2026 FIFA World Cup - Special Thread

Kwenye soka lolote linaweza kutokea lakini sioni namna gani Wanaweza kupambana na Argentina. Argentina safari yake itafika mwisho kama atakutana na England semi final
Norway ndiyo timu itakayotoa upinzani mkali kwa Argentina kwenye Semi-Final.

#Hallelujah!!!
 
FBI ipo kwenye hatua ya awali ya uchunguzi (preliminary investigation) na kulingana na taarifa zilizochapishwa na lile gazeti Nancion (sina hakika na spelling zake)

Gazeti hilo lilidai kuwa FBI ipo kwenye hatua ya kukusanya ushahidi kuhusu viongozi wa AFA na uhusiano wa kampuni ya TourprodEnter LLC iliyopo Marekani.

Kinachofanya FIFA waingie kwenye huu msala ni kutokana na tuhuma za utakatishaji fedha ambao unamkabili Raisi wa AFA na wenzake.

Hizo pesa zinawa link FIFA kwasababu wao ndio waliokuwa wahusika kwenye kutuma hizo pesa ambapo walitakiwa wazitume kwenye account rasmi ya AFA kule Argentina.

Badala yake zikatumwa kwenye account ya TourprodEnter LLC.

Kwanini FIFA inahusishwa? FIFA ndio mwenye mamlaka ya utoaji na uidhinishaji wa malipo au zawadi kwa washindi.

Na kisheria FIFA ina idaranya ukaguzi ambayo inalazimika kuzuia fedha kwenda kwenye account binafsi au taasisi isiyoeleweka.

Sasa pamoja na hayo bado FIFA walisaini na kuidhinisha hayo malipo.

FIFA haiishii tu hapo kwenye kulipa haya mashirikisho pesa za ushindi na zawadi, FIFA pia wana mandatenya kukagua hesabu na matumizi ya hayo mashirikisho ambayo yapo chini yake.

Na kingine kikubwa zaidi ambacho kinampa title Romain Molina ni uchunguzi wa kashfa za unyanyasaji wa kijinsia.

Mmoja wa makocha wa zamani wa bijana aliwahi kushtakiwa kwa unyanyasaji na wachezaji kadhaa lakini FIFA walifunga jalada la kesi hii bila kuchukuliwa hatua huyo muhusika kwa madai ya kwamba hakuna ushahidi wa kutosha.

Unaikumbuka ile kashfa ya FIFA Gate ya 2015?

Pattern zake jinsi ilivyoanza inafanana kabisa na hi sakata.

Ngoja mpaka mtu aliwe kichwa ndio mtaamini.
 
We subiria Molina aendelee Kutoa habari, huwezi mfananisha Molina na hivyo vijarida, unaweza ukauweka ushahidi hapa hizo hela zimeingia kwenye Mali za viongozi wa AFA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…