A Black Christian is a Traitor to the Memory of his Ancestors | Africa Wake Up

Call me GHOST

Member
Jan 18, 2019
53
95
BOOK SUMMARY: WHITE POISON

(A Black Christian is a Traitor to the Memory of his Ancestors..Africa Wake Up !)

MWANDISHI: Kayemb “Uriël” Nawej

MCHAMBUZI: Ghost Writer()

Tuanze kwa kumnukuu Rais wa kwanza wa KENYA Bw. Jomo Kenyatta kipindi cha uhai wake aliwahi kusema kwamba;-

"Wazungu walipokuja Barani Africa, walitukuta tuna Ardhi yenye rutuba, na wao walikuja na Biblia, Wakatufundisha kusali tukiwa tumefumba macho, na tulipofumbua macho baada ya kusali walikuwa tayari wanamiliki ardhi yetu na sisi tukapewa Biblia.."

Sasa twende mdogo mdogo tuone alikuwa anamaanisha nini

Tukirudi nyuma mpaka mwaka 1883 huko Ubelgiji Mfalme wa ubelgiji KING LEOPOLD II alitoa hotuba fupi kwenye semina ndogo iliyoandaliwa kwa lengo la kuwanoa Wamishionari kabla ya kuja Barani Africa na kati ya Mbinu waliyoitumia kuliteka Bara la Africa ilikuwa ni ASSIMILATION(Kuwafundisha Waafrica Lugha na utamaduni wa Kizungu)

Assimilation imegawanyika katika tanzu mbalimbali ikiwemo KI-DINI,-UCHUMI, -SIASA na -JAMII Hivyo wakaona ni vyema Kuanza na KIDINI( Religious Assimilation) kwa sababu ndio ingekuwa rahisi kuwarubuni waafrica na pia ingesaidia kuanzisha Mifumo hii mingine kiurahisi.

Baadhi ya mambo aliyowaeleza ni kama yafuatayo;

1. Aliwaambia wamishionari wasiwafundishe waafrica mambo ambayo tayari wanayajua kwa mfano imani kwa wakati huo tayari africa ilikuwa ina imani na walikuwa wanaabudu miungu ambayo sehemu kama Congo MUNGU alikuwa anajulikana kwa majina kadhaa wa kadhaa ikiwemo MUNDI, MUNGU(kama tunavyomuita ata sasa) na DIAKOMBA

Hivyo miongoni mwa majukumu waliyopewa hawa wamishionari ambao walikuja kama viongozi wa dini yaani PRIESTS ni kuhakikisha wanatimiza jukumu la kiutawala walilokabidhiwa toka Nchini kwao Ubelgiji.

2. Wamishionari walipewa jukumu la kuitafsiri injili kwa waafrica kwa minajiri ya kulinda na kufanikisha Malengo yao katika Bara la Africa.

3. Jukumu lingine lilikuwa kuhakikisha Waafrica wanapoteza hamasa juu ya Ardhi yao iliyojaa UTAJIRI mkubwa na yenye rutuba kwa maana bila kufanya hivo Waafrica wasingekubali kuona Wazungu wakichukua Mali zao hivyo wangepigana.

Kwahiyo kwa kuwapumbaza ilibidi wawadanganye waafrica kupitia vifungu kadhaa vya kwenye Biblia vitakavyowapa hofu

Ukisoma Mathayo 5: 3-12 utaona ni kwa namna gani wamishionari walihakikisha wanatumia elimu yao juu ya injili kuwawezesha kuwaambia waafrica kwamba ili kuurithi ufalme wa MUNGU lazima mtu uwe na Unyenyekevu n.k

Soma: (Mathayo 5:3)
"Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.."

Na wakaenda mbali zaidi kwamba ni ngumu sana kwa MATAJIRI kuurithi UFALME wa MUNGU hivyo waafrica wengi wakawa waoga kutumia Rasirimali zao kwa kuogopa kutajirika na kwenda motoni.

4. Wamishionari walikuwa na jukumu la kuhakikisha hawawapi nafasi Waafrica Kuhoji( CRITICAL THINKING) yale yote
wanayoambiwa kupitia mafundisho ya kidini wanayopewa. Hivyo walikuwa wanafundishwa KUAMINI na sio KUHOJI

Soma: (Yohana 20:29)
"Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.."
(AMINI ata kama HUJAONA)

5. Mfalme Leopord II aliwaambia wahakikishe wake zao( wanawake wa kiafrica) wanawaamini na kuwanyenyekea kwa kuwaletea zawadi mbalimbali kama Mbuzi, kuku au Mayai kama ishara ya shukrani( GESTURE OF GRATITUDE) kila wakati wanapotembelea vijijini kwao(..na jambo hili linaendelea hadi leo..loh). Kwa kifupi waliambiwa wahakikishw waafrica hawatajiriki kwa sababu wakiruhusu watajirike hawawezi kuwa WANYENYEKEVU

6. Waliambiwa wahakikishe Waafrica wanalipa KODI kila wiki siku za makusanyiko ya JUMAPILI(..yaani Siku ya kusali ile sadaka ndio kodi..Mmmh hatari!!)

Kisha tumieni Fedha hizo kujenga Hospitali, Mashule na Makanisa kwa ajili yao ili waone tunawapenda na kuwa jali sana waendelee kupumbazika..Sisi Hao..Balaa!!!

Kisha anzisheni mfumo wa Kutubia ( CONFESSION SYSTEM) utakaowawezesha kuchunguza na kujua kama mbinu zenu mlizozitumia zinafanya kazi kwa sababu watakuwa wakikosea wanakuja kutubu(..wakienda kinyume na mafundisho ya kwenye Kitabu cha Mathayo 5: 3-12)

Baada ya wamishionari kufika Africa sana sana Kongo, Aliyekuwa kiongozi wa Makoloni ya Ubelgiji Bw. Jules Renquin mnamo mwaka 1920 aliongezea nyama nyama kwenye kile kilichokwisha semwa na King Leopold II hapo awali na kusema mambo yafuatayo:

Waafrica waambiwe kuabudu sanamu ni kumuabudu shetani hivyo inabidi waache kufanya hivo kisha wamishionari waliambiwa wachukue masanamu hayo wayapeleke kwenye majumba yao ya makumbuko(Museum) lengo kubwa likiwa kuhakikisha waafrica wanawasahau mababu(Ancestors) na utamaduni wao.

Kuwachukulia waafrica wote kama watoto wao wa kufikia..hivyo kuwafundisha wawaite FATHER(Baba)..Mfumo huu nadhani unaendelea mpaka leo Wakatoliki wanamuita kiongozi wao wa kiroho FATHER na wakristo wengine wanamuita kiongozi wao wa kiroho BABA MCHUNGAJI

Wafundisheni Mafundisho lakini nyie msiyafuate hayo mafundisho kwa sababu ni ya uongo na endapo wakiwaliza kwanini nyie hamyatendi na kuyafuata yale yote mnayoyahubiri na kuyanena muwajibu " Mnapaswa kufuata kile ninachokisema na sio kile ninachokitenda"(kauli hii inatumika sana kwa wakatoliki na wakristo wengi mpaka sasa) kwani "Heri ya wale wanaosadiki bila kuona" kama isemavyo biblia.

Maneno ya King Leopold II na Bw. Jules Renquin yamekuwa yakifuatwa kila siku na ikawa ni utamaduni kwa wanawake wa kikongo wakati huo.

Ukisoma kitabu cha ABO UNE FEMME DU CONGO (A woman of Kongo) kilichoandikwa na Ludo Martens kilichochapishwa mwaka 1995 utaona ni kwa kiasi gani mwandishi amejaribu kuzungumzia suala hili kiundani kwa mfano katika ukurasa wa 68 amezungumzia mambo kadhaa yanayoendana na haya tuliyokwisha jadili hapo awali. Alienda mbali na kusema mambo yafuatayo..

Mababu zetu walikuwa wakijitegemea na walikuwa huru kwenye nchi yao lakini wakoloni walipokuja kwa lengo la kuwatawala kijiji baada ya kijiji, waliwaletea babu zetu chumvi na samaki waliokaushwa ili kuwarubuni washirikiane nao ila walikataa. Baada ya kukataa ilibidi watumie silaha za moto(Bunduki) na kwa Muafrica yeyote alieendelea kukataa kwa aliyekutwa na Upinde au Mshale mkononi alipigwa risasi papo hapo kisha wakawalazimisha babu zetu kuwafanyia kazi ngumu na wale walioonekana ni wavivu wakawa wanauawa.

Kisha wakatuletea Wamishionari (Tuwekane sawa kidogo hapa neno Missionary limetokana na Mission-ary ikiwa na maana walikuja na Mission yao) wakiwa na lengo(Mission) la kuwarubuni waafrica ili wawafanyie kazi kwa kujitolea kiroho safi (Ndio maana wakaja na ile mbinu ya Assimilation)

Waliwachukua watoto wadogo kutoka kwa mama zao na kuwafundisha dini kwa kisingizio eti ni Yatima hivyo watoto wamekuwa wakifundishwa dini na kukua wakijua ni Yatima hivyo kuwanyenyekea wao. Hivyo mdogo mdogo wakawa wakiisambaza dini yao baina yetu.. Hii inamanisha nini!?

Wao wamekuwa wakitukataza tusipende Pesa ila tumpende M/MUNGU aliye hai kuliko pesa lakini Wao Je! Hawapendi pesa!? Kampuni zao ikiwemo The Oil Mills of Belgium Congo inaingiza mamilioni ya pesa kupitia jasho letu. Je! Kutopenda pesa ni kuukubali Utumwa kwa kupewa ujira mdogo wakati wao wananufaika zaidi!!?

Walitukataza TUSIUE(Kutoka 20:13), Je! Wao hawaui!!?.. Hapa kilamba Mwaka 1931 waliuwa zaidi ya wanakijiji 1000.

Walitukataza TUSIIBE(Kutoka 20:15), Lakini wao wameiba ardhi yetu yenye rutuba, utajiri wetu na rasilimali zetu nyingi lakini Mtu mweusi alikuwa akiiba lazima aende KUTUBU na kumwambia kila kitu Mchungaji(Priest) kisha baada ya hapo mchungaji anapeleka taarifa kwenye Uongozi wao na yule mtu anakamatwa na kuwekwa Gerezani.

Sasa leo, Unaanzaje kuwa Mkatoliki au Mkristo!?

Unawezaje kuabudu dini ya watu wale waliokutesa!?

Unawezaje kuabudu dini ya watu walio-tesa,-dhurumu,-nyanyasa,-dharirisha,-ua babu zako!?

Wakatoliki na Wakristo wote ambao ni Waafrica wote ni WASALITI kwa mababu zao walioteswa, nyanyaswa,dhurumiwa,na kuuawa na wakoloni hawa.

Ni bora ata waafrica wenzangu waabudu zingine kuliko hii ya hawa waliotunyanyasa zaidi

Unaweza kuwa mkimbagu, mbuddha, muislamu na ata kuwa muumini wa dhehebu lingine lakini sio la hawa Wakristo kwa sababu kufanya hivo ni sawa na kuwatukana Babu zetu..

Hadi leo hii tunaona kuna viongozi wakubwa wa dini hizi ambao ni Waafrica wenzetu..hii inamaanisha nini!?

Waafrica bado tunatawaliwa na tutaendelea kuwa watumwa wa kifikra kutokana na huu Ukoloni mambo leo ulioletwa na watesi wetu.

Je! wakati makanisa ya Catholic, Protestant, Adventist, Baptist na mengineyo yaanzishwa na hawa wazungu kulikuwa ata na muafrica mmoja kati yao!!? Bila shaka jibu ni HAPANA!!

Angalia leo sasa, Sio Ghana, Kongo, Angola, Cameroon na sehemu zingine zote waafrica wanaabudu dini hizi kwa maelfu na maelfu yao huku wakitumia Biblia Takatifu kama kitabu cha marejeo lakini wamesahau hii hii Biblia ndio ilikuwa ikitumika kama kitabu cha marejeo na sheria zilizotumika kuwapumbaza Babu zetu na kusahau imani zao za asili walizowakuta nazo.

Itaendelea!!
(Ghost..)
 
Tuliomo kwenye huu uzi tuweni wapole jamani mana ni kama tunasafiri na mtumbwi MTO Kongo muda so mrefu tutakutana na maporomoko.
 
Unaweza kuwa mkimbagu, mbuddha, muislamu na ata kuwa muumini wa dhehebu lingine lakini sio la hawa Wakristo kwa sababu kufanya hivo ni sawa na kuwatukana Babu zetu..


Unataka kusema ubudha na uislamu ni asili ya muafrika mweusi? Huo ukimbagu siufahamu labda utuambie ndio kitu gani?
 
BOOK SUMMARY: WHITE POISON

(A Black Christian is a Traitor to the Memory of his Ancestors..Africa Wake Up !)

MWANDISHI: Kayemb “Uriël” Nawej

MCHAMBUZI: Ghost Writer()

inaendelea..

Kabla ya ujio wa wakoloni Watu weusi walikuwa wakiabudu miungu( Polytheism) lakini baada ya ujio wa hawa wazungu mambo yakaanza kubalika baada ya kuanzisha imani ya Mungu mmoja( Monotheism) kwa kusema Miungo tuliyokuwa tunaiabudu ni imani potofu kwani kuna Mungu mmoja tu ambaye yuko juu.

Kabla ya ujio wao, watu weusi walikuwa na zaidi ya lugha 7 ambazo walikuwa wakiongea na kuzitumia kuandika baadhi ya maandiko yao mbalimbali. Kulikuwa na Yoruba, Nsibidi, Gicandi, Mende, Vai, Loma, Ge'ez, Bete na Bamum

Yoruba ilikuwa ikiongewa baadhi ya sehemu ikiwepo Nigeria, Ghana, Benin, Togo na Ivory Coast

Nsibidi ilikuwa ikiongelewa sana Nigeria na Cameroon

Gicandi ilikuwa ikiongelewa Nchini Kenya tu hapo kwa jirani zetu ambayo sahv nadhani niyo wanaita Kikuyu

Mende ilikuwa ikitumika zaidi Sierra Leone na Liberia

Vai ilitumika sana Liberia na Sierra Leone pia

Loma ilitumika Liberia, Guinea na sehemu zingine

Ge' ez ilikuwa ikitumika Nchini Ethiopia

Bete nayo ilikuwa ikitumika Nchini Ivory Coast

Lakini pia Bamum ilikuwa na yenyewe inatumia Cameroon n.k

Na katika Maandiko hayo yote yaliyoandikwa na watu weusi kabla ya ujio wa wazungu yalikuwa yakigusa sehemu mbalimbali ikiwepo sayansi, sanaa, ushairi n.k lakini wengi wetu tumekuwa tukijua kwamba wazungu ndio walitufundisha kusoma na kuandika kwani walitukuta hatujui kusoma wala kuandika( Illiterate)

Kwa lugha ya Lingala, kusoma ni Kotanga na kuandika ni Kokoma

Kwa lugha ya Bambara, kusoma ni Kalan na kuandika wanaita Sebe

Kwa lugha ya Fulani, kusoma wanaita Janguigol na kuandika ni Windugol

Kwa lugha ya Yoruba, kusoma ni Kika na kuandika ni Kiko.

Tumeona kwamba bila ata ya ujio wa Waarabu na Wazungu tayari Africa ilikuwa na lugha zake , Swali la kujiuliza ni inawezekanaje Africa iwe na maneno yanayomaanisha KUSOMA na KUANDIKA ikiwa hawajui kusoma na kuandika!!?

Hivyo basi, Wazungu walikuja kutubadilishia mfumo wetu na kutufundisha mfumo wao ila sio kwamba walitukuta hatujui Kusoma na Kuandika.

Tukirudi nyuma kidogo tukamuangalia Mwanahistoria wa kigiriki ya kale 'Deodorus of sicily' katika nyakati za Julius Caesar ni kwamba maandiko ya kigiriki( Hellenic writing) ambayo ndiyo yalizaa maandiko ya Kirumi na Latin yalikuwa yakifundishwa na Mtu mweusi aliyekuwa anaitwa Cadmos kutoka Misri ya kale. (Tutalizungumzia hili kiundani katika maandiko yanayofuata na uthibitisho kadri inavyowezekana).

Je unajua kwamba viongozi waa kikristo sana sana Papa wamekuwa wakiunga mkono biashara za utumwa!?

Je umekuwa ukijua kuwa wamekuwa wakisema kwa muda mrefu kwamba watu weusi hawana nafsi!?

Je unajua kuwa babu zetu walibadili dini na kuwa wakristo kwa kulazimishwa, kunyanyaswa, kuteswa na mauaji ya halaiki!?

Hivi unafikiri Babu zetu wanajiskiaje huko walipo wakiwa wanatuangalia kwamba kunaipenda dini ya wale waliowatesa na kuwauwa!?

Kwa miaka mingi zaidi ya waafrica 15,000,000 wanaume, wanawake kwa watoto wamekuwa wakichukuliwa kama punda( Beast of burden) kwa kubebeshwa mizigo kama watumwa huku wakidanganya na maneno potofu kwamba "Mpende Jirani yako kama nafsi yako"(Mathayo 22:39) lakini wao walikuwa wanawapenda jirani zao ambao wamewafanya kuwa watumwa!?

Usilolijua wale wafalme watatu Melchior, Gasper na Balthasar waliokwenda kumuhani Yesu baada ya kuzaliwa mmoja wapo alikuwa ni Mtu mweusi. Melchior ambaye alikuwa mfalme wa Persia, Gasper alikuwa mfalme wa india na Balthasar alikuwa mfalme wa Arabia ama ukipenda Ethiopia.

