A Million Dollar Question...

A Million Dollar Question...

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,279
Reaction score
7,681
========================Je, Ben Saanane atatajwa mahakamani???========================

Imefahamika kuwa zaidi ya kuwa na tuhuma za kurekodiwa akipanga utekaji nyara, Bw. Lwakatare pia anatuhumiwa kutoa sumu kwa lengo la kudhuru binadamu.

Hakimu wa Mahakama ya Kisutu alielezwa kuwa mnamo tarehe 28.12.2012 Bw. Lwakatare akishirikiana na Ludovick walitoa sumu kwa lengo la kumdhuru nd. Dennis Msacky. Jambo hilo walilifanya katika mtaa wa King'ong'o huko Kinondoni Dar es Salaam.

Katika mlolongo wa kesi hii tutaweza kujua sumu hiyo anashutumiwa nani alipewa ili kuifikisha kwa mlengwa. Na iwapo watakutwa na hatia pengine itakuwa chanzo cha kujua kama ni mara ya kwanza jambo hili linafanyika au lilishawahi kufanyika awali.

Ikumbukwe kuwa tuhuma za kutumika sumu ndani ya chadema sio mpya. Kulikuwa na tuhuma kama hizi zikilenga kumduhuru kiongozi wa chama hicho kwa kumtumia kijana aliyepewa kazi hiyo maalum. Hata hivyo tuhuma za awali ziliishia kwenye malumbano yasiyo rasmi na hazikufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Je, kijana huyo ataingia kwenye mlolongo wa kesi hii? - This is a million dollar question...

==========================================================================================

Kumbukumbu 1...:::::

Mnamo tarehe 20 Desemba 2012 kulikuwa na thread inayoelezea jambo hili:

"KUHUSU BEN SAANANE NA KUTUMIKA KUMUUA ZITTO KABWE

Wana jf,Nakili wazi hili swala lilitokea mnamo mwezi wa 5 mwaka 2012 tukiwa Lunch time hotel external kwenye mazungumzo ya kawaida(ambavyo ben saanane anaita ni vikao vya kuhujumu chama). Siku ya tukio tukiwa meza moja na Ben Saanane mkono wake wa kushoto alifunga bandeji akidai ameumia mkono(nakumbuka). Kwa babati mbaya sana katika maongezi yale Ben alilewa pombe (alikuwa anakunywa bia(kilimanjaro). Kulewa kwake pombe alijisahau na kutoa bahasha ya kaki yenye fedha, ndani ya bahasha ile wakati wa kutoa fedha alipe huduma ya chakula na vinywaji alidosha karatasi ya nailoni ndogo ikiwa na unga mwekundu ndani.

Tulimuuliza ni nini hicho akadai ni kuberi,na kuing'ang'ania tusifungue(aliyekiokota ni mwampamba).Lakini Mwampamba aligoma kumpa na kudai lazima ifunguliwe pale pale.

Ben saa nane akiwa katika hali yake ya kulewa alifura kwa hasira kutaka arudishiwe ilekaratasi,haliiliyopelekea uvunjifu wa amani pale lunch time hotel.Mwampamba aliondoka na mzigo ule kwa kukimbia nao, usiku ule Ben alitafutana na mwampamba hadi nyumbani kwake(temeke) akidai huo mzigo(ikumbukwe mwampamba na mm nimeishi kwake na nikaka yangu) . Lakini katika hali ya kusikitisha ben aliomba mzigo ule usiende mbali na kuahidi atasema kweli kile ni nini.

Ben saanane alikili wazi kwamba ile ni sumu lakini anapeleka nyumbani kwa ajili ya kuulia panya, Swala hili halikuishia usiku ule,ben hakufanikiwa kupata mzigo ule kesho yake asubuhi(jumapili) alikwenda kumsihi mwampamba ampatie mzigo.

Sharti lilikuwa aseme ni nini kwasababu huwezi kuwa na sumu eneo la starehe kama pale hotelini huku akisisitiza kuonana na zitto ambaye alisafiri usiku ule kwenda marekani bila kuonana na yeyote kati yetu?

Ndipo Ben saanane akakili ile ni sumu akilenga kumpatia zitto akiwa ametumwa na Dr.slaa
.Tulihamaki kusikia kile kitu(hapa tulikua tabata reli stand tukisubiri usafi).Nilimuuliza uthubutu wake wa kufanya kitu kama hicho na kwanini afanye unyama huo,akadai ametumwa Kisa kikiwa ni zitto kumsakama dr.slaa ndani ya vikao vya chama.

Swala hili lilifika mbali kwa kuwekeana mipaka ya kula vyakula mahotelini na kutoshirikiana tena katika ushikaji wetu kama masalia.

