Hapana miwani hiyo ya kuangalizia katika 3D TV set si cheap ndugu yangu. Miwani ya wakubwa ni $299 na watoto ni $249 (sasa fikiria nyumba ya mume, mke na watoto wanne na mishahara ya kwetu) hii ni samsung ambayo ndiyo wametoa set zao za 3D TV mwezi uliopita. Sony niliwauliza wanadaia wao set zao za 3D zitaanza kupatikana June, lakini awali vitu hivi huwa na bei mbaya na baada ya muda vinaanza kushuka taratibu.
Jana nilikuwa naangalia mechi kati MAN UTD na MAN CITY kwenye 3D TV CHANNEL, kwa kweli nilichokiona hakikunishawishi kununua 3D TV once zikianza kuuzwa madukani.
Sikuona tofauti kubwa sana na normal channel (zilikuwa zinaonyeshwa sambamba) zaidi ya clarity ambayo unaweza kuipata ukitumia HD CHANNEL.
Je wenzangu ambao mmeona 3D TV mmeionaje?
[/COLOR]
Mkuu hata kama una 3D capable receiver kama Broacasters hawana 3D transmission system itakuwa ni kazi Bure. Mfano kwa bongo hata uwenayo 3D capable receivers utaona 2D kwa sababu TBC , ITV are not broadcasting 3D contents na ndio maana now 3D ni vitu ambavyo vinaoneshwa kwenye cinema halls
[/COLOR]
Mkuu hata kama una 3D capable receiver kama Broacasters hawana 3D transmission system itakuwa ni kazi Bure. Mfano kwa bongo hata uwenayo 3D capable receivers utaona 2D kwa sababu TBC , ITV are not broadcasting 3D contents na ndio maana now 3D ni vitu ambavyo vinaoneshwa kwenye cinema halls
Miwani zake ni very cheap.... hata wewe unaweza kutengeneza mwenyewe....kwa hiyo ukinunua hiyo 3D inabidi uvae na miwani yake ndio utaona tofauti....hahaaa. sasa uto tumiwani tunaweza kuwa tungapi kwenye seti moja ya 3D maana familia zetu hizi za watoto watatu plus baba na mama , bila kusahau ndugu mmoja wa upande wa mume na mmoja wa upande wa mke , plus dada wa kazi , bado jirani hajakuja kuangalia DSTV ili amuone ROONEY ama Scholes akifunga goli la kichwa....kweli nahisi kama tumiwani hatutatosha maana .
kaka heshima mbele,nimeenda zaidi ya mara 3 kuangalia 3D cinema na mara zote narudi na 3D glasses kwa kiingilio cha £8 sasa jamaa si wangepata hasara kugawa hii miwani bure
usichanganye 3D GLASSES na 3D GLASSES ZA RAYBAN AU OAKLY hizo kweli zitakuwa $200-300
Mkuu nakushauri nunua kwa sababu nilipata bahati ya kuangalia demonstration ya Jamaa wa Smasung kama mwezi mmoja uliopita na tulikuwa kama watu watano hivi na miwani ilikuwa moja kwa kweli nilitamani nisiivue ile miwani kutokana na utofauti uliokuwepo
Miwani zinatofautiana Quality kwa hiyo hata efficiency yake lazima itakuwa Tofauti
Mbebabox,
Jamaa kidogo wamekuchanganya. Ulichoandika ni kweli kabisa na si uongo. Ukweli ni kama ntakavyoandika hapa chini.
Tangu watengeneze film ya AVATAR ambayo ilikuwa ni film ya kwanza kutengeneza moja kwa moja ikiwa kwenye 3D na nyingine kwenye 2D (kumbuka kuna kamera tayari za 3D). Sasa kinachotokea hapo, ni tofauti na ilivyokuwa zamani.
Niliposikia kuwa kuna TV 3D, nilifuatilia na kufahamu habari chache. Ukweli ni kwamba hadi leo hii, wako kwenye utafiti kwani picha za 3D kwenye TV hazijawa kwenye kiwango cha kufurahisha. Na wanakiri kuwa hii itawachukua muda. Lengo hasa ni kwamba mmtu uwe na uwezo wa kuangalia TV bila ya kutumia miwani. Kuna jamaa yangu Europe nilimuuliza baada ya kuangalia film ya Clash of Titans (2010) ameniambia jambo ambalo kidogo limenishangaza. Anasema kuwa "wakati akiangalia, (hakuwa Imax) walipewa miwani ya 3D, wakati akiangalia, hakufurahishwa sana na quality ya picha na akaamua kuondoa miwani ili aisafishe. Alishangaa kuwa aliweza kuangalia hiyo film bila miwani. Aliamua kuangalia hiyo film hadi mwisho bila kutumia miwani na picha iliendelea kuonekana nzuri tu ingawa si ile quality aliyoizoea. Image zilikuwa ndiyo zinasogea ila hazisogei sana kwa waangaliaji kama inavyotakiwa kuwa...."
Kwa maana nyingine nilivyomuelewa ni kwamba, ukiangalia film za 3D bila miwani, unaona kama image zimelaliana na zinaumia macho. Hii unaangalia bila ya miwani na unaona effect na macho hayaumi. Na hii kama nilivyosoma mwanzo, lengo la 3D TV na Film ni kuwa huko mbele watu wawe wanaangalia bila ya kutumia miwani. Tayari wameanza kutengeneza na utafiti unaendela na kama sikosei waliandika itachukua muda sana kufikia leongo ambalo waangaaliaji watafurahia product zao.
Kwa hiyo mkuu, kama uliangalia bila miwani, ni sawa tu. Kama mtu unahela ya kuchezea, unaweza kwenda kununua hizi TV set zikianza kuuzwa ila kama hela yako ya kutafuta kwa mbinde, basi vuta subira kwenye miaka kama mitano ijayo, wanaweza kuwa wameboresha sana quality yake. Soma maelezo ya 3D TV hata kwenye wikipedia wameandika kidogo kuhusu weak quality ya hizi TV kwa sasa.
umenisoma vizuri,alichokiona huyo rafiki yako ndio mimi nimekiona kabisa,nakumbuka kuna watu niliokuwa naangalia nao hawakuvaa miwani,na mama mmoja akaniuliza ''does it make big difference?(yeye alikuwa hakuvaa miwani) nikamwambia nope akasema ''thats why i dont bother put on those silly glasses''
Mkuu nakushauri nunua kwa sababu nilipata bahati ya kuangalia demonstration ya Jamaa wa Smasung kama mwezi mmoja uliopita na tulikuwa kama watu watano hivi na miwani ilikuwa moja kwa kweli nilitamani nisiivue ile miwani kutokana na utofauti uliokuwepo
Mkuu Ndege, mimi nitasubiri hizo za Phillips ambazo hazihitaji miwani.