97.2% ya magonjwa yasiyoambukiza hutokana na ulaji mbovu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Tafiti za wataalamu wa masuala ya afya na lishe bora zinabainisha kuwa asilimia 97.2 za viashiria vya magonjwa hayo yanatokana na kutozingatia kanuni bora za lishe,huku Mkoa wa Dodoma ukitajwa kuongoza kwa 42.27%,ikifatiwa na mkoa wa Geita 39.94 na Arusha 38.6%.

Dkt Omari Ubuguyu ni Meneja Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya anabainisha kuwa Serikali imeendelea na mpango wake kwa vitendo Katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ambukiza ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wataalam zaidi ya 200 kwa lengo la kwenda katika kuhudumia jamii kwa kutoa elimu kuhusu magonjwa haya yasiyo ambukiza.

"Miongoni Mwa afua ambazo zimekuwa zikisaidia kwa Kasi kubwa Katika Mapambano haya ni pamoja na kufanya mazoezi miongoni mwetu,kwani mazoezi yamekuwa yakisaidia sana,hivyo Ukifanya mazoezi,ukizingatia kanuni za Lishe na kuachana na matumizi ya tumbaku na pombe uhakika wa kujilinda na magonjwa haya ni uhakika,Alisema Dkt Ubuguyu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela alisema Kauli mbiu ya wiki ya Magonjwa yasiyo ambukiza imebeba Ujumbe mzito kwa jamii na kuwataka kuendelea kutumia afua zinazo pendekezwa na wataalam wa afya.

"Badili Mtindi wa Maisha Boresha Afya yako" kauli mbiu hii iwe Chachu ya kukabiliana na magonjwa haya yasiyo ambukiza ili tuwe na Taifa lenye watu imara kiafya kwa ajili ya shughuli za uzalishaji,kwa uchumi wa Taifa hili,hivyo mazoezi ni miongoni mwa mambo ya msingi,tupunguze kula chumvi na sukari nyingi katika Lishe zetu"Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Wataalamu wa afya nao ni miongoni mwa wadau muhimu Katika Mapambano haya Dkt Rose Mende ni miongoni mwa madaktari bingwa wa Magonjwa ya Figo anabainisha kuwa mfumo hasi wa ulaji kwa walio wengi tangu ngazi ya familia ni miongoni mwa sababu zinazo pelekea kuongezeka kwa Idadi ya waathirika wa Magonjwa yasiyo ambukiza nchini.

Kando na hilo,kwa upande wake Afisa Lishe Prosper Mushi ambaye ni miongoni wawezeshaji kuhusu elimu hiyo anatumia jukwaa hilo kusisitiza matumizi ya Lishe bora na kujiepusha kula vyakula vyenye mafuta mengi suala ambalo huatarisha afya ya mlaji.

Juma la Magonjwa yasiyo ambukiza limezinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa utamaduni na michezo Paulina Gekul,Jiji Arusha ambapo kilele chake ikitarajiwa kuwa Novemba 13 huku viongozi mbalimbali wakitarajiwa kushiriki akiwemo Waziri wa afya Dkt Dorothy Gwajima, ikiwa ni sehemu ya kampeni maalumu ya kupiga vita magonjwa yasiyo ambukiza nchini.

Naibu Waziri wa Utamaduni sanaa na michezo Mhe Pauline Gekul (kulia )akikata utepe maalumu kuashiria uzinduzi wa muongozo wa namna ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ambukiza Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela.

Katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ambukiza,Jamii imetakiwa kuwa na tamaduni ya kushughulisha mwili kwa kufanya mazoezi ya mara kwa mara ikiwa Sambamba na kuzingatia kanuni za Lishe bora.

Michuzi Blog
 
watu kula ovyo ovyo ndio starehe pekee walio nayo duniani. poleni sana wahanga wa hili vya duniani vinawapita vingi, unakalia mapenzi na wali mwisho wa siku presha na kisukari wanakua maswaiba wako
 
watu kula ovyo ovyo ndio starehe pekee walio nayo duniani. poleni sana wahanga wa hili vya duniani vinawapita vingi, unakalia mapenzi na wali mwisho wa siku presha na kisukari wanakua maswaiba wako
Mkuu mtaa ninao ishi Ni sweken maisha yetu ni ya kawaida Sana wali Hadi msibani au harusini.
Binafsi NIMEKUWA Ni mtu wa mazoezi kwa takribani maisha yangu yote HAKUNA wiki ilipita bila kufanya mazoezi kwa km 5 kila siku japo hupumzika siku mbili za wiki lakini nikapata kisukari na karibu 85% visukari + presha hapa vimeshamiri ni ajabu Sana. Watafiti mkuje huku
 
Basi ni umerogwa.
Jini laweza muingia mtu na kutengeneza ugonjwa kama, kansa, kisukar na presha.

Mbali na hapo huwezi jitetea ety kwamba nina mwili wa mazoezi na huku na kisukari.

Ni kawaida kujitetea, utakutana na mtu mwili umejaa mafuta (obesity)
Alafu anajitetea ety kunenepa ni kuridhika tu mimi hata siri ovyo ovyo.
Weee kakwambia nani?
Kisansi kabisa, kuwa mnene sana hutokana na kula chakula kilichozidi matumizi ya mwili wako, kwahiyo kinachobaki inabidi kihifadhiwe mwilini kama mafuta.
 
Basi ni umerogwa.
Jini lawaza muingia mtu na kutengeneza ugonjwa kama, kansa, kisukar na presha.

Mbali na hapo huwezi jitetea ety kwamba nina mwili wa mazoezi na huku na kisukari.

Ni kawaida kujitetea, utakutana na mtu mwili umejaa mafuta (obesity)
Alafu anajitetea ety kunenepa ni kuridhika tu mimi hata siri ovyo ovyo.
Weee kakwambia nani?
Kisansi kabisa, kuwa mnene sana hutokana na kula chakula kilichozidi matumizi ya mwili wako, kwahiyo kinachobaki inabidi kihifadhiwe mwilini kama mafuta.
Mkuu Nina urefu wa cm 168 Nina uzito wa kg 66 huwa nahakikisha hauzidi kg 67.
Nilikua na utaratibu mzuri Sana wa kula .labda mkuu maana haiwezekani mtaa mmoja mdogo kuwe na kiwango kikubwa namna hiyo Cha Wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
 
Am spiritual man.
Talk to me.
Mimi najivunia sana kuwa daktari wa kimwili na kiroho.
Nahakika shida yako niya kiroho.
 
Mkuu Nina urefu wa cm 168 Nina uzito wa kg 66 huwa nahakikisha hauzidi kg 67.
Nilikua na utaratibu mzuri Sana wa kula .labda mkuu maana haiwezekani mtaa mmoja mdogo kuwe na kiwango kikubwa namna hiyo Cha Wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Yaweza kuwa sukari yako ni ya kurithi! Angalia kwenye ukoo wenu.

Pia yaweza kuwa kwenye diet kuna sehemu moja ulikuwa unakosea, mfano ukute kila siku ulikuwa unajipigia Pepsi yako moja bariiiidi!
 
Back
Top Bottom