2025, nchi iwe na Bunge lenye weledi

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,060
Hatushangai sana kwa uduni wa Bunge la sasa. Kwa vyovyote inatokana na namna lilivyopatikana, na pia inatokana na ubaya wa katiba tuliyo nayo.

Bunge hili la sasa, halina faida yoyote kwa yeyote, labda kwa familia za wanaoliunda, yaani hao wanaoitwa wabunge.

Bunge bandia upatikanaji wake ulikuwa kwa njia bandia, ambapo mtu mmoja aliamua kuwateua watu kuwa wabunge, lakini ukweli ni kwamba, lengo lilikuwa kuwafanya kuwa vikaragosi wake.

Kwa hiyo, hasa zaidi walitafutwa watu walio na uwezo mdogo, upeo mdogo, au watu wanafiki ambao uwezo wao unaishia kwenye kuitikia NDIYO na kuimba nyimbo za kumsifu aliyewateua.

Hawa waliteuliwa wakafanye kazi moja tu, ya kuimba nyimbo za aliyewateua kwa namna ambayo aliyewateua alitaka waimbe.

Mtu mwenye akili nzuri kabisa, aliyeelimika kikamilifu (siyo kukaa tu darasani miaka mingi), mwente weledi, anayejitambua kuwa yeye ni mwanadamu aliye na akili timamu, mkweli wa nafsi, hata siku moja hawezi kukubali kufanywa kuwa kikaragosi. Hivyo hawa waliopo huko Bungeni hawana hizi sifa ndiyo maana walikubali kuwa vikaragosi.

Japo, najua kwa hii nchi yetu haiwezekani, ilifaa sana Bunge hili la sasa lisilo na faida lingefutwa. Serikali ikatekeleza mambo yote, kuanzia kupanga bajeti, kupitisha na kuisimamia, na ofisi ya CAG ikafanya kazi kikamilifu. Report zote za CAG zikajadiliwa kwenye Bunge litakaloundwa baada ya uchaguzi wa 2025.

Faida ya jambo hili, kwanza tungeokoa pesa nyingi wanayolipwa wabunge wasio na faida, na taasisi zake. Pesa ambayo ingetumika na Bunge ingetumika kutengeneza mradi mmoja au miwili mikubwa ambayo itabakia kuwa kumbukumbu, ambayo ingeweza kuwaajiri baadhi ya vijana wetu wanaohangaika kutafuta ajira.

Hili Bunge la sasa, uwezo wake unaishia kujadili vitu vidogo vidogo visivyo na tija wala faida kubwa kwa nchi na kwa wananchi. Mambo yaliyo muhimu kama vile report ya CAG, ni mambo makubwa mno kwa watu ambao walijua kuwa kuwepo kwao bungeni ilikuwa kwenda kuimba mapambio ya kusifu na kumwabudu mtawala.

Hiyo ni kazi rahisi sana maana ilihitaji tu maandalizi ya sauti ya kusema NDIYO kwa nguvu ili uonekane, hayakuhitaji maandalizi ya akili wala weledi.

Tunavyoelekea 2025, tuanze kuwaona watu wanaofaa kuwa wabunge mapema, nje ya hawa waliosukumiziwa ubunge. Tupate watu wapya kabisa, walio wakweli wa dhamira na nafsi, wenye uelewa mkubwa, weledi mkubwa, upeo mkubwa, wasioandamwa na njaa za tumboni na vichwani, wanaoamini kuwa wao ni binadamu kamili wenye uwezo wa kufikiri na kuamua, siyo wale ambao wanaamini kwenda Bungeni, ni kufanya kazi ya unafiki wa kumpamba Rais ili kuvizia uwaziri.

Kwa upande mwingine, kama katiba mpya itakuwa haijakamilika, mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yaambatane na mabadiliko ya muundo wa Serikali utakaowaondoa wabunge kuwa mawaziri, kufuta nafasi za wakuu wa wilaya, na kuwatambua ma-OCD kuwa wakuu wa kamati za ulinzi na usalama kwenye wilaya zao.
 
Yaani bunge linakuwa duni kwa kuwa hakuna matusi ya akina sugu na lema ?

USSR
 
Uzi wa maana lakini tayari watu wameanza kumwaga uharo.
Wanafanya hivi kwa makusudi maana wanauona ukweli mchungu, namna pekee ni kumwaga shombo ili wapoteze watu kwenye uzito wa hoja yenyewe. Watu kama hawa hawakosekani kokote, cha muhimu ni kuwapuuza.
 
Bunge hili la sasa, halina faida yoyote kwa yeyote, labda kwa familia za wanaoliunda, yaani hao wanaoitwa wabunge.

Bunge bandia upatikanaji wake ulikuwa kwa njia bandia, ambapo mtu mmoja aliamua kuwateua watu kuwa wabunge, lakini ukweli ni kwamba, lengo lilikuwa kuwafanya kuwa vikaragosi wake.
Tuombe 2025 tukawe na Bunge lenye rodhaa ya wananchi tofauti na ubakaji uliofanywa na yule mwovu!
Bunge halina mvuto kabisa na limekuwa la kisanii mno! halina watu wenye kujua kujengqa hoja badala yake ni hoja nyepesi.
 
Uzi wa maana lakini tayari watu wameanza kumwaga uharo.
Watu kama USSR, Jilala, and the like, ni wa kupuuzwa. Hawajawahi kutoa mchango wowote wa maana kwenye hoja yoyote.

Tukubali tu kuwa kila mahali watu wenye mawazo na matendo ya hovyo hawakosekani. Ukishawatambua, unawapuuza.
 
Wanafanya hivi kwa makusudi maana wanauona ukweli mchungu, namna pekee ni kumwaga shombo ili wapoteze watu kwenye uzito wa hoja yenyewe. Watu kama hawa hawakosekani kokote, cha muhimu ni kuwapuuza.
Hakika umenena vema sana.
 
Hakuna bunge hapo zaidi ya kusanyiko la majangili
Ni genge la kufilisi pesa ya umma. Hakuna justification ya malipo kwa watu hawa. Wabunge pekee wanaostahili kulipwa ni wale waluoteuliwa Rais. Wabunge wengine uhalali wao ni kura halali za wananchi.

Fikiria pale Shinyanga, Masele alipata kura 320 za wajumbe. Katambi alipata kura 3. Akakatwa Masele, wakakatw wapinzani, Katambi akapewa ubunge na unaibu Waziri. Hao ndio waliojaa huko Dodoma.
 
Kwa mfumo wetu huu wa katiba na tume yetu ya uchaguzi ni ngumu kupata bunge lenye weledi maana sifa ya kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika kwa sifa hii tu hatuwezi pata bunge lenye weledi hata siku moja zaidi ni kupata vilaza.

Tunahitaji kufanya mageuzi ya kimfumo ya kiutawala na hapa ndo hoja ya katiba mpya inachukua nafasi ya kipekee kabisa kama kweli tuna nia ya dhati basi tunapaswa kama taifa kufanya agenda ya katiba mpya kuwa agenda ya kitaifa na Wala sio kusubili hisani ya watawala maana watawala wanapita lakini uhai wa taifa ni bora kuliko uhai wa mtawala.
 
Back
Top Bottom