A call up for peace in Burundi

mwalimutz

New Member
Jun 12, 2015
3
2
Nimemuandikia barua Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa, barua hiyo imetokana na uhalisia wa hali ilivyo nchini Burundi na jinsi RAIA wa nchi hiyo wanavyoteseka. Kilichonisukuma kuandika barua hiyo yenye wito wa Amani ni

*Mimi kama kijana wa kiafrika najiona ni sehemu ya kila kinachoendelea katika bara langu

*Kijiji nilichozaliwa Kagunga ni sehemu pekee inayopokea wakimbizi kutoka Burundi kuliko sehemu nyingine yoyote.

*Watanzania wa Kagunga wanaathirika moja kwa moja na machafuko au vita nchini Burundi, hivyo sijahadithiwa nimeyaona mwenyewa kwa macho yangu na nimewahi kuwa sehemu ya wahanga.

Barua hiyo nimeinakilisha kwa viongozi wafuatao ambao kila mmoja nimempelekea nakala yake Mimi mwenyewe kwenye Ofisi yake/Embassy yake Dar_Es_Salaam Tanzania;

*Rais wa Zimbabwe Ndugu Robert Mugabe kama Mwenyekiti wa AU
*Rais wa Jakaya Kikwete kama Mwenyekiti wa EAC na Rais wa Tanzania
*Rais Uhuru Kenyatta_Kenya
*Rais Paul Kagame_Rwanda
*Rais Yoweri Museveni_Uganda
*Rais Pier Nkurunziza_Burundi
*Rais Barrack Obama_USA
*Rais François Hollande_Ufaransa

Lengu mahsusi la barua yangu ni kuomba na kuwashauri kuona ni namna gani viongozi Hawa wanaweza kuyanusuru maisha ya Akinamama, Watoto na Wazee ambao ndio victims wakuu pindi zinapotokea vita.Suala la Burundi likifikia pagumu wala hatuhitaji kutafuta mchawi wakati mamilioni ya akinamama, watoto na wazee wameshateswa na kuuaawa bila hatia.

Haitakuwa na maana ICC iwahukumu watu kumi wakati tumeshawapoteza Dada na kaka zetu 300,000 baada ya vita.Mwalimu.Khalid Shaban nipo Geita.
 
Back
Top Bottom