2022 Tutatoboa?

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
341
301
Ni siku ya pili ya mwaka 2022. Wapo watu ambao tayari washapanga malengo na mipango kwa mwaka huu wengine bado tunaendelea kupanga nini tufanye.

Jambo moja ambalo litatusaidia kufikia malengo yetu ni kuwa na IMANI ya ushindi juu ya mipango na malengo yetu.

Ni vyema kuwa na malengo lakini kuwa na imani ya kufanikiwa katika yale tuliyoyapanga ni jambo kubwa zaidi hata ya malengo na mipango yenyewe.

Ujionavyo nafsi mwako ndiyo silaha kuu ya kutoboa ama sumu ya kuuua mipango uliyonayo. Hata Bible inasema Mithali 23;7 “Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo”~Mithali 23:7.

Kama unajiona hutatoboa katika malengo uliyonayo kaa chini na ujiulize; kwanini sitatoboa na tatizo lipo wapi hasa. Kama ukikosa imani kabisa ni bora ubadilishe malengo yako na kupanga malengo ambayo ndani yako utaamini kuwa utafanikiwa.

Faida kubwa ya Imani iliyoko ndani yako nikukusukuma wewe kila siku kufanya kazi kwa bidii bila ya kuchoka.

Vilevile itakusaidi kukabiliana na changamoto na vizingiti vyote kwani ndani yako unaamini ushindi upo upande wako na hata likiwa gumu kiasi gani unaamini hilo litapita tuu.

Kinyume chake ni kwamba kutokuwa na imani juu ya malengo yako hata changamoto ndogo kama sisimizi ikija itakuangusha tuu kwani moyoni wewe ushajiona ni wakushindwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom