2021 unaenda kuwa mwaka mmoja mgumu sana kwa Watanzania, usipojipanga utakupanga

Mtu anayeitwa mpumbavu ni yule yeyote asiyejielewa! Unashabikia vitu vya kijinga, unajua kabisa nguvu huna unataka kupambana na mwenye nguvu, hekima ni kumkwepa mwenye nguvu. Ndo maana nikasema wakina Nyerere walikuwa na hekima, wakubwa wanaposema habari ya ushoga hawa maanishi wanataka mfirane, hapana. Ila kutetea haki za binadamu, yaani maisha ya binadamu yaheshimiwe kwa namna yoyote, la sivyo tutaanza kuona damu za mashoga zikimwagika na baadaye watakuja walevi na baadaye wazinzi nk.
Wakubwa wanataka equilibrium , dunia itulie sio kuleta harakati, ndo maana hata waovu wengine kama mashoga hawamdhuru mtu, wameunda chama ili kujitetea wasi fuatwe fuatwe.
Hivyo nitaendelea kutumia neno wapumbavu hadi akili zitakapoingia na ufahamu kuonekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasamehe mkuu ni elimu tu wamekosa kidogo. Ila tutaendelea kuwaimbia hivi mpaka akili ziwakae sawa
 
Wahenga wanasema, ‘’siasa ni maisha, lazima uyaishi’’. Kwa namna moja ama nyingine, siasa itashawishi mtindo na mwelekeo wa maisha yako. Yaweza kuwa mwelekeo wa peponi wa kukenua meno ama yaweza pia kuwa mwelekeo wa maisha ya kuzimu ya jasho la damu.

Kuna nchi tumeshuhudia zilikuwa na maisha ya furaha, amani, na maendeleo lakini kutokana na matokeo ya maisha ya siasa mambo yamebadilika kwa haraka. Nchi kama Venezuela, ambayo kwa wakati mmoja iliwahi kuwa nchi yenye uchumi mkubwa America ya Kusini lakini leo hii imedumbukia kuzimu. Zimbabwe na Libya hali kadhalika kwa wakati mmoja zilikuwa nchi zilizopigiwa mfano hapa barani Afrika.

Hiyo ni mifano ya namna gani mambo katika nchi na raia wake yanaweza kubadilika ndani ya kipindi cha mda mfupi. Na ubaya wa kuogofya ni kwamba katika nchi hizi zote, ilichukua mda mchache sana kuanguka kwenda kuzimu, na tangu waanguke ni miaka sasa hawana dalili za kuinuka tena. (Hili tuliweke akilini)

Madhila yaliyowakuta Venezuela, Zimbabwe, na Libya ni sababu zinazofanana. Na nchi zote hizo ziliadhibiwa bila huruma na viranja wa dunia baada tu ya viongozi wao wa kisiasa na serikali zao kuonesha vitendo ambavyo vilitafsiriwa na viranja wa dunia kama ukiukwaji wa haki za binadamu.

Ni ukweli usiopingika, kwa namna mambo yanavyojidhihirisha kwa sasa, Tanzania na sisi kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, tupo katika rada ya viranja wa dunia. (Hakuna wa kupinga hili) Tupo katika rada ya kuelekea kushughulikiwa kama zilivyoshughulikiwa nchi nilizozitaja hapo juu. (Kwa maoni yangu).

Kwa sasa viranja wamejipanga kila idara, kikubwa kinachongojewa ni uchaguzi wa October 2020. Wenyewe wameshajua kwamba ni vigumu uchaguzi ukawa wa haki na usawa, hata sisi watanzania wengine tunajua kwamba uchaguzi hauendi kuwa wa haki na usawa. (Nadhani pia ndo mana wamenza kuzikoki bunduki zao mapema tayari kutulenga).