Lakini urafiki wetu na ben uliendelea na tukayamaliza haya mambo kishikaji kawa wanasiasa vijana,Ben alifurahi sana ndipo akaja na wazo la PM7 kama movement ya kuendesha harakati huru ndani ya chadema zikilenga kukataa kutumika na viongozi wa chama kama ben alivyotumika kutaka kumuua zitto.
"

Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-dr-slaa-kwenye-siasa-za-juliana-shonza.html

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Kumbukumbu 2...:::::

Majibu ya Zitto

"
quote_icon.png
By Zitto

Ninasikitika sana kuona wanachama wa CHADEMA wanavyoweza kutumika kwa maslahi ya kundi fulani kuharibu heshima ya viongozi wao mbele ya jamii.

Ninaomba ndugu Ben Saanane aje hapa jukwaani kuthibitisha maelezo haya ya Bwana Mamuya kutoka Arusha. Mimi binafsi nikikutana na Ben Saanane leo naweza kupishana naye maana sijawi kumwona, wala kukutana naye. Ndugu Ben Saanane nimewasiliana naye kwenye simu mara mbili au tatu kuhusu masuala yake ya kitaaluma au pale alipohisi kuonewa ndani ya chama. Sijawahi kukutana naye hata siku moja. Kama nasema uwongo yeye binafsi aje hapa kukanusha.

Mimi pamoja na wenzangu tumejenga chama hiki mpaka hapa tulipofika. Tumeingiza watu kwenye chama hiki ili kwa pamoja tuweze kujenga asasi imara kabisa ya kidemokrasia. Chama hiki kina damu yangu. Chama hiki kina muda wangu. Chama hiki kina jasho langu. Nitakuwa mtu wa mwisho kusaliti chama hiki. Sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa tofauti na CHADEMA. Sitarajii kuwa mwanachama wa chama zaidi ya CHADEMA.

Ninawasihi wana CHADEMA tuache propaganda za kuchafuana. Nguvu kubwa inayotumika kumchafua Zitto ielekezwe kwenye kujenga taasisi imara ya CHADEMA, chama chenye demokrasia, kisicho na upendeleo, chenye uwakilishi wa kitaifa na chenye kuthamini nafasi ya kila mwanachama.

Mamuya, mara kadhaa umetaka kuniona kwa sbaabu nisizozijua na imekuwa ikishindikana. Unapata dhambi kubwa sana kumwaga sumu unayomwaga kwa mtu usiyemjua wala hujawahi kukutana naye.Acha kutumika. Jisimamie. Simamia chama.

Vijana, wote wa vyama vyote, siku zote simamieni misingi (principles) na sio kusimamia watu. Watu sio mawe. Mtaja juta. Misingi inadumu. Watu hawadumu. Acheni kuramba miguu ya watu. Simamieni misingi ya chama. Misingi ya nchi yetu. Misingi ya demokrasia. Kataeni kutumika.

Angalieni, wanaozungumzia sana usaliti waweza kuta ndio wasaliti wakubwa. wanazungumzia usaliti kama 'defensive mechanism'.

Tuacheni ujinga huu. Tufanye kazi. Kazi tu ndio kipimo cha ukamanda na sio kurambaramba visigino vya watu.

Mwisho, nasikia sikia sana habari za kuchinjana. Kuuana nk. Nasikia habari hizi kwa watu wale wale wa kikundi kile kile. Moja, natoka Kigoma. Nimeaga kwetu. Nitakufa kwa amri ya Mungu. Siogopi kufa. Iwapo kifo changu kitatokana na mkono wa mtu, sidhani kama kwa mtu huyo kama hata panya atabaki nyumbani kwao. Underline this.

Pili, revolutioneries don't talk about deaths. Only cowards do."
 
Wataingia vujana wengi tu mbona hata kwa Waganga walifichuana?
Du bora mambo yameenda mahakamani huko tutasikia mengi maana mpaka sasa tumefichwa kama ni kweli Lwakatare na Ludovick wapo pamoja au Ludo ni shahidi,
 
Ludovick na Lwakatare wote ni washtakiwa. Wanashtakiwa kuwa wameconive.
 
Ludovick na Lwakatare wote ni washtakiwa. Wanashtakiwa kuwa wameconive.

Yaani serikali yetu ingefanya hivi kwa wale waliotanjwa kuhusiana na utekwaji, na ukatili aliofanyiwa Dr Ulimboka nineonana haki inatendeka kote kote..... Mtu amewataja kabisa hata kuhojiwa tu hatujasikia matokeo yake wanamshikilia mkenya aw watu anayeomba Ulimboka aitwe kuthibitisha mbele ya mahakama bila mafanikio.....
 
Ludovick na Lwakatare wote ni washtakiwa. Wanashtakiwa kuwa wameconive.
ZeMarcopolo bado kule kwao kuna vijana waliosuka huu mpango sasa wamezungukana na bado hawajatajana ndio mana mpira unatupwa kwa TISS, CCM na POLISI kuwavunja nguvu lakini pumba sasa tutaziona
 
Last edited by a moderator:
Ni mwehu ndo anaweza kujiuliza maswali kwa hii issue
 
Yaani serikali yetu ingefanya hivi kwa wale waliotanjwa kuhusiana na utekwaji, na ukatili aliofanyiwa Dr Ulimboka nineonana haki inatendeka kote kote..... Mtu amewataja kabisa hata kuhojiwa tu hatujasikia matokeo yake wanamshikilia mkenya aw watu anayeomba Ulimboka aitwe kuthibitisha mbele ya mahakama bila mafanikio.....

