kalenda inaonyesha ilikuwa ni siku ya jumamosi.kwa wale wa enzi hizo mnaweza kutueleza mlikuwa wapi siku hiyo?naomba uzoefu wenu.
Mshua wangu alikuwa na miaka nane,maza kabisaaa bado hajazaliwa
Kama nlikuona vile ukifurahi kupewa pesa yenye tundu katikati ilikuwa inaitwa hela tano, nyingine hela saba n.k.na zilikuwa zimepamba kwa picha ya meno ya tembo hivi. Siku zile neno Uhuru lilikuwa linawashinda kutamka baadhi ya majirani zako na kutamka buluu badala ya uhuru.Nilikuwepo, kitu nnachokumbuka ni mafashfash na nnakumbuka bendera zilizopambwa barabarani hususan nje ya nyumba yetu, kumbuka nyumbani kwetu ni jirani kabisa na ilipozaliwa TANU na nnakumbuka ngoma iliyopigwa nje ya nyumba yetu usiku kucha nadhani lilikuwa ni gombe sugu, nilikuwa ni mdogo sana kiasi cha kuwa na "vague" memories. Nakumbuka bibi yangu alitupa wote (wajukuu) senti tano tano kama sadaka kwa furaha yake (senti tano siku hizo ilikuwa na tundu kati).
Nikikumbuka mengine ntarudi.