Wapinzani wenyewe wanajua hatuendi kuwa na uchaguzi huru, haki na usawa, kwa hiyo nahisi kinachofanyika; wanaenda kuwa chambo ya kudhihirisha dunia ni namna gani Tanzania inavovunja haki za binadamu.

Mbinu za kushughulikiwa ni zile zile za kibepari ambazo matokeo ndo yataleta shuruba kwa maisha ya watanzania.

  • Kwanza kabisa, vikwazo vya kibiashara havikwepeki,.. (Nachoka akili nikifikiri kwamba tukizuiwa kuuza madini na mazao) tutapataje fedha za kigeni.. (KIZA KINENE)
  • US na EU wanaweza kuzuia raia wao kuzuru Tanzania ( hapo utalii ndo mwanzo wa mwisho).. Hii ilifanyika ZIMBABWE na kwetu itaweza fanyika pia
  • Misaada yote ya donnors pia ndo inapata ground za kukatwa moja kwa moja kwa kigezo cha ukiukwaji wa haki za binadamu.
  • Moody’s lazima waingie kazini halafu waanze kusema wamei downgrade Tanzania. (Ikumbukwe nchi ikishakuwa Downgraded means hapo inakuwa ngumu hata kupata mikopo nje ya nchi maana wanakuambia risk of default inakuwa ni kubwa)
  • Hii reserve yetu kiduchu ya dola nadhani ndo itatuumbua mapema sana, mambo yakishakuwa hovyo demand ya dola itaanza kuwa kubwa, hao makabachori wana passport mbili mbili huwez kuwaona bongo tena watataka ku change mipunga yao wapeleke kwenye dola watimke mpaka mambo yatapokaa sawa. Hapo sasa ndo kimbembe unaweza shangaa mwezi wa 12 dola ishafika 3000.
  • Dola ikianza ku shoot inflation na yenyewe inaanza kuitikia ni pua na mdomo ( Jiuulize ni kwanini nchi kama Venezuela, Zimbabwe soon baada ya kushughulikiwa ni kwanini inflation zili shoot sana?)
  • Hapo tusiombe machafuko, maana yakitokea, ICC wapo hapo matakoni yaani ni shida kila idara.
Kwa ufupi sana ni kwamba nchi yetu imejiingiza kwenye mtego mmoja mmbaya sana, na kadri mda unavozidi kwenda nahisi kama tunazidi kudidimia kwenye shimo. Ilichobaki sasa ni Raia kama Raia ujue kama mambo yakianza kudorora utakuwa umejipanga kivipi.

Ni dhahiri usipojipangwa lazima hii 2021 ikupange. Mabepari hawana huruma, wanataka wakianza kupiga dunia ishuhudie, na dunia haiwezi kushuhudia kama Raia hawatoki jasho la damu.

Niwalaumu tu viongozi wetu moja kwa moja kwa kutuingiza kwenye hii madhila, Iwe iwavyo, fikiria kwa vyovyote, Viranja wa dunia wanataka regime change Tanzania, wasipoipata regime change lazima watafute namna tushughulikiwe.

Huku na huku wakina Bibi Kidawa Manzese wanakuambiwa CCM Mbele kwa Mbele. Hivi akina Bibi Kidawa wanajua viranja wa dunia wamepanga kitu gani?

Nipo kujiandaa na 2021

N.Mushi
Umeaema yote kwa usahihi na ukweli. Ni ukweli unaouma lakini kwa hali halisi haukwepeki. Wenye uwezo na mamlaka ya kuidadili hali ya mambo wameweka pamba masikioni sababu mfumo uliopo unawafavour na wala hawaioni hatari hiyo ijayo.

Hakuna jinsi ya kujiandaa mtu binafsi kujiponeaha maana system zikishakuwa corrupted kila kitu hakitaenda.Tusubiri kunyolewa tu, hamna namna.
 
Mkuu 'Kamongo', mbona unajichanganya mwenyewe.
Mwanzo umesema "sisi sio wamoja, tunachukiana wenyewe...; halafu hapo hapo unasema "ni rahisi sana hao mabeberu kutuchonganisha."

Ina maana unawasingizia mabeberu kuwa wachonganishi..

Ukweli uliopo ni kwamba umoja wetu unavurugwa na viongozi wetu waliopo madarakani sasa hivi na sio 'mabeberu'. Tuache visingizio visivyokuwa na sababu yoyote.

Haihitaji 'mabeberu' tena kuja kutuchonganisha, tayari sisi wenyewe tumekwishajichonganisha.

Na kwa kweli sasa hivi hata haihitaji 'mabeberu' kuja kutuangamiza, hata hawa viji'beberu', na majirani zetu tu, kama Rwanda akitaka kwa sababu yoyote ile anaweza kututwanga tu huku tukimsaidia kutusambaratisha.
Nakubaliana na wewe kwa hali ilivyo sasa viongozi wetu ndio wa kulaumiwa,wametengeneza Uadui mkubwa baina yao na wananchi
 
Usibishe sana mkuu pitia kwanza historia, pia geopolitics za dunia uzielewe vema ndo uweze kuandika. Upo na mawazo local sana mpaka nakushangaa
Ni hasara kubwa sana kwa kizazi hiki cha leo kuwa na fikra potofu kama hizi.

Hii sasa ni zaidi ya mababu zetu. Wao anagalao hawakuwa na 'exposure' iliyowawezesha kujua dunia ilivyo na kutambua umhimu wa ubinaadam wao.

Leo hii tuna watu wanajipeleka wenyewe tena kwenye kudhalilishwa? Ilikuwa na maana gani ya kudai uhuru wetu kama tunajua 'neo-colonialism' ni nzuri kuliko ukoloni, si bora tungekazana tu tuingie moja kwa moja kwenye hiyo 'neocolonialism' mnayoililia?

Kizazi chenye hasara kabisa hiki.
 
Wewe wacha huo ubishi unajiaibisha.. kwenye mambo ya mikopo huwa kuna ambayo inakuwa renewed year on year. Mfano kama Stand By facilities. Sasa endapo wakisema hawawezi ku renew na nchi inahitaji pesa unadhani itakuwaje. Unajidhalilisha sana acha kupisha vitu hujui mkuu. BTW usidhani ubishi wako utakuongezea maksi za kuwa mtanzania zaidi yangu.
Unazidi kujidhalilisha aisee!
Mara hii umekwishakimbilia kwenye 'standby', na huko juu unazungumzia "kulipa kwa mkupuo."
Nimekuuliza ni wapi ilishafanyika hivyo; hujibu unazunguka kwingine kabisa.
 
Y
Kwanza ukae ukijua sisi sio wamoja,tunachukiana wenyewe kwa wenyewe kuna mgawanyiko mkubwa katika jamii yetu,ni rahisi sana hao mnaowaita mabeberu kutuchonganisha
Watawala wamerudia makosa waliyofanya gadafi na saddam kutowaunganisha watu wao adui akawatumia waliotengwa kuwasambaratisha.Panapo umoja hakuna utengano.Taifa lolote lisilo na umoja haitaji dakika 10 kulisambaratisha.Watawala awakuliona hilo
 
Kwa hiyo mabeberu watatupiga njaa, bora kuongeza ushirikiano na nchi kama china na urusi kwa sababu wao hawana hiyana sana
Mrusi labda akupe silaha sio Pesa yuko hoi kiuchumi,mchina tumemnyima miradi mikubwa hivo sio tegemeo
 
Nashindwa kuelewa mleta uzi anataka nini? Kwani ili uchaguzi uwe Huru na wa haki ni kwamba lazima nchi ichukuliwe na upinzani? Nafikiri hawa wenzetu hawana rafiki wala adui wa kudumu. Kilichopo waje wawepo wakati wa uchaguzi. Wakisubiri kuambiwa haitakuwa sawa.
Ukiruhusu uchaguzi huru ni kutoitendea haki ccm itakufa
 
Wao waje Wamchukue mtu wao wakamshughulikie uko uko, sisi hatutaki kesi mtu Mwenyewe ashauriki Nchi anaiona kama mali yake anafanya anachojisikia, kauli za ovyo/za kukera
 
Mkuu 'Ben Bella'; nitakujibu kwa upole sana, kwa sababu naona unapata shida kweli kuelewa unachosoma.

Lakini kwanza nieleweshe tafadhali, "MATAGA" ndio akina nani? Pamoja na kunipa jina/cheo hicho, kwa bahati mbaya kwangu hakina maana yoyote kama sikijui!


Kiufupi mkuu wangu 'Ben Bella' ni hivi: Usitegemee kabisa na kufurahia kwamba kuna mtu yeyote toka nje atakayekuja kujufanyia kazi ambayo ni kazi yako wewe, na mimi, na waTanzania wote kwa ujumla wetu.

Hii ni kazi yetu, unataka ukawatafute watu wengine waje wakukomboe wewe, kwa sababu zipi?

Utaniambia huwezi kufanya kazi hiyo kwa vile huna jeshi na mabunduki ambayo waliowateka ndiyo wanayoyatumia kuwanyanyasa, kuwatishia, na wakati mwingine kuwaua kwa kuyatumia hayo mavyombo mliyowakabidhi wayafanyie kazi ya kulinda usalama wa nchi yetu, ..., badala yake wanayatumia kutulenga sisi.

Bila shaka swali unalouliza. tutawezaje sisi raia kukabiliana na haya masilaha bila ya kuwatumia hao 'vinara' wa dunia?

Mimi nakwambia hivi, kama upo kwenye siasa, weka kipaumbele chako kuwaelimisha wananchi. Wape elimu waelewe hatari inayotukabili. Sio lazima uitishe mikutano kuifanya kazi hiyo. Acha hicho kisingizio cha kunyimwa ruhusa ya mikutano.

Kazi zenu wanasiasa mnaolilia watu wa nje waje kuwafanyia kazi kirahisi ili nanyi mpate njia ya kwenda kuwakandamiza waTanzania, hilo lisahaulini. Lazima mtoke jasho, tuone kweli mnao uchungu na nchi yetu.

Njoni huku vijijini, 'mlango kwa mlango', 'jirani kwa jirani', 'klabu ya pombe kwa klabu ya pombe', mke/mme, n.k.; fanyeni kazi. Tuelezeni tujue nchi yetu inakoelekea.

Wakati mkiyafanya haya, 'of course' baadhi yenu mtakuwa mkishirikisha 'Jamii ya Kimataifa', hata hao 'wabae' wa dunia wajue mnahitaji msaada wao katika mambo kadhaa ambayo nyinyi hamna uwezo nayo - kama hayo ya mabunduki; wayazuie hayo mabunduki, na kuhakikisha maandaizi ya kupiga kura yatakuwa huru na haki kwa kila raia atakayeshiriki.

Sasa niambie, hapo shida ipo wapi? Unalilia watu waje wakukomboe, kumbe nyenzo za kujikomboa unazo mwenyewe?

Wanachi wa nchi hii ndio pekee wa kujiletea ukombozi. Wanahitaji tu uongozi utakaosimamia harakati hizo.
Kuna watu Mna ujinga Mwingi sana Vichwani Mwenu,. Ushabiki wenu wa Kipumbavu ndo utakaotufikisha pabaya..
 
Uchaguzi wa Serikari za Mitaa umeuonaje, ulikua huru na wa haki?
Nashindwa kuelewa mleta uzi anataka nini? Kwani ili uchaguzi uwe Huru na wa haki ni kwamba lazima nchi ichukuliwe na upinzani? Nafikiri hawa wenzetu hawana rafiki wala adui wa kudumu. Kilichopo waje wawepo wakati wa uchaguzi. Wakisubiri kuambiwa haitakuwa sawa.
 
Mku wengine mbona umewaacha au wao wako pazuri?
Rome was not built on one day au overnight .(Roma haikujengwa kwa siku moja) Hivyo Majibu ya Matatizo lukuki ya Tanzania ambayo yaliikumba jamii yetu hayawezi kupatikana kwa siku moja au mwaka moja, ni mwendo wa kimoja baada ya kingine ndugu yangu.
 
Moderators!Ujinga sio tusi ni kutokujua jambo!!!magufuli anatuumiza na hajui kama tunaumia!yeye anafurahia tu wakati tunaumia!!huo ndio ujinga wenyewe!!!
 
Moderators!Ujinga sio tusi ni kutokujua jambo!!!magufuli anatuumiza na hajui kama tunaumia!yeye anafurahia tu wakati tunaumia!!huo ndio ujinga wenyewe!!!
 
Mimi hapa Napendezwa na utawala huu, Na pia sina uhakika na udhalimu unaouzungumzia unless uniwekee details za kuaminika hapa apart from those empty accusations filled with anger.

Japo si support hata kidogo sula la watu kupotea abruptly, Nashawishika kuamini kama kweli kuna mkono wa serikali basi kulikuwa na sababu ya msingi hao unawaowataja kupotezwa. Wamarekani wenyewe tu huwa hawana huruma kabisa na mtu anayetishia usalama wa Taifa lao.
Sababu za msingi zisizofahamika?
 
Kuna watu Mna ujinga Mwingi sana Vichwani Mwenu,. Ushabiki wenu wa Kipumbavu ndo utakaotufikisha pabaya..
"Robidinyo"

Sijawahi kukusoma wala kukusikia popote humu JF kwa mchango wowote wa maana, na hata hiyo mibovu kama huu hapo juu hadi hii leo.

Nitakuwa mpuuzi sana kujadili chochote na wewe kuhusu hayo uliyoandika.

Kama unayo akili timamu utaelewa nilichoandika hapa.
 
Umeaema yote kwa usahihi na ukweli. Ni ukweli unaouma lakini kwa hali halisi haukwepeki. Wenye uwezo na mamlaka ya kuidadili hali ya mambo wameweka pamba masikioni sababu mfumo uliopo unawafavour na wala hawaioni hatari hiyo ijayo.

Hakuna jinsi ya kujiandaa mtu binafsi kujiponeaha maana system zikishakuwa corrupted kila kitu hakitaenda.Tusubiri kunyolewa tu, hamna namna.
Anza kuweka akiba ya dola walau kidogo kidogo.. Mambo yakigeuka baada ya uchaguzi, impact za haraka haraka kuonekana itakuwa ni 1) Bei ya dola kupanda maana demand itakuwa kubwa sana na vile hatuna reserve ya dola ya kutosha kama nchi ina maana kupanda kwa bei ya dola kutakuwa kukubwa na kwa haraka, 2) Inflation, vitu vitapanda bei sana tena kwa haraka na hii itakuwa inatokana kwa sehemu kubwa kwa kupanda kwa bei ya dola.

Kwa mazingira hayo kama utakuwa na akiba ya shilingi ni kwamba purchasing power yako itakuwa inapungua kadri bei ya dola na inflation zitavokuwa zinapanda. So kama tayar utakuwa ulishakuwa na reserve ya dola ina maana hizi dynamics kwenye uchumi hazitakuathiri hata kidogo. Utaishi maisha kawaida kabisa maana itakuwa ni wewe kwenda kubadili dola kidogo na kufanya matumizi.

Hiyo ndo best practice mkuu. Mimi kwa upande wangu nafanya taratibu.. nimeenza ku liquidate baadhi ya uwekezaji wangu japokuwa ni mdogo na very soon before election ntakuwa nipo long kwenye dola.
 
Back
Top Bottom