A confused president and a constitutional crisis!

Angalia teuzi za jiwe kaka
Waislamu wanamwangalia tu!
Bila shaka atakaa miaka yake michache iliyobaki na kisha atakwenda zake
Lakini umma utabaki!!
 
Haya mambo ya siasa za kijinga ndiyo yametufikisha hapa! Hatuchagui viongozi wenye kujielewa wala kuelewa katiba ya nchi! Bunge lingekuwa na watu makini zaidi ya hizi rubber stamps za jiwe(na ccm kwa ujumla kuteua na kuchagua viongozi kwa umahiri wa kutukana wenye mawazo tofauti ya kisiasa), mngeona mambo! Ungekuta limeshamwajibisha jiwe kitambo sana kwa mujibu wa katiba yetu!

"Bunge laweza kumshtaki Rais Sheria ya 1992 Na.20 ib.8 Sheria ya 1995 Na.12 ib.4 46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii. (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais...

(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au

(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge."
 
Mkuu, hizi hapa chini ni sababu ambazo bunge lingeweza kumuwajibisha rais, lakini mfumo wetu ambao hata jiwe anaupendelea, ni kuweka vilaza humo wa ndiyo mzee na wa kupiga meza kwa hoja za kudidimiza taifa letu! Kati ya vipengele vyote hapo chini, yani aa, bee na chee, vyote jiwe yumo, lakini hakuna ufuataji wa katiba!

Rais anaweza kushitakiwa endapo...

"a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au

(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge."
 
Umeandika upuuzi mrefu lakini hakuna hata mahali ulipoonyesha jinsi katiba ilivyovunjwa.
Hupaoni kwasababu macho ya kuangalia umeyakalia na kichwa cha kufikiri umekikanyagia na unatumia visigino kufikiri! Isembo!
 
Sasa kwa bunge hili lilolojaa waoga wa kufuatiliwa na Nissan nyeupe unadhani itawezekana mkuu?
Pia hao waliojaa wagonga meza kuvimbisha matumbo yao tu nakupitisha sheria ambazo sasa hivi ni hasara kwa maendeleo ya Tanzania?
Bunge letu tukufu linahitaji kuongozwa na spika kama yule mwanamama wa Uganda mwenye uthubutu hata wa kumkosoa rais, hapo tutapata wabunge jamii ya kina Tundu Lissu na Zitto Kabwe
 
Asante kwa post nzuri.Tumekusikia mama
 
Miaka 5 ni mingi sana kwa Rais wa dizaini ya Jiwe. Kila hotuba yake moja lazima izue mijadala pingani isiyohesabika!
 
Jiwe anajua anachofanya. Ndo maana anadhoofisha upinzani kwa ufisadi wa kununua wanasiasa ili kupunguza au kuondoa kabisa wakosoaji wake.

Hata haki ya wananchi kuchagua wawakilishi ni kama haipo kwa sasa. Maigizo na wizi wa wazi kwny chaguzi umetamalaki
 
Inaonesha kuwa kumbe watu walio madarakani siyo lazima wawepo kwa ajili ya watu wanaowaongoza. Kila kitu hutegemea utashi zaidi kuliko taratibu zinazowekwa.
Na, hivi katiba yetu iliandikwa lini, na nani, na ilipataje mambo ya kuandikwa humo?
Wananchi "majority" yao sidhani hata wanajihusisha, yote yafanyikayo ni kwa utashi na hisani zaidi.
 
Hivi kwa nini huu ubaguzi unaendelea na sisi kama Taifa tumekaa kimya? Ilianza kupigwa marufuku mbunge wa jimbo moja kuongea na watanzania wa jimbo lingine. Sasa imekuja ya kupiga marufuku kupeleka maendeleo kwenye jimbo la chama tofauti na chama cha kiongozi wetu wote.
 
Kaya yetu kwa sasa haiongozwi kwa kanuni na sheria za kaya yenyewe bali kwa utashi wa aliyekalia kiti.
 
Awamu hii kuna mambo mabaya sana yameinuka.
ukanda/ukabila
upendeleo wa waziwazi wa kikanda na itikadi
demokrasia imebanwa mno
uhuru wa vyombo vya habari hakuna
Tusali, kufunga na kuomba sana kwani hata Mungu hawezi kuwa kati yetu tena.
 
Huwa najiuliza sana mkuu. Nadhani kuna tabia ambazo ni general kwetu sisi waafrika ambazo bila shaka ziliwavutia hata wageni kututawala.

Pia utamaduni wa kutizama individuals Zaidi bila kufahamu kwamba taifa letu linaongozwa kwa taratibu zake, mfano katiba ambapo hakuna aliye juu yake hata rais wa nchi.
 
Awamu hii kuna mambo mabaya sana yameinuka.
ukanda/ukabila
upendeleo wa waziwazi wa kikanda na itikadi
demokrasia imebanwa mno
uhuru wa vyombo vya habari hakuna
Tusali, kufunga na kuomba sana kwani hata Mungu hawezi kuwa kati yetu tena.
Yote hayo mkuu wangu ni kinyume kabisa na katiba hii tuliyonayo. Tatizo ni bunge.
 
Yote hayo mkuu wangu ni kinyume kabisa na katiba hii tuliyonayo. Tatizo ni bunge.

Bunge lenyewe halionyeshwi wazi kwa wananchi tena kama ilivyokuwa awamu ya4..tatizo ni Huyu "kichaa" tulonaye na watanzania wasipoamka na kudai haki zao kwa protests and strikes hakika tutatawaliwa na sio kuongozwa..hili limejidhihirisha wazi Trillion 1.5 inafanya kazi ya kununua wabunge madiwani na viongozi wengine wa serikali...ili apate nguvu ya kubadilisha katiba aendeleze utawala wake usio na misingi ya sheria.. sijui Huyu mtu. Tanzania is a country that is going down in history like never before, having this lunatic who has proven himself a maniac is a disgrace to mental health Tanzanians...He must go

Over
 
I see there is a serious problem somewhere. Nyakati za nyuma, wananchi walijali kidogo kuhusu katiba ya nchi. Enzi za chama kimoja, kulikuwepo na wale kina Njelu Kasaka. Walisimamia katiba and they were proud of it. Kuna namna viongozi wetu wanacheza na akili za watanzania. As if baada ya multiparty system, hakuna tena katiba ya kuongoza nchi. Hili ni tatizo kubwa, hakuna uzalendo. Na uzalendo unajengwa na katiba bora mtu asikudanganye.

Kwasasa nchi ni kama inaongozwa na waswaga ng'ombe na ng'ombe ndo wananchi! Sijawahi kusikia wananchi wakiwa proud kuhusiana na katiba yao ambayo imebeba haki zao zinazovunjwa kila kukicha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…