3D Modelers,Animators and Graphics Designers Piteni Hapa Kidogo

3D Modelers,Animators and Graphics Designers Piteni Hapa Kidogo

mkuu
msaada wangu kwako ni huu.naomba uuzingatie sababu hauna gharama ya school fees,ni wewe tu na bidii yako .


kwanza kabisa uwe na computer yenye uwezo mkubwa wa ku-render 3D computer graphics na computer hiyo uwe na access nayo mda wowote utakapo jisikia kubuni kitu au kufanya mazoezi.yaweza kuwa laptop au desktop.


pili u-install 3D modeling softoware ambayo kwako umeona utaielewa kwa haraka.(usijilazimishe kujifunzia software flani sababu tu flani anaitumia au anakutambia nayo).


baada ya hapo,nunua modem ya mtandao wenye speed nzuri ya kuweza ku-play youtube videos.jiunge kwenye kifurushi cha bundle,ingia youtube for special mission(sio kutazama video za bongofleva).tafuta tutorials za software uliyo install ili uanze kujifunzia as a beginner.


fanya hivyo kwa mda wa miezi miwili au mitatu,huku ukiwa unaingia JF kuuliza maswali pale unapokwama (JF kuna magwiji wa kila taaluma).


nakuhakikishaia ukifatisha formula hii niliyo kuwekea hapa,utakuwa mtu mwingine baada ya miezi kadhaa.kinyume na hapo itabidi utenge fedha ya kutosha, uende nje ya nchi ukasomee mambo haya since bongo vyuo vya 3D ni magumashi.
asante.

Nashkuru mkuu na hii soffware naweza pata vp kama una link ambayo itakuwa rahc kuipata niwekee mkuu, ahsante
 
Wadau wa huu uzi mpo? kimya sana, sasa naombeni msaada wa jinsi ya kupata free plug-ins za adobe after effects cs 5 MacOs, nimejaribu google sipati, labda sijui jinsi ya kutafuta.

C.c adobe Aftre Effects, na wengine ambao sikuwataja please...
 
Last edited by a moderator:
Wadau wa huu uzi mpo? kimya sana, sasa naombeni msaada wa jinsi ya kupata free plug-ins za adobe after effects cs 5 MacOs, nimejaribu google sipati, labda sijui jinsi ya kutafuta.

C.c adobe Aftre Effects, na wengine ambao sikuwataja please...

pole sana mkuu,
swala la upatikanaji wa plugins ni swala pasua kichwa kwa kila mwana-field hii.uzoefu wangu unaniambia ni rahisi kupata full package ya software lakini si rahisi kupata plugins.kwanini?,kwa sababu karibia zote zinauzwa(hazipatikani bure) na hazina trial version.hata zile zinazopatikana kiujanja ujanja kwa kuzipakua mtandaoni,nazo unakuta hazija kamilika au zina mapungufu.

siku za nyuma nilikuwa na full package ya optical flares plugin,a very powerful plug-in for creating reflection and scattering light.bahati mbaya sana external HD ambayo niliifadhi,ili kufa ghafla.nilihuzunika sana.tangu wakati huo,sijabahatika kuipata tena.hata wadau wenzangu hawana.

msaada pekee ninaoweza kukusaidia ni kukuwekea baadhi ya majina ya plugins ambazo ni muhimu na ni bora sana kwa AE.wenyewe wanasema "after effects plugins every motion designer should have,(utazitafuta wewe mwenyewe kwa mbinu unazo zijua,ukizipata usisite kunigaia japo kamoja mkuu:madgrin🙂.

1:cosmo
2:Trapcode Particular
3😛rimatte Keyer
4:Optical Flares
5😀enoiser
6:Magic Bullet Looks
7:Element 3D
8:Mojo
9:Sapphire Distort
10:Trapcode Shine
11:Trapcode Particular
12:Element 3D
13😛lexus
14:Newton
15:Continuum Complete
16:twitch nk

kwa msaada zaidi ingia HAPA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom