25% ya m-pesa

25% ya m-pesa

ARV

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2011
Posts
5,560
Reaction score
8,002
Msaada kwa anaejua hii 25% vodacom wanayotutangazia kila siku eti tukinunua muda wa maongezi kwa mpesa inaongezwa,hivi hii inaongezwa wapi?, kwa mfano mimi sasa hivi nilikuwa na salio la tshs 56/= nikanunua salio la shs 2,000/= kutoka mpesa, wakaniletea msg yao inaniambia nimenunua muda wa maongezi wa tshs 2000/= na nyongeza ya 25%,lakini nikiangalia salio ni tshs 2056;kuna mtu kaniambia nicheki kwenye *102*01# nakuta nako kuna tshs 0.00.Ina maana hii 25% wanatufunga kamba? na kama haipo kwa nini wanaleta msg 'umeongezwa 25%?'
 
Voda hapo ndo wanapo2ibia jamani,voda machz hawa akili **** nina zao hao.
 
Hiyo ni lugha ya biashara tu
kuna cku mm nilinunua Tsh.400/=
nikitegemea ntaongezwa 25/% ili iwe 500/= then nijirushe internet,
nilipopata msg kuwa imethibitishwa nimenunua, nikajaribu kujirusha eti naambiwa huna salio la kutosha!
Huu co mtandao tuhameni jmn!
 
Lakini mimi nimeshawahi kununua mara nyingi na wakaniongezea,tatizo ni kwamba hiyo nyongeza yako haiingii kwenye kiasi ulichonunua,ila ukipga *102*01# wanakuonyesha salio lako.Alafu pia pengine mtu aliponunua alipga simu na ile nyongeza ikatumika kwanza kabla ya salio la kawaida kuanza kutumika. Ila sijui,pengine wanatuibia kweli.
 
Hiyo ni moja ya promotion mwizi, binafsi sijawahi kuona kama kuna salio linaloongezeka. TCRA wana kazi kubwa bado
 
Wana JF: Ni vyema TUJIFUNZE Kuseme jambo baada ya kufanya research kwanza. Kimsingi hiyo 25% NI KWELI wanakupatia ukiongeza salio. Ili kuthibisha: Kwanza; Angalia salio la nyongeza kwa kupiga *102*01#, Pili; Ongeza salio kwa Mpesa hata kama ni tsh 200, Tatu; Baada ya kupata confirmation msg ya kupokea salio toka mpesa, Piga tena *102*01#. Utaona ongezeko la 25% tofauti na awali.
 
Back
Top Bottom