84% ya wahitimu kidato cha nne wamepata F kwenye hesabu

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Kwa takwimu zilizotolewa jana kuhusu matokeo ya kidato cha nne, somo la hesabu ndio limekua limewatesa wahitimu wengi.

Ufaulu wa somo waliopata hili ni asilimia 16, ikimaanisha ambao hawajafaulu, yaani waliopata daraja F ni aslimia 84.

Huu ufaulu wa hesabu umekua hivi miaka yote.

Je hili somo la hesabu mtaala wake ubadilishwe au tufanyeje ili kuwe na afadhali?
 
Mwalimu mwenyewe aayefundisha hesabu alipata d ya hesbu halafu unategemea mwanafunzi amzidi mwalimu?
 
Hesabu sio ngumu ila tatizo ni serikali inaajiri walimu wenye ufaulu hafifu kwenye hilo somo.
Serikali ibuni namna nzuri ya kupata walimu weledi katika somo hilo kuanzia ngazi ya chekechea.
Siku zote mtoto anapoanza shule, somo la kwanza kabisa kulimaster ni hisabati hata kabla hajajua kusoma. Ila kadri anavyozidi kujifunza jitihada ya mtoto ktk somo hili huvulugwa na mwalimu wake ikiwa mwalimu mwenyewe somo hili halikuwa chaguo lake.

Serikali itoe motisha nzuri na mishahara minono kwa walimu/wahitimu wa hesabu.
Iajiri walimu wenye ufaulu mzuri kuanzia ngazi ya chekechea mpaka kidato cha sita.
Itoe ahadi nzuri kwa wahitimu waliotayari kujitolea kuwa walimu i.e kuwapa mishahara minono na kuwahakikishia elimu ya bure kadri mwalimu atakavyoamua kujiendeleza katika somo hilo.
Makazi ya uhakika, motisha nono kadri atakavyo faulisha watoto, mikopo yenye riba nafuu na vitendea kazi vya uhakika ndivyo vitaleta mapinduzi ktk somo hili.
 
Hapo umenena. Ukipata mwalimu mzuri mbona hesabu rahisi tu
 
Mwalimu mwenyewe aayefundisha hesabu alipata d ya hesbu halafu unategemea mwanafunzi amzidi mwalimu?
sidhani, anayesomea degree ya ualimu unakuta alisoma pcm, pgm,au egm advance, na kusoma combinations hizo unatakiwa uwe umepata angalau c ya hesabu o level
 
waliopata F wengi wametokea shule za kata....Elimu gharama..'If u think that education is expensive..try ignorance'
 
hata kabla ya shule za kata hazijaanza, hesabu ilikua tatizo
lilikuwa tatizo kwa wanafunzi kutolipenda lakin walifundishwa vizur sasa hiv imekuwa tatizo kwa wanafunzi kutofundishwa vizur
 
Sasa mwalimu wa hesabu na kiswahli wanalipwa mshahara sawa,unadhan huyo wa hesabu atakua anafundisha au analipua tu?
 
kama serikali itaifanyia marekebisho mtaala wake wa elimu na kutoa motisha kwa masomo ya sayansi ikiwemo hesabu, mm nitarudi kufundisha hesabu sekondari otherwise never!
 
Tatizo la kufeli kwa hesabu inawezekana lisiwe la serikal wala walimu, ni tatizo la cc wanafunz wenyewe, ebu chukulia mfano wakati unakua mamaako anakwambia babako hatujali,hatusikilizi wala haeleweki, kwa sababu we ni mtt unaweza ukayachukua hayo maneno kama yalivyo na ukamchukia baba yako bila kufanya uchunguzi wwte, baadae unakuja kugumdua kwamba babakao alikuwa hana matatizo yyte ila ni mama ndo alikuwa tatizo.

Ni sawa na hesabu, watu wanajengewa uwoga kabla hawajafika kidato cha kwanza, mwanafunzi anaweza akawa anajua hesabu shule ya msingi ila sekondari anaambiwa
"Weee sekondari si mchezo hesabu swali moja karatasi mbili yani usipime ni ngumu balaa" wakati sio kweli cha muhimu ni jukumu la mzazi,mlezi pamoja na walimu kuwa pamoja kushirikiana katika swala hili!!

Na nirahisi sana kulimaliza sisi tumesoma shule za kata zina walimu watano hakuna mwalimu wa hesabu, Chemistry wala Physics ila unaingia mtaani unatafuta material unasoma maisha yanakwenda na watu walifanya vizuri kwenye hayo masomo kwa hiyo mi naamini kila kitu ni kuamua na kumuomba mungu! Ila mchango wa jamii na wazazi ni muhimu sana ili kuweza kulifanikisha hili.

Ahsante
 
Tatizo la kwa hesabu inawezekana lisiwe la serikal wala walimu, ni tatizo la cc wanafunz wenyewe, ebu chukulia mfano wakati unakua mamaako anakwambia babako hatujali,hatusikilizi wala hana haeleweki kwa sababu mi mtt unaweza ukayachukua hayo maneno kama yalivyo na ukamchukia baba yako bila kufanya uchunguzi wwte baadae unakuja kugumdua kwamba babakao alikuwa hana matatizo yyte ila ni mama ndolie alikuwa tatizo.

Ni sawa na hesabu watu wanajengewa uwoga kabla hawajafika kidato cha kwanza mwanafunzi anaweza akawa anajua hesabu shule ya msingi ila sekondari anaambiwa
"Weee sekondari si mchezo hesabu swali moja karatasi mbili yani usipime ni ngumu balaa" wakati sio kweli cha muhimu ni jukumu la mzazi,mlezi pamoja na walimu kuwa pamoja kushirikiana katika swala hili!!

Na nirahisi sana kulimaliza sisi tumesoma shule za kata zina walomi watano hakuna mwalimu wa hesabu, Chemistry wala Physics ila unaingia mtaani unatafuta material unasoma maisha yanakwenda na watu waliganya vizuri kwenye hayo masomo kwa hiyo mi naamini kila kitu ni kuamua na kumuomba mungu! Ila mchango wa jamii na wazazi ni muhimu sana ili kuweza kulifanikisha hili.

Ahsante
mkuu hapa umenena, wanafunzi nao wanahusika katika hili,
mimi huwa nasema ukiona system ni mbaya, usipotafuta njia ya ku beat ile system na wewe ni mzembe
 
Kweli kabisa yani mtu anaogopa kitu kabla hajakiona na jamii pia inamlaghai kwa maneno yanayokatisha tamaa, kiukweli mwanafunzi wa aina kufaulu itakuwa ngumu sana hata angekuwa anajielewa vp.
 
.....SASA HIVI WATAANZA KUPIGA KELELE WANAONEWA....LET WAITS.....KUMBE VICHWANI ...HAKUNA ....KITU.
 
Back
Top Bottom