Kati ya watu wanaomfanya Rais achukiwe ni Makonda. Ni kiongoza aliyekosa busara. Ni kiongozi asiyeweza kufikiri kabla ya kutamka na kutenda.
Wajinga wapo wengi, waliokosa hekima wapo wengi na wapo kila nchi. Lakini ajabu kubwa ni pale unapoona aliyekosa hekima na mjinga, amepewa madaraka makubwa ya kuwaongoza wenye hekima, wenye ufahamu na wajinga wengine.
Rais amewadharau sana watu wa Dar. Kumfanya Makonda kuwa mkuu wa mkoa, tena mkoa wa Dar, ni tusi na dharau kubwa sana.
Umefika wakati nawaona PM na Vice Presidaa kuwa nao hawafai kabisa. Maana hata katiba inasema wao ndio wasaidizi wa Rais na washauri wakuu?iweje wanaona Makonda anaifedhehesha serikali Mara kwa Mara kwa utendaji wa hovyo hawamshauri? Au nao ni walewale wachumia tumbo?
Kumbe hata Magu kumteua mgombea mwenza mwanamke ilikuwa kwa vile ataweza kumdhibiti?
PM naye ndio huyu anayetishiwa hadharani shangazi zake kupewa kipigo ananywea?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.