2025, nchi iwe na Bunge lenye weledi

2025, nchi iwe na Bunge lenye weledi

Hatushangai sana kwa uduni wa Bunge la sasa. Kwa vyovyote inatokana na namna lilivyopatikana, na pia inatokana na ubaya wa katiba tuliyo nayo.

Bunge hili la sasa, halina faida yoyote kwa yeyote, labda kwa familia za wanaoliunda, yaani hao wanaoitwa wabunge.

Bunge bandia upatikanaji wake ulikuwa kwa njia bandia, ambapo mtu mmoja aliamua kuwateua watu kuwa wabunge, lakini ukweli ni kwamba, lengo lilikuwa kuwafanya kuwa vikaragosi wake.

Kwa hiyo, hasa zaidi walitafutwa watu walio na uwezo mdogo, upeo mdogo, au watu wanafiki ambao uwezo wao unaishia kwenye kuitikia NDIYO na kuimba nyimbo za kumsifu aliyewateua.

Hawa waliteuliwa wakafanye kazi moja tu, ya kuimba nyimbo za aliyewateua kwa namna ambayo aliyewateua alitaka waimbe.

Mtu mwenye akili nzuri kabisa, aliyeelimika kikamilifu (siyo kukaa tu darasani miaka mingi), mwente weledi, anayejitambua kuwa yeye ni mwanadamu aliye na akili timamu, mkweli wa nafsi, hata siku moja hawezi kukubali kufanywa kuwa kikaragosi. Hivyo hawa waliopo huko Bungeni hawana hizi sifa ndiyo maana walikubali kuwa vikaragosi.

Japo, najua kwa hii nchi yetu haiwezekani, ilifaa sana Bunge hili la sasa lisilo na faida lingefutwa. Serikali ikatekeleza mambo yote, kuanzia kupanga bajeti, kupitisha na kuisimamia, na ofisi ya CAG ikafanya kazi kikamilifu. Report zote za CAG zikajadiliwa kwenye Bunge litakaloundwa baada ya uchaguzi wa 2025.

Faida ya jambo hili, kwanza tungeokoa pesa nyingi wanayolipwa wabunge wasio na faida, na taasisi zake. Pesa ambayo ingetumika na Bunge ingetumika kutengeneza mradi mmoja au miwili mikubwa ambayo itabakia kuwa kumbukumbu, ambayo ingeweza kuwaajiri baadhi ya vijana wetu wanaohangaika kutafuta ajira.

Hili Bunge la sasa, uwezo wake unaishia kujadili vitu vidogo vidogo visivyo na tija wala faida kubwa kwa nchi na kwa wananchi. Mambo yaliyo muhimu kama vile report ya CAG, ni mambo makubwa mno kwa watu ambao walijua kuwa kuwepo kwao bungeni ilikuwa kwenda kuimba mapambio ya kusifu na kumwabudu mtawala.

Hiyo ni kazi rahisi sana maana ilihitaji tu maandalizi ya sauti ya kusema NDIYO kwa nguvu ili uonekane, hayakuhitaji maandalizi ya akili wala weledi.

Tunavyoelekea 2025, tuanze kuwaona watu wanaofaa kuwa wabunge mapema, nje ya hawa waliosukumiziwa ubunge. Tupate watu wapya kabisa, walio wakweli wa dhamira na nafsi, wenye uelewa mkubwa, weledi mkubwa, upeo mkubwa, wasioandamwa na njaa za tumboni na vichwani, wanaoamini kuwa wao ni binadamu kamili wenye uwezo wa kufikiri na kuamua, siyo wale ambao wanaamini kwenda Bungeni, ni kufanya kazi ya unafiki wa kumpamba Rais ili kuvizia uwaziri.

Kwa upande mwingine, kama katiba mpya itakuwa haijakamilika, mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yaambatane na mabadiliko ya muundo wa Serikali utakaowaondoa wabunge kuwa mawaziri, kufuta nafasi za wakuu wa wilaya, na kuwatambua ma-OCD kuwa wakuu wa kamati za ulinzi na usalama kwenye wilaya zao.
Uzi bora kabisa huu.
Lile jitu sijui lilikusudia kutuachia ya namna gani sijui.
Ndo mana Lisu alisema tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea.
Sio rahisi kuyasema mabaya yote ya shetani lile. Itoshe tu kumweka kwenye kumbukumbu vizazi vijavyo visije vikaangamia kwa kuweka mtu wa aina ile.
 
Yaani bunge linakuwa duni kwa kuwa hakuna matusi ya akina sugu na lema ?

USSR
Mwenyewe umeridhiiika unaona hili bunge bora kwa kuwa tu liliwekwa na lile shetani lenu la Chato
 
Hatushangai sana kwa uduni wa Bunge la sasa. Kwa vyovyote inatokana na namna lilivyopatikana, na pia inatokana na ubaya wa katiba tuliyo nayo.

Bunge hili la sasa, halina faida yoyote kwa yeyote, labda kwa familia za wanaoliunda, yaani hao wanaoitwa wabunge.

Bunge bandia upatikanaji wake ulikuwa kwa njia bandia, ambapo mtu mmoja aliamua kuwateua watu kuwa wabunge, lakini ukweli ni kwamba, lengo lilikuwa kuwafanya kuwa vikaragosi wake.

Kwa hiyo, hasa zaidi walitafutwa watu walio na uwezo mdogo, upeo mdogo, au watu wanafiki ambao uwezo wao unaishia kwenye kuitikia NDIYO na kuimba nyimbo za kumsifu aliyewateua.

Hawa waliteuliwa wakafanye kazi moja tu, ya kuimba nyimbo za aliyewateua kwa namna ambayo aliyewateua alitaka waimbe.

Mtu mwenye akili nzuri kabisa, aliyeelimika kikamilifu (siyo kukaa tu darasani miaka mingi), mwente weledi, anayejitambua kuwa yeye ni mwanadamu aliye na akili timamu, mkweli wa nafsi, hata siku moja hawezi kukubali kufanywa kuwa kikaragosi. Hivyo hawa waliopo huko Bungeni hawana hizi sifa ndiyo maana walikubali kuwa vikaragosi.

Japo, najua kwa hii nchi yetu haiwezekani, ilifaa sana Bunge hili la sasa lisilo na faida lingefutwa. Serikali ikatekeleza mambo yote, kuanzia kupanga bajeti, kupitisha na kuisimamia, na ofisi ya CAG ikafanya kazi kikamilifu. Report zote za CAG zikajadiliwa kwenye Bunge litakaloundwa baada ya uchaguzi wa 2025.

Faida ya jambo hili, kwanza tungeokoa pesa nyingi wanayolipwa wabunge wasio na faida, na taasisi zake. Pesa ambayo ingetumika na Bunge ingetumika kutengeneza mradi mmoja au miwili mikubwa ambayo itabakia kuwa kumbukumbu, ambayo ingeweza kuwaajiri baadhi ya vijana wetu wanaohangaika kutafuta ajira.

Hili Bunge la sasa, uwezo wake unaishia kujadili vitu vidogo vidogo visivyo na tija wala faida kubwa kwa nchi na kwa wananchi. Mambo yaliyo muhimu kama vile report ya CAG, ni mambo makubwa mno kwa watu ambao walijua kuwa kuwepo kwao bungeni ilikuwa kwenda kuimba mapambio ya kusifu na kumwabudu mtawala.

Hiyo ni kazi rahisi sana maana ilihitaji tu maandalizi ya sauti ya kusema NDIYO kwa nguvu ili uonekane, hayakuhitaji maandalizi ya akili wala weledi.

Tunavyoelekea 2025, tuanze kuwaona watu wanaofaa kuwa wabunge mapema, nje ya hawa waliosukumiziwa ubunge. Tupate watu wapya kabisa, walio wakweli wa dhamira na nafsi, wenye uelewa mkubwa, weledi mkubwa, upeo mkubwa, wasioandamwa na njaa za tumboni na vichwani, wanaoamini kuwa wao ni binadamu kamili wenye uwezo wa kufikiri na kuamua, siyo wale ambao wanaamini kwenda Bungeni, ni kufanya kazi ya unafiki wa kumpamba Rais ili kuvizia uwaziri.

