Ndugu zangu mashabiki wa Messi, swali moja kwenu ambalo mnapaswa kujiuliza ni, Messi angekuwa wapi bila Negreria na Infantino?
Nakubali kuwa ni mchezaji bora, mwenye kipaji ambacho hakijawahi onekana kabla. Maono yake, uwezo wake wa kupiga pasi na dribbling skills are all insane.
Lakini wachezaji wote wazuri wanahitaji mataji kudhihirisha thamani zao, bila upendeleo wa kimfumo, bila upendeleo kutoa kwa marefa ambao ni wa miaka na miaka, angeweza kushinda hayo mataji yote ambayo saizi ako nayo?
Dont believe me at all, ask yourself this question. Some of you are well educated, google the facts over the last 20 years.
Na saizi mambo yamerahisisha kuna hadi AI, angalia ushindi wa Barcelona kwenye Champions League I'm telling you, you might find some rigged ones.
Angalia yote yaliyotokea kwenye kipindi cha Negreria case. Ngoja niwakumbushe kidogo.
Negreira alikuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Waamuzi ya Hispania (CTA). Kamati hii ndiyo yenye mamlaka ya kuchagua refa gani achezeshe mechi gani (ikiwemo El ClΓ‘sico)
Ni kamati ambayo ilikuwa na mamlaka ya kuamua nani apandishwe daraja kwenda La Liga, na nani ashushwe daraja.
Huyu Negreria amepata umaarufu kupitia tuhuma mbaya zilizofanya kesi yake kupewa jina lake.
Jina lake limekuwa kubwa kimataifa kutokana na "Kesi ya Negreira" (Negreira Case).
Unaweza kujiuliza Kwanini?
Jibu hili hapa.
Kampuni zake binafsi zilibainika kupokea mamilioni ya euro sawa na zaidi ya bilioni 20 za kitanzania kutoka kwa klabu ya Barcelona wakati yeye akiwa bado kiongozi wa marefa.
Na ukumbuke kuwa mwaka 2016 refa msaidizi Pau Norbert CebriΓ‘n Devis. alikuwa suspended kwa wiki mbili kufuatia ushahidi wa wazi ambao ulimkuta na hatia ya kuipendelea Barcelona kila inapochezwa El Classico.
Pau Norbert CebriΓ‘n Devis. alikuwa hadi dressing room ya Barcelona anaingia, hadi kwenye korido za kuelekea dressing room alikuwa pamoja na wachezaji wa Barcelona.
Mechi ya Argentina Vs Netherlands kwenye World Cup ya 2022, ni mechi ambayo ilikuwa na matukio mengi ya vurugu, faulo nyingi huku Argentina wakiepuka adhabu nyingi ikiwemo matukio ya kadi nyekundu.
Wanna know who was incharge that day?
Kwenye nusu fainali ya Copa America ya 2007 kuna tukio moja tata alifanya Messi la kushika mpira kwa mkono tena makusudi katika dakika za mwisho za mchezo.
Na wakati huo Messi alikuwa tayari ana kadi ya njano aliyoipata kwenye michezo iliyopita, hiyo ina maana angepewa kadi ya pili ya njano kwa kosa la kushika mpira kwa mkono ingemfanya akose mechi ya fainali.
Lakini hakupewa kadi ya njano.
Septemba 2014 aliyekuwa refa mstaafu Carlos ChandΓa aliyechezesha hiyo mechi ya nusu fainali, alifanya mahojiano na kituo cha habari cha ESPN alisema hivi namnukuu
"
Nilienda kwa Messi na kumwambia: 'Hili kosa ni la kadi ya njano, lakini ishu hii itakugharimu jezi yako.' Sikuonyesha kadi."
Kwa hiyo kosa la Messi lilikuja kuwa solved kwa jezi.
Ndio maana nasisitiza muda mwingine it's not about giving an unfair penalty or red card, sometimes the referee helps by calling every 50-50 foul is one team's favour.
Hiyi ndio maana ya systematic corruption inavyofanywa.
Najua humu ndani baadhi yenu hamumpendi kabisa Ronaldo na kwa Messi mna upendo wa kuwafanya hadi muonekane vipofu, you would rather be in delusion than be corrected. That's also fine.
Kwenu naweza kusema ni sawa kusapoti na kusherehekea cheating lakini tambua watu wanasema Karma always hit back.
Rodri kachukua tuzo ya Golden ball akiwa hana assist, hana goli sijui kuhusu dribbles kama anazo ila nauhakika sio kwa kiwango cha kum outnumbered Messi.
Situation kama hii ya Rodri ingemkuta Messi, miongoni mwenu hakuna ambaye angeweza kuthubutu ku doubt uhalali wa hiyo tuzo.
Now Karma is coming back.