kadoda11,
Nilipotea kwa sababu nimebanwa na mambo ya hapa na pale.
MAONI YANGU:
ARTISTICALLY
Ni jaribio zuri kwa anayeanza kujifunza Adobe AfterEffects (AE). Tumia 3D capability ya AE kutengeneza backgrounds za motion graphics na artificial environments. So, ulichofanya kinaridhisha kwa anayeanza kujifunza. Unahitaji kufanya bidii sana. Bidii sana. SANA.
TECHNICALLY
AE ni software ya kiwango cha juu kwa kazi za Motion Graphics na hata Visual Effects. Hata hivyo si nzuri sana kwa 3D animations. Ni kweli ina 3D capability kwa maana ya ku-position na ku-animate assets katika
3d space lakini kwa aina ya kazi uliyoonesha hapa AE haifanyi vizuri sana. Kuna plugin yake ya Zaxwerks Invigorator na pia Zaxwerks ProAnimator hizi zinaiongezea zaidi 3D capability. Sijui kama zinaendelea kuwa developed. Pia AE CS6 imekuwa enhanced na 3D capability kwa maana ya rendering ambayo quality (Ray tracing) yake inafikia ya dedicated 3D software kama Maya etc but modeling is so limited.
Cheki hapa.
VideoCopilot wametengeneza plugin iitwayo Element ambayo inaiongezea uwezo zaidi kuimport 3D assets from 3D Software katika format obj. Cinema 4D inaweza kuwa imported natively.
Hivyo nachosema ni kuwa 3D space ya AE (Actually ni 2.5D) ina matumizi yake but si kwa kile ulichofanya hapo juu, unless unajifunza tu ili upate idea namna inavyo-handle 3D, ila ukitaka kufanya advanced 3D ni lazima utumie software iliyo-dedicated ku-achieve professional quality.
MAONI YANGU JUU YA KIWANGO CHAKO.
Unajitahidi. Ongeza nguvu mara 9 ya ufanyavyo sasa.
ZAIDI
Ni lazima usome sana vitabu vya designing pamoja na kutazama tutorials za wengine. Nasisitiza rudi
VideoCopilot na fuata maelekezo ya Andrew Kramer. Ukipambana mwenyewe basi hakikisha kuwa unajua WORLD CLASS ya graphics ni ipi na u-Struggle kufikia kiwango hicho. HATA HIVYO HAYA NI MAONI YANGU TU SI LAZIMA UYAFUATE, KAMA UNADHANI UNARIDHIKA NA KILE UFANYACHO BASI FUATA HISIA ZAKO. Kila la Heri.
JARIBIO LANGU LA HIVI KARIBUNI
SOFTWARES:
Maxon Cinema 4D: Modelling, Animation & Multipass rendering.
Eyeon Fusion: Compositing.
MAELEZO KIDOGO
Kwa sasa siwezi kuwanya modelling ya binadamu na wanyama (Character modelling) ndiyo maana mkokoteni unaenda peke yake otherwise ningeweka mtu anauvuta. Nimetengeneza kwa mawazo kuwa mkokoteni unavutwa na si kusukumwa (Kuna watu wanaweza kushangaa kuwa unaenda nyuma badala ya mbele).