Waliozoea nyimbo za wanaoimba "hakunaga,nataka kulewa,mpenzi jini,mawazo,follow me,nimpende nani, n.k" watauchukia wimbo huo kwani wao wanapenda nyimbo zinazohamasisha ngono tu. Kimsingi Roma amejitahidi kugusa yale yanayoisibu jamii moja kwa moja.Ni kweli wasanii wengine kama Solo Thang na wimbo 'miss Tanzania' ameonesha maudhui ila kwa mafumbo kiasi kwamba vichwa ngumu vinaweza kuambulia ujumbe kidogo sana.Maana ya sanaa ya Hip hop siyo tu kutengeneza maneno kiufundi ila kujua namna hadhira watakavyoupokea ujumbe na kuelewa...Kuna mstari anasema "RPC usitume polisi,ili kuwazima CHADEMA,itakulilia damu ya Mwangosi,Iringa semeni amina" Huu ni ujumbe ulionyooka bila kificho.Anaongezea..."uchafu wa Mrisho,usiwe usafi wa Benja..." Je,si kweli kwamba kuna madhaifu fulani ya Mrisho then,watu wanasema afadhali Benja aliendesha vizuri uchumi na mahusiano ya kidini,huyo Benja aliiba vingapi na kusainishwa mikataba inayoligharimu taifa hadi leo, mfano Kiwira coal mining,EPA na kashfa ya BOT?