Picha ya Bikira Maria( Cult of the virgin Mary) haikuwepo wakati wa ukristo mwanzoni ila baada ya mwaka 431 ndio walianza kuitumia kanisani

Mfumo wa Kuabudu sanamu za Mitume na Malaika ( Veneration) haukuepo mpaka mwaka 609 ndio walianza kuweka sanamu za mitume na malaika kwenye Makanisa yao. Lakini pia walianza kuziweka picha za mitume hao Makanisani kuanzia mwaka 787

Mfumo wa Utawa( Celibacy) ulipitishwa kwa Mapadri na viongozi wengine Mwaka 1074 ila huko nyuma haukuwepo na Mitume wote walioa isipokuwa Yohana na Paulo.

Mfumo wa kuvaa Taji la kristo ( Crown of christ) ulianzishwa mwaka 1090

Utoaji wa sakramenti( The sacrament of Penitence) ulianzishwa mwaka 1213

Matumizi ya Mkate( wafer) kama mwili wa kristo yalianza mwaka 1215

Matumizi ya Mvinyo( wine) kama damu ya kristo yalianza mwaka 1415

Na imani hii ya kutumia Mkate na Mvinyo( Transubstantiation) kama ishara ya mwili na damu ya kristo ulithibitishwa kutumika rasmi mwaka 1551 wakati wa mikutano ya Council of Trent ikiendelea

Na mengine mengi ikiwemo imani ya Immaculate conception iliyowekwa bayana mwaka 1854 na Amri ya Papal infallibility iliyotolewa kwenye First Vatican Council mwaka 1870

Unaweza kuona mambo yote haya yaliyoanzishwa baada ya kuondoka kwa Yesu kristo lakini hakuna ata kimoja alichokianzisha yeye kati ya hivo.

itaendelea!!
(Ghost..)
 
Haya maandishi yameandikwa kwa Shumom/Bamum
write-3.jpg
 
Haya ni baadhi ya maandiko yaliyoandikwa kwa lugha ya Ge'ez ilikuwa ikitumika huko Ethiopia na utamaduni wao umekuwa ukilindwa zaidi na Mfalme Menelik II kipindi hiko kiasi cha kuwafukuza wavamizi wa kiitalia na ndio sababu Ethiopia kuwa Nchi pekee Barani Africa ambayo haikutawaliwa na wakoloni
170px-Ethiopian_Scroll_comprising_prayers_against_various_ailments_Wellcome_L0031387.jpg
200px-Ethiopic_genesis_(ch._29%2C_v._11-16)%2C_15th_century_(The_S.S._Teacher's_Edition-The_Ho...jpg
 
Unaweza kuwa mkimbagu, mbuddha, muislamu na ata kuwa muumini wa dhehebu lingine lakini sio la hawa Wakristo kwa sababu kufanya hivo ni sawa na kuwatukana Babu zetu..


Unataka kusema ubudha na uislamu ni asili ya muafrika mweusi? Huo ukimbagu siufahamu labda utuambie ndio kitu gani?
Kimbaguism ni dini ya asili iliyoanzishwa na Simon Kimbagu huko Congo mwaka 1921

Tukija kwenye suala la Ubuddha sio kwamba ni lazima iwe imeanzishwa/ ni utamaduni wa Mtu mweusi ila mwandishi alichokuwa anamaanisha ni bora kufuata imani ya kibuddha ya kuabudu miungu kuliko kuamini katika ukristo( Monotheism)
 
Kimbaguism ni dini ya asili iliyoanzishwa na Simon Kimbagu huko Congo mwaka 1921

Tukija kwenye suala la Ubuddha sio kwamba ni lazima iwe imeanzishwa/ ni utamaduni wa Mtu mweusi ila mwandishi alichokuwa anamaanisha ni bora kufuata imani ya kibuddha ya kuabudu miungu kuliko kuamini katika ukristo( Monotheism)
Asante sana kwa elimu hii.
 
Kimbaguism ni dini ya asili iliyoanzishwa na Simon Kimbagu huko Congo mwaka 1921

Tukija kwenye suala la Ubuddha sio kwamba ni lazima iwe imeanzishwa/ ni utamaduni wa Mtu mweusi ila mwandishi alichokuwa anamaanisha ni bora kufuata imani ya kibuddha ya kuabudu miungu kuliko kuamini katika ukristo( Monotheism)

Uislamu je? Maana hapo umeelezea kimbanguism na Ubudha.
 
Back
Top Bottom