Ni kweli kabisa. Under ideal conditions ilibidi angalau wahojiwe...
 
ZeMarcopolo bado kule kwao kuna vijana waliosuka huu mpango sasa wamezungukana na bado hawajatajana ndio mana mpira unatupwa kwa TISS, CCM na POLISI kuwavunja nguvu lakini pumba sasa tutaziona

Hii kesi inaweza kutengeneza chain ndefu sana.
Ndio maana Dr. Slaa alihemukwa alivyoona Lwakatare kakamatwa...
 
Kuna uzi upo humu wa Pro-Chadema waliuanzisha kwa ajili ya kujifariji na kujiliwaza wakisema DPP na Polisi wajichanganya.

Hawakujua kama kuna mambo yakuwekeana sumu ambayo yanafanywa na viongozi wao.

A Million Dollar Question....BAVICHA mpo¿
 
Ni mwehu ndo anaweza kujiuliza maswali kwa hii issue

Wavivu wa kujiuliza maswali siku zote huwaachia wengine wafikirie kwa niaba yao.
Wewe ni mmoja wao. Unamsubiri Dr. Slaa akutengenezee majibu...
 
Kuna uzi upo humu wa Pro-Chadema waliuanzisha kwa ajili ya kujifariji na kujiliwaza wakisema DPP na Polisi wajichanganya.

Hawakujua kama kuna mambo yakuwekeana sumu ambayo yanafanywa na viongozi wao.

A Million Dollar Question....BAVICHA mpo¿

Vijana wa bavicha wanafikiri propaganda inaweza kutatua maswala yote ya kisiasa.

Huu nyororo utaanza kuwataja mmoja baada ya mwingine. Hapa inabidi wajiulize je, polisi wamepata vidhibiti vingapi vya kufungulia kesi ya sumu?
 
Hii issue imeichafua sana chadema na itaendelea kufanya hivyo kwa kuwa mengi yataibuka

Dr. Slaa amefanya kosa kubwa sana kutoka hadharani kumtetea Lwakatare mbele ya vyombo vya habari.

Angejifunza kwa Maggid, ambaye amekuwa very quick kujiweka mbali na mtuhumiwa Ludovick.

Kitendo cha Slaa kujitoa kimasomaso kinamaanisha officially chadema na Lwakatare lao moja, atakalokutwa nalo ni la chadema...
 
Hivi huyo Ludo si gamba damu dam?

Ludo leo mahakamani alionyesha ishara ya vidole viwili juu kama jinsi alivyofanya Lwakatare.

Kimataifa ishara hii inamaanisha amani, lakini kwa Tanzania ishara hii hutumika kama utambulisho wa affiliation to chadema...
 
Ni mwehu ndo anaweza kujiuliza maswali kwa hii issue
kaka unapoteza tu muda wako,hii issue kwa sasa iko clear kabisa,na wananchi wana hasira sana huku mitaani,you can not cover up,ache sheria ichukue mkondo wake,ushauri kwa chadema,ingetoka huko mafichoni sasa na kuja hadharani kuwaomba radhi wale wote ambao ni wahanga wa oparesheni za lwakatare na chadema wakianzia na familia ya marehemu rasta chacha wangwe..
 
Dr. Slaa amefanya kosa kubwa sana kutoka hadharani kumtetea Lwakatare mbele ya vyombo vya habari.

Angejifunza kwa Maggid, ambaye amekuwa very quick kujiweka mbali na mtuhumiwa Ludovick.

Kitendo cha Slaa kujitoa kimasomaso kinamaanisha officially chadema na Lwakatare lao moja, atakalokutwa nalo ni la chadema...
Ukiiuwa sana damu za watu zinaku haunt unaanza kujitaja hadharan, masikini ya Mungu wakamchinja na mtu wao Arumeru ili tu kupata sympath.
 
Vijana wa bavicha wanafikiri propaganda inaweza kutatua maswala yote ya kisiasa.

Huu nyororo utaanza kuwataja mmoja baada ya mwingine. Hapa inabidi wajiulize je, polisi wamepata vidhibiti vingapi vya kufungulia kesi ya sumu?

Sasa hivi ni maswala ya kisheria zaidi siyo maneno matupu Bavicha wamenasa kwenye Trap hawawezi kutoka.

A Million Dollar Question...
 
Ukiiuwa sana damu za watu zinaku haunt unaanza kujitaja hadharan, masikini ya Mungu wakamchinja na mtu wao Arumeru ili tu kupata sympath.

Halafu kitendo cha Dr. Slaa kumtetea Lwakatare na kumkana Ludovick kuwa hamfahamu ni very risky. Iwapo Ludovick atapata vithibitisho vya kufahamiana na Dr. Slaa basi Dr. ataaibika mno.

Hii ishu ya sumu itazua mengi sana...
 
Back
Top Bottom