Kwa hiyo dribbles ndio ubora?
Mchezaji anaweza kupiga chenga hata watu watatu hadi wanne akamchukua na kipa, halafu mwisho akapiga shuti ovyo au akapaisha kabisa.
Hapo dribbles inakuwa na maana gani?
Assist inahesabika kuwa ni assist pale mtu aliyepasiwa akafunga.
Maana ya assist, maana yake ubora wako unahukumiwa na uwezo wa mfungaji.
Yani unaweza ukatoa pasi bora zaidi katika eneo zuri na la wazi, lakini mshambuliaji akapaisha na assist yako ikapotea.
View attachment 3641263
Mpira umebebwa na tukio moja kubwa ambalo ni goli kufungwa.
Goli ndio tukio linaloenda kuamua mshindi na loser.
Goli ndio imekuwa kipimo cha kwanza hata katika kutafuta Makocha.
Goli ndio linaloweza kubadilisha flow ya timu, mchezaji anaweza kucheza vibaya dakika zote 90 halafu dakika ya mwisho ya nyongeza akafunga bao la ushindi, akawa amefuta makosa yake yote na kuibuka shujaa.
Wakati huo yule beki wa upande wa pili aliyefanya vizuri kuzuia kwa dakika 90 lakini kosa la sekunde moja lililozaa goli, mechi nzima ya kiwango chake inaharibika.
Kwa ufupi kila kitu kinachofanyika uwanjani sijui chenga, pasi, kukaba, na mbio. Lengo lake kuu la mwisho ni kuzuia goli lisiingie upande wako au kulipeleka upande wa mpinzani. Goli ndio hitimisho la soka.
Sasa kwa factor hizi nani bora?