kabla hata hajajua la kufanya, soli ngumu ya kiatu cha Iris ilikita kwenye mdomo wake na kuzidi kumpoteza kabisa.

Akiwa kasimama katikati ya wanajeshi wale wawili. Alisikia mlio wa simu toka mle ndani. Kwa haraka akaanza kukimbia kuelekea dirishani na kupasua kioo kilichokuwa kimebakia baada ya kupasuliwa mara ya kwanza na wale C.O.D.EX soldiers. Akajitupa nje na hapo helikopta kubwa ilitokea angani lakini helkopta hiyo ilijikuta inapoteza muelekeo wa Idris baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye nyumba ya Dokta Ice.

Akili zao zikawaza kuwapoteza wale wanajeshi wawili na kumsahau kabisa Idris ambaye alidandia pikipiki moja kubwa iliyokuwa nje ya geti la Dokta Ice. Akaingiza gia, na kuanza kutokomea toka eneo lile akiwaacha wale wababe wengine wakihaha ndani ya jumba la Dokta Ice.

ENDELEA.

Safari ya Idris iligotea kwenye hotel moja ya kifahari Jijini New York. Akaingia huko na kuchukua lift ambayo ilimpandisha hadi ghorofa ya juu kabisa na huko alikutana na Dokta Ice ambaye muda mwingi alikuwa kasimama kwenye dirisha la chumba alichopanga.

“Unajua ni sababu gani nimekuachia wewe huru?” Dokta Ice aliongea baada ya Iris kuingia na kusimama kiheshima nyuma ya Ice.

“Hapana Mkuu.” Akajibu kikakamavu kama wafanyavyo wanajeshi.

“Ni kwa sababu dunia haina usawa kabisa. Dunia hii inamambo ambayo ukiingia kiundani, haitendi vile tunavyotaka itende.” Akaanza kwa hasira kidogo Dokta Ice. “Wametengeneza….. Hapana, tumetengeneza wanajeshi, lakini wanajeshi hawa ni kama silaha. Hawana huruma hata kidogo. Kabla hatujaingia wazo la kuwawekea chipu za huruma, wamewachukua baadhi ya wanajeshi na kuwapeleka huko wanapopajua. Huko kuna baadhi ya mateka wakiwa watoto na wanawake wameuawa kikatili sana na hawa wanajeshi. Mwenye roho kama mimi, siwezi kuvumilia. Nimekutengeneza wewe ili kidogo wafahamu kuwa nyie si silaha za maangamizi bali pia ni wokovu kwa wasiojiweza.” Alitabanainisha Dokta Ice.

“Umeoa Mkuu?” Akauliza swali ambalo Dokta Ice hakulitegemea. Akamuangalia mwanajeshi wake kisha akatabasamu kwa masikitiko.

“Yeah! Nilioa na nilipata mtoto mmoja wa kike lakini niliwapoteza kwa ajali ya gari miaka kumi iliyopita. Toka hapo sikuwa na haja ya kuoa tena.

“Ilikuwaje ukawapoteza kwa ajali na wewe ukabaki?” Akauliza tena Idris Iris.

“Ni kama wewe navyotaka kufanya. Nilikuwa nawatorosha kwa sababu CIA walikuwa wananiwinda sana kwa ajili ya kutengeneza upya folmura ya C.O.D.EX. Sasa ili niepushe familia yagu kuingia matatizoni, nikataka kuwahamisha na kuwapeleka Afrika.” Alihadithia Dokta Ice.

“Afrika. Tanzania tena au wapi?” Akamuuliza swali lingine.

“Ndio. Nilitaka kuwapeleka Tanzania kwa sababu kule pana amani na wanaurafiki mkubwa na nchi zenye nguvu duniani hivyo kama Marekani wakiamua kuwapiga Watanzania, wajue watakuwa vitani na Cuba, China, Urusi na nchi zote za ujamaa.”

“Ajali ilikuwaje?” Akaendelea na maswali Iris.

“Mke wangu ndiye alikuwa dereva. Mimi nilimwambia akimbie na nikabaki nawazubaisha CIA kwa gari lingine. Walipogundua kuwa mke wangu anakimbilia uwanja wa ndege, ndipo wakatuma helikopta ambayo iliifutilia mbali familia yangu kwa kuizinga kwa taa zake na kisha kulipotezea muelekeo gari alilokuwa anaendesha mke wangu. Likaingia darajani na kupinduka huko. Likawaka moto na baadae kulipuka.”

“Mwanao alikuwa na miaka mingapi kipindi hicho?” Swali lingine toka kwa Idris. Dokta akamtazama kwa macho ya masikitiko kisha akamtaka mwanajeshi wake akae kwenye kitanda cha hotel ile.

“Alikuwa na miaka tisa pekee,” Dokta Ice akamjibu na kisha akaendelea. “ Hamna kitu kinachouma kama kumpoteza mtu au watu unaowapenda. Hadi leo inaniuma sana. Nilitaka kujivika roho ya kikatili na kulipa kisasi kwa watu ambao hawana hatia, lakini moyo umekataa kabisa baada ya kushuhudia mauaji ya kutisha ya kule Iraq kwa wale mateka.

“Samahani na pole kwa hilo mkuu. Lakini swali la mwisho, mkeo yeye alikuwa anafanya kazi gani?” Akaulizwa tena.

“Alikuwa ni daktari mwenzangu. Baada ya mimi ni yeye. Hata hii folmura ya C.O.D.EX ni mimi na yeye ndio tuliijenga lakini kulikuwa na kashikashi fulani ambazo zilinifanya nitake kumtorosha mke wangu. Hapo ndipo yakatokea yaliyotokea.” Akajibu swali kwa ufasaha kabisa Dokta Ice.
Macho ya Idris yakaonesha yanajambo la kutaka kuongea lakini hakutoa nafasi ya kuyatoa ambayo kayahisi toka moyoni mwake.

Japo Idris Iris alikuwa ni mwanajeshi wa kutengenezwa, lakini yeye aliumbwa kiufasaha sana na Dokta Ice. Yeye aliweza kuhisi yale ambayo kila binadamu anaweza kuyahisi. Lakini yeye hakuwa sana na binadamu kwa sababu alikuwa na kiruhusuji au activetor maalumu ya kulipua mabomu ya nyuklia. Mbali na hapo, yeye hakuwa sawa na wale wanajeshi wengine ambao wanaweza kuungua mavazi pekee. Yeye aliweza kuungua hadi kuisha kabisa mwili wake na kubaki vyuma fulani vilivyopandikizwa mwilini mwake kwa kemikali za C.O.D.EX ambazo ndizo zinamfanya aungue mwili mzima na baadae kemikali hizo, huanza kuujenga mwili wake kwa kutengeneza ngozi mpya. Tendo hilo huchukua dakika moja pekee.

“Unatakiwa kuondoka usiku huu Idris. Utashukia Dar es Salaam. Na hapo utakuta ndege maalumu kwa ajili yako, nayo itakupeleka hadi Arusha. Huko napo utakuta gari maalumu kwa ajili yako, nalo litakuchukua hadi kwako. Huko ishi kwa amani.” Aliongea Dokta Ice huku akikusanya baadhi ya vitu na kutumbukiza kwenye mkoba maalumu wa nguo.

“Kwa nini mimi lakini?” Akauliza Idris.

“Ukifika sehemu yoyote, fungua kompyuta hii, kisha tazama mafaili pamoja na video kadhaa ambazo zipo humo. Sina muda wa kukuhadithi kila kitu kwa sasa. Muda si mrefu C.O.D.EX wanatuvamia hapa.” Alijibu Dokta Ice na kulazimika kuanza kumzoa zoa Idris ili waondoke mle ndani.
Bomu lililolipuka nyumbani kwa Dokta Ice, ni bomu ambalo lilitegwa na dokta huyu mwenyewe. Ni bomu la kawaida ambalo halikuwadhuru wale wanajeshi. Hivyo baada ya kuokolewa, wale wanajeshi walipewa mavazi mapya tayari kwa kurudi kuwasaka Ice na Iris.
****
Saa mbili usiku, gari moja la kifahari lilisimama kwenye jiji la maraha nchini Marekani. Jiji la Las Vegas. Lakini kwa bahati mbaya gari hilo halikuwa limekuja kushangaa raha za Las Vegas na badala yake, alishuka Idris na Ice na kisha kuchukua treni ya umeme ambayo iliwapeleka hadi uwanja wa ndege. Huko Idris aliagana na Dokta Ice ambaye baada ya kuhakikisha kuwa mwanajeshi wake amekwishakwea ndege, akarudi haraka kwenye treni inayorudi mjini ambapo alliacha gari lake.

Idris akiwa katulia ndani ya ndege kabla haijaanza kuondoka, alichungulia nje kwa mara ya mwisho kabla ya kuanza safari ya kuiaga Marekani.

“America, Land of Opportunities. Godbless America. (Amerika, nchi/ardhi ya bahati/nafasi. MUNGU ibariki Amerika)” Idris aliongea maneno hayo akimaanisha kuwa Marekani ni nchi ya bahati au nafasi. Yaani alimaanisha kuwa, yeyote atayeishi Marekani basi anauwezo mkubwa wa kutoka kimaisha. Kifupi, nchi ya Marekani kama ukijishughulisha, basi unauhakika wa kuishi kama mfalme. Hamna ambaye anajishughulisha Marekani kisha awe fukara. Idris alilitambua hilo.

Baada ya nusu saa, ndege ilikuwa angani na Idris aliamua kutoa kompyuta mpakato aliyokabidhiwa na Dokta Ice. Akaifungua na kisha alianza kusoma mafaili kadhaa yaliyomo humo lakini kwa bahati mbaya, hakuwa akielewa ni nini hasa yalikuwa yanamaanisha. Akaamua kufungua video zilizomo humo, huko ndipo alipotulia na kuanza kuumia moyo wake.

“Happy Birthday to you… Happy Birthday To You…. Happy Birthday Dear Best, Happy Birthday To You.” Wimbo huo ulikuwa unaimbwa na watu kadhaa huku mwanaume mmoja mwenye nywele nyingi akiwa kakamata keki akielekea ilipokuwa meza kubwa.
Wakati anaelekea huko kwenye meza, mchukua video ile alianza kuwachukua watu waliokuwa wamehudhuria kwenye sherehe ile ya siku ya kuzaliwa.
Mama mmoja mwenye asili ya weusi, alionekana mwenye furaha sana na mchukua video alikuwa anamchukua kwa makini zaidi kwani mama yule alienda mahali hadi alipokuwa amekaa mtahiniwa wa sherehe ile. Hapo Idris akashtuka baada ya kumuona mtoto aliyekuwa anasheherekea miaka yake mitano ya kuzaliwa.

Alikuwa ni mtoto mweusi kama mama yake. Na kilichomfanya ashtuke ni ule muonekano ambao ulionekana kama yeye. Japo yeye alikuwa mkubwa kulikoni yule kwenye video, lakini hakutilia shaka kabisa kuwa yule kafanana naye. Akabonyeza stop na video ile ikasimama.

“Huyu ni mimi, lakini anaitwa Best, na mimi ni Idris.” Akajiwazi na kwa haraka akafungua mafaili ambayo hapo mwanzo aliyafunga kwa sababu hakuyaelewa.
“Best Boucher. Kazaliwa tarehe….” Akaanza kusoma yale mafaili kwa makini zaidi.
Baba yake Dokta Boucher, alikutwa kajinyonga ndani ya chumba chake baada ya kumuua mkewe. Mtoto wao alikutwa kajificha kwenye zizi la farasi na jukumu la kulelewa alipewa Dokta Ice ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Dr. Boucher.
Best alipotimiza umri wa miaka kumi na saba. Alipotea katika mazingira ya kutatanisha na baadaye taarifa zilitoka kuwa amekutwa kwenye fukwe za Miami amefariki.

Ni kifo cha utata sana kwa sababu Dokta Ice hakuwa tayari kufanya mazishi hayo wala kutaka maiti ionekane. Na yeyote aliyethubutu kuhoji kuhusu mwili wa Best, alipewa kilema cha maisha na watu wasiojulikana.

Katika vifo vya Dokta Bouncher na Mkewe ambaye alikuwa ni Mwanasheria, iligundulika kuwa mke wa Bouncher hakuuawa na mumewe na wala mumewe hakujinyonga. Mwili ulivyopimwa, kulikutwa na sumu kali sana ambayo leo hii wanaiita C.O.D.EX. Kemikali hii kwa maiti huwafanya wazinduke na kuwa watu wenye nguvu sana, lakini kwa wale wazima huwapotezea uhai wao haraka sana kwa kuwatoa damu kwenye kila tundu linalopatikana kwenye miili yao.
Mtu aliyefanya uchunguzi huo alikutwa maiti ndani ya ofisi yake na taarifa hizi zilizuka miaka mitano mbele kwa mtoto wa yule aliyefanya uchunguzi kuziweka hadharani. Naye hakuchukua muda, akapigwa risasi siku moja wakati anatoka mahakamani kusimamia kesi ya mtuhumiwa fulani huko Marekani.

Vifo vya familia ya Boucher vilijaa utata pekee na kila aliyejaribu kuvifuatilia alikutwa anakilema cha maisha au mfu. Hata mawakili wakubwa duniani, walikwishakataa kuzungumzia kesi ya Bouncher.

Idris akaendelea kuyasoma maelezo muhimu ndani ya mafaili yale ya kwenye kompyuta. Aliporidhika, akarudi kwenye video zilizopo. Akafungua video nyingine iliyokuwepo mbele ya kioo cha kompyuta.

“Dokta Ice. Tunakaribia kupotezwa. Mimi na familia yangu tunapotezwa muda si mrefu. Naomba umtunze mwana wetu. Nakuomba Dokta. Ukumbuke pia ile formula mpya C.O.D.EX.” Video hiyo iliongea hayo na picha ya Boucher ilionekana akiwa na wasiwasi mwingi sana, kwani aliangalia huku na huko wakati anayaongea hayo. “Nimemficha mwanangu kwenye zizi la farasi, utamkuta huko. Mlee vema kama…..” Hakumaliza maneno yake Dokta Bouncher, mlango wa nyumba yake ukafunguliwa kwa kishindo cha bunduki.
Kwa haraka akakimbilia kwenye kabati moja lililomo mle ndani na kufungua kisha akatoa gobole, lakini alikuwa amekwisha chelewa sana. Mwanajeshi mmoja mkubwa wa mwili alikuwa nyuma yake, na Bouncher alipogeuka tu! Akakuta na kabali nzito na kunyanyuliwa juu huku akiliachia gobole lake na kuanza kutapatapa.
Hayo yote yaliendelea kuonekana kwenye video ambayo ilikuwa inacheza kwenye kompyuta mpakato ya Idris.

ITAENDELEA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom