2021 unaenda kuwa mwaka mmoja mgumu sana kwa Watanzania, usipojipanga utakupanga

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Wahenga wanasema, ‘’siasa ni maisha, lazima uyaishi’’. Kwa namna moja ama nyingine, siasa itashawishi mtindo na mwelekeo wa maisha yako. Yaweza kuwa mwelekeo wa peponi wa kukenua meno ama yaweza pia kuwa mwelekeo wa maisha ya kuzimu ya jasho la damu.

Kuna nchi tumeshuhudia zilikuwa na maisha ya furaha, amani, na maendeleo lakini kutokana na matokeo ya maisha ya siasa mambo yamebadilika kwa haraka. Nchi kama Venezuela, ambayo kwa wakati mmoja iliwahi kuwa nchi yenye uchumi mkubwa America ya Kusini lakini leo hii imedumbukia kuzimu. Zimbabwe na Libya hali kadhalika kwa wakati mmoja zilikuwa nchi zilizopigiwa mfano hapa barani Afrika.

Hiyo ni mifano ya namna gani mambo katika nchi na raia wake yanaweza kubadilika ndani ya kipindi cha mda mfupi. Na ubaya wa kuogofya ni kwamba katika nchi hizi zote, ilichukua mda mchache sana kuanguka kwenda kuzimu, na tangu waanguke ni miaka sasa hawana dalili za kuinuka tena. (Hili tuliweke akilini)

Madhila yaliyowakuta Venezuela, Zimbabwe, na Libya ni sababu zinazofanana. Na nchi zote hizo ziliadhibiwa bila huruma na viranja wa dunia baada tu ya viongozi wao wa kisiasa na serikali zao kuonesha vitendo ambavyo vilitafsiriwa na viranja wa dunia kama ukiukwaji wa haki za binadamu.

Ni ukweli usiopingika, kwa namna mambo yanavyojidhihirisha kwa sasa, Tanzania na sisi kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, tupo katika rada ya viranja wa dunia. (Hakuna wa kupinga hili) Tupo katika rada ya kuelekea kushughulikiwa kama zilivyoshughulikiwa nchi nilizozitaja hapo juu. (Kwa maoni yangu).

Kwa sasa viranja wamejipanga kila idara, kikubwa kinachongojewa ni uchaguzi wa October 2020. Wenyewe wameshajua kwamba ni vigumu uchaguzi ukawa wa haki na usawa, hata sisi watanzania wengine tunajua kwamba uchaguzi hauendi kuwa wa haki na usawa. (Nadhani pia ndo mana wamenza kuzikoki bunduki zao mapema tayari kutulenga).

Wapinzani wenyewe wanajua hatuendi kuwa na uchaguzi huru, haki na usawa, kwa hiyo nahisi kinachofanyika; wanaenda kuwa chambo ya kudhihirisha dunia ni namna gani Tanzania inavovunja haki za binadamu.

Mbinu za kushughulikiwa ni zile zile za kibepari ambazo matokeo ndo yataleta shuruba kwa maisha ya watanzania.

  • Kwanza kabisa, vikwazo vya kibiashara havikwepeki,.. (Nachoka akili nikifikiri kwamba tukizuiwa kuuza madini na mazao) tutapataje fedha za kigeni.. (KIZA KINENE)
  • US na EU wanaweza kuzuia raia wao kuzuru Tanzania ( hapo utalii ndo mwanzo wa mwisho).. Hii ilifanyika ZIMBABWE na kwetu itaweza fanyika pia
  • Misaada yote ya donnors pia ndo inapata ground za kukatwa moja kwa moja kwa kigezo cha ukiukwaji wa haki za binadamu.
  • Moody’s lazima waingie kazini halafu waanze kusema wamei downgrade Tanzania. (Ikumbukwe nchi ikishakuwa Downgraded means hapo inakuwa ngumu hata kupata mikopo nje ya nchi maana wanakuambia risk of default inakuwa ni kubwa)
  • Hii reserve yetu kiduchu ya dola nadhani ndo itatuumbua mapema sana, mambo yakishakuwa hovyo demand ya dola itaanza kuwa kubwa, hao makabachori wana passport mbili mbili huwez kuwaona bongo tena watataka ku change mipunga yao wapeleke kwenye dola watimke mpaka mambo yatapokaa sawa. Hapo sasa ndo kimbembe unaweza shangaa mwezi wa 12 dola ishafika 3000.
  • Dola ikianza ku shoot inflation na yenyewe inaanza kuitikia ni pua na mdomo ( Jiuulize ni kwanini nchi kama Venezuela, Zimbabwe soon baada ya kushughulikiwa ni kwanini inflation zili shoot sana?)
  • Hapo tusiombe machafuko, maana yakitokea, ICC wapo hapo matakoni yaani ni shida kila idara.
Kwa ufupi sana ni kwamba nchi yetu imejiingiza kwenye mtego mmoja mmbaya sana, na kadri mda unavozidi kwenda nahisi kama tunazidi kudidimia kwenye shimo. Ilichobaki sasa ni Raia kama Raia ujue kama mambo yakianza kudorora utakuwa umejipanga kivipi.