Kwa upande mwingine, kama katiba mpya itakuwa haijakamilika, mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yaambatane na mabadiliko ya muundo wa Serikali utakaowaondoa wabunge kuwa mawaziri, kufuta nafasi za wakuu wa wilaya, na kuwatambua ma-OCD kuwa wakuu wa kamati za ulinzi na usalama kwenye wilaya zao.
Tuna vioja kule mjengoni
 
Kwani ni mwaka gani tangu tupate uhuru Tanzania imewahi kuwa na Bunge imara?
Bunge letu la Tanzania limefunga ndoa na serikali kupitia CCM na ndiyo maana Wabunge wa CCM wakitaka kuisimamia serikali ipasavyo wanaitwa kwe Party Caucus kupewa onyo na vitisho!
 
Tuombe 2025 tukawe na Bunge lenye rodhaa ya wananchi tofauti na ubakaji uliofanywa na yule mwovu!
Bunge halina mvuto kabisa na limekuwa la kisanii mno! halina watu wenye kujua kujengqa hoja badala yake ni hoja nyepesi.
bila tume huru; bado nina wasi wasi
 
Kuna siku eti babutale kasimama anataka kuliimbisha bunge wimbo wa mama Amina. Mimi sitegemei kitu chochote Kwa hili bunge
 
Unataka bunge lenye weledi kwa tume ileile ya uchaguzi. Ok ngoja tuone huruma ya mama
 
Uko sahihi@Bams.
Katiba yetu mbovu ilituletea Rais mbovu, naye akatuletea Bunge bovu - yote kwa gharama na hasara za Taifa.

Kuna watu eti wanadanganywa Katiba Mpya si muhimu maana haimpi mtu chakula, ajira nk halafu wanakubali. Ni wapumbavu.

Gharama za kuendesha Serikali mbovu, kufanya "chaguzi" hewa na bandia, kuwa na bunge bovu, "mipango" na matumizi mabovu ya rasilimali, tozo haramu, mikataba mibovu, miradi hewa nk nk - Katiba Mpya ndio dawa yake. Katiba inaathiri na kugusa nyanja zote, inagusa vitu ambavyo mwishoni vinagusa moja kwa moja maisha na vipato vya watu mpaka chini. Lakini hao waitwao "wanyonge....wavuja jasho...." ndio wa kwanza kushabikia wabaki na katiba hii mbovu inayowaumiza na kuwakandamiza! Incredible!

Mwisho, Rais hawezi kuacha kuteua mawaziri toka miongoni mwa wabunge maana hilo ni takwa la Katiba ya sasa.

Pia Katiba ya sasa haiwezi kuzaa Tume Huru ya Uchaguzi, IMPOSSIBLE! Katiba ya sasa itaendelea kutupa Tume mbovu na chaguzi mbovu. FACT.

Hatujitaji viraka, tunadai na kutaka Katiba Mpya kabla ya uchaguzi wa 2025. Mbona muda na rasilimali viko vya kutosha kutekeleza hilo?

HITIMISHO:

Wanaita "utashi", mimi naita NIA (motive, intent, will). 'Penye NIA pana njia', lakini sio penye utashi pana njia.

Utashi is a bit lousy 'politically correct' phrase. No commitment, no responsibility, no accountability, no purpose or plan; everything is just relative to 'moods' and is subjective to feelings. Laissez faire type.
You will never accomplish anything of note or value with that approach. NEVER!

Mwaka mmoja wa serious work unatosha kabisa kutupa katiba nzuri, safi na itakayotupeleka next level.
 
Kwa uwezo wako wa kuelewa, bunge la ndio mzee kwako ndio bunge sahihi. Hakuna wa kukulaumu kwenye hili.
Bunge likiwa na Wabunge haramu kwa jinsi walivyoingia na lenyewe litakuwa HARAMU!! Ukijumuisha na kuwaruhusu COVID 19 kukaa bungeni!
 
Back
Top Bottom