Ni dhahiri usipojipangwa lazima hii 2021 ikupange. Mabepari hawana huruma, wanataka wakianza kupiga dunia ishuhudie, na dunia haiwezi kushuhudia kama Raia hawatoki jasho la damu.

Niwalaumu tu viongozi wetu moja kwa moja kwa kutuingiza kwenye hii madhila, Iwe iwavyo, fikiria kwa vyovyote, Viranja wa dunia wanataka regime change Tanzania, wasipoipata regime change lazima watafute namna tushughulikiwe.

Huku na huku wakina Bibi Kidawa Manzese wanakuambiwa CCM Mbele kwa Mbele. Hivi akina Bibi Kidawa wanajua viranja wa dunia wamepanga kitu gani?

Nipo kujiandaa na 2021

N.Mushi
 
Mada yako inaudhi.

Tanzania haiwezi kufanya mambo kuwapendeza hao unaowaita 'viranja'.

Tanzania na viongozi wake wanatakiwa kufanya mambo kuwapendeza waTanzania na kwa maslahi ya Tanzania yenyewe bila kujali hao 'viranja' wako wanataka nini.

Sasa ni kwa bahati mbaya sana inapotokea, kama ilivyo sasa, kwa viongozi wa Tanzania kufanya mambo yanayoudhi waTanzania na maslahi mazima ya waTanzania.
Hapo tu ndipo wanapotoa mwanya kwa hao 'viranja' kuja kuingilia mambo yanayotuhusu sisi; na kwa kiasi kikubwa yasiyokuwa kwa maslahi yetu.

Kwa hiyo, kama unalalamika, lalamikia hao viongozi wanaovuruga nchi yetu kwa visingizio mbalimbali, kama "kuleta maendeleo" kwa kuminya haki za raia na kuwanyima uhuru wa kuchagua wenyewe viongozi wanaowataka.

Sasa, kama unataka, waambie hao 'viranja' wako kwamba sisi hatutaki waje watuzidishie vurugu kama huko kwingine ulikokutaja. Hayo sisi hatuyataki. Kama wanayo nia ya kutusaidia, waje kwa mwaliko wetu watusaidie kuhakikisha kwamba raia wetu wanapata fursa ya kuchagua viongozi wao kwa kuwapigia kura bila ya kulazimishwa na yeyote, ikiwa ni pamoja na hao viranja. Wao waje tu hapa, kwa uwezo walio nao, watuhakikishie kwamba tutafanya uchaguzi wetu kwa haki, wazi na bila mizengwe.
Yeyote tutakayemchagua, huyo ndie atakayekuwa kiongozi tunayemtaka, na tusishurutishwe na mtu kufanya vinginevyo.

Tanzania ni yetu sote, na hatma yake ni yetu waTanzania. Hakuna taifa jingine lolote lenye haki na uwezo wa kuja kututawala tena.

Maana ya yote haya ni kwamba, ni wajibu wetu sasa kuhakikisha kuwa viongozi tunaowachagua wasijifanye wao ndio wajuaji zaidi yetu. Tunapowachagua kuongoza, wasigeuke na kutufanya sisi kuwa mateka wao kiasi cha kwamba hata kuwaondoa madarakani inakuwa shida.
 
Mkuu hatuwaogopi hao, tuna bahari mito na maziwa tutakula samaki na dagaa mwanzo mwisho, tutakula mihogo na kachumbari tu nyanya zipo zakumwaga tunalima wenyewe, Mananasi kiwangwa na geita yanatulisha nchi nzima, machungwa pale michungwani tutayala yapo kibwena tu, viazi pale uyole mbeya, mchele tunao kibwena, Gairo pale mahindi yapo kibwena, alizeti tunakamua wenyewe kifupi tutaacha kutumia hela tunakamua zetu butter trade mwanzo mwisho..

Na hawa mabeberu wakituwekea vikwazo, Serikali ituruhusu nasisi kufanya biashara za Magendo all over the world kuanzia bhangi, Cocain, mirungi majahazi yatakuwa busy balaa na mamafia wa deep sea wote watakuwa jamaa zetu kishenzi, Tunamruhusu North korea aje Kuchimba Uranium hapa na Mrussi, ule mwamba wa gas kule deep sea tunamkabidhi faster Yukos ya Urusi hata vitalu viwili na hiyo dhahabu wavimba macho wanaitaka kweli tunawapa wachimbe tu wakaweke stock kwao...
 
Hili tumelisemea sana wengine humu ndani, time without number, kwa sababu nchi hii haina kabisa ubavu wa kujihami dhidi ya mkakati wowote wa kuhujumu uchumi wake.

Serikali hii kwa muda mrefu sana imekuwa ikifumbiwa macho hasa linapokuja kwenye maswala ya uchaguzi kwani ccm hufanya kile inachoona inawapendezea tena "With flagrant impunity".

Mwaka 2015, kwa kiburi tu ccm kiliamua kufuta uchaguzi wa Zanzibar baada ya kushindwa na baada ya kuona hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yao sasa wanataka wageuze hiyo kuwa "Convention" kitu ambacho dunia ya wastaarabu wanaona hawawezi kuvumilia zaidi.

Sasa kitakachofuata huenda kikapelekea historia ya nchi hii kuandikwa upya na kuiweka ccm well on the receiving end. Let us wait and see.
 
kwa hio wataka "Regime change" kwa mafunaa ya mabepari na mafisadi?
 
Mada yako inaudhi.

Tanzania haiwezi kufanya mambo kuwapendeza hao unaowaita 'viranja'.

Tanzania na viongozi wake wanatakiwa kufanya mambo kuwapendeza waTanzania na kwa maslahi ya Tanzania yenyewe bila kujali hao 'viranja' wako wanataka nini.

Sasa ni kwa bahati mbaya sana inapotokea, kama ilivyo sasa, kwa viongozi wa Tanzania kufanya mambo yanayoudhi waTanzania na maslahi mazima ya waTanzania.
Hapo tu ndipo wanapotoa mwanya kwa hao 'viranja' kuja kuingilia mambo yanayotuhusu sisi; na kwa kiasi kikubwa yasiyokuwa kwa maslahi yetu.

Kwa hiyo, kama unalalamika, lalamikia hao viongozi wanaovuruga nchi yetu kwa visingizio mbalimbali, kama "kuleta maendeleo" kwa kuminya haki za raia na kuwanyima uhuru wa kuchagua wenyewe viongozi wanaowataka.

Sasa, kama unataka, waambie hao 'viranja' wako kwamba sisi hatutaki waje watuzidishie vurugu kama huko kwingine ulikokutaja. Hayo sisi hatuyataki. Kama wanayo nia ya kutusaidia, waje kwa mwaliko wetu watusaidie kuhakikisha kwamba raia wetu wanapata fursa ya kuchagua viongozi wao kwa kuwapigia kura bila ya kulazimishwa na yeyote, ikiwa ni pamoja na hao viranja. Wao waje tu hapa, kwa uwezo walio nao, watuhakikishie kwamba tutafanya uchaguzi wetu kwa haki, wazi na bila mizengwe.
Yeyote tutakayemchagua, huyo ndie atakayekuwa kiongozi tunayemtaka, na tusishurutishwe na mtu kufanya vinginevyo.

Tanzania ni yetu sote, na hatma yake ni yetu waTanzania. Hakuna taifa jingine lolote lenye haki na uwezo wa kuja kututawala tena.

Maana ya yote haya ni kwamba, ni wajibu wetu sasa kuhakikisha kuwa viongozi tunaowachagua wasijifanye wao ndio wajuaji zaidi yetu. Tunapowachagua kuongoza, wasigeuke na kutufanya sisi kuwa mateka wao kiasi cha kwamba hata kuwaondoa madarakani inakuwa shida.
Hivi MATAGA akili zenu zinakaa tumboni au?
Hivi ni mtanzania yupi anapendezwa na utawala wa kidhalimu wa Meko?

Wananchi wanauawa kama Ben Saanane, Azori Gwanda na Lwajabe (to mention a few), kutekwa kama ilivyotokea kwa Mo Dewji, Roma na Mdude Chadema na hata kubambikia watu kesi kama walivyobambikwa akina Eric Kabendera, Theo na Tito Magoti.

Ni bora hata hao mabeberu waingilie kati kutunusuru na udhalimu tunaofanyiwa na serikali ya huyu dikteta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usitutishe, regime change wasiitake Uganda huko waje ya Tanzania hata miaka mitano haijamaliza.
 
Mkuu hatuwaogopi hao, tuna bahari mito na maziwa tutakula samaki na dagaa mwanzo mwisho, tutakula mihogo na kachumbari tu nyanya zipo zakumwaga tunalima wenyewe, Mananasi kiwangwa na geita yanatulisha nchi nzima, machungwa pale michungwani tutayala yapo kibwena tu, viazi pale uyole mbeya, mchele tunao kibwena, Gairo pale mahindi yapo kibwena, alizeti tunakamua wenyewe kifupi tutaacha kutumia hela tunakamua zetu butter trade mwanzo mwisho..

Na hawa mabeberu wakituwekea vikwazo, Serikali ituruhusu nasisi kufanya biashara za Magendo all over the world kuanzia bhangi, Cocain, mirungi majahazi yatakuwa busy balaa na mamafia wa deep sea wote watakuwa jamaa zetu kishenzi, Tunamruhusu North korea aje Kuchimba Uranium hapa na Mrussi, ule mwamba wa gas kule deep sea tunamkabidhi faster Yukos ya Urusi hata vitalu viwili na hiyo dhahabu wavimba macho wanaitaka kweli tunawapa wachimbe tu wakaweke stock kwao...

Hizo nyanya zenyewe sasa hivi ni bidhaa adimu,Da! Vitu vingine havitaki ushabiki,sisi bado taifa changa sana ni kumuomba mungu tu,wazee wakiamua ni hatarii.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mada yako inaudhi.

Tanzania haiwezi kufanya mambo kuwapendeza hao unaowaita 'viranja'.

Tanzania na viongozi wake wanatakiwa kufanya mambo kuwapendeza waTanzania na kwa maslahi ya Tanzania yenyewe bila kujali hao 'viranja' wako wanataka nini.

Sasa ni kwa bahati mbaya sana inapotokea, kama ilivyo sasa, kwa viongozi wa Tanzania kufanya mambo yanayoudhi waTanzania na maslahi mazima ya waTanzania.
Hapo tu ndipo wanapotoa mwanya kwa hao 'viranja' kuja kuingilia mambo yanayotuhusu sisi; na kwa kiasi kikubwa yasiyokuwa kwa maslahi yetu.

Kwa hiyo, kama unalalamika, lalamikia hao viongozi wanaovuruga nchi yetu kwa visingizio mbalimbali, kama "kuleta maendeleo" kwa kuminya haki za raia na kuwanyima uhuru wa kuchagua wenyewe viongozi wanaowataka.

Sasa, kama unataka, waambie hao 'viranja' wako kwamba sisi hatutaki waje watuzidishie vurugu kama huko kwingine ulikokutaja. Hayo sisi hatuyataki. Kama wanayo nia ya kutusaidia, waje kwa mwaliko wetu watusaidie kuhakikisha kwamba raia wetu wanapata fursa ya kuchagua viongozi wao kwa kuwapigia kura bila ya kulazimishwa na yeyote, ikiwa ni pamoja na hao viranja. Wao waje tu hapa, kwa uwezo walio nao, watuhakikishie kwamba tutafanya uchaguzi wetu kwa haki, wazi na bila mizengwe.
Yeyote tutakayemchagua, huyo ndie atakayekuwa kiongozi tunayemtaka, na tusishurutishwe na mtu kufanya vinginevyo.

Tanzania ni yetu sote, na hatma yake ni yetu waTanzania. Hakuna taifa jingine lolote lenye haki na uwezo wa kuja kututawala tena.

Maana ya yote haya ni kwamba, ni wajibu wetu sasa kuhakikisha kuwa viongozi tunaowachagua wasijifanye wao ndio wajuaji zaidi yetu. Tunapowachagua kuongoza, wasigeuke na kutufanya sisi kuwa mateka wao kiasi cha kwamba hata kuwaondoa madarakani inakuwa shida.
None sense

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi MATAGA akili zenu zinakaa tumboni au?
Hivi ni mtanzania yupi anapendezwa na utawala wa kidhalimu wa Meko?

Wananchi wanauawa kama Ben Saanane, Azori Gwanda na Lwajabe (to mention a few), kutekwa kama ilivyotokea kwa Mo Dewji, Roma na Mdude Chadema na hata kubambikia watu kesi kama walivyobambikwa akina Eric Kabendera, Theo na Tito Magoti.

Ni bora hata hao mabeberu waingilie kati kutunusuru na udhalimu tunaofanyiwa na serikali ya huyu dikteta.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu 'Ben Bella'; nitakujibu kwa upole sana, kwa sababu naona unapata shida kweli kuelewa unachosoma.

Lakini kwanza nieleweshe tafadhali, "MATAGA" ndio akina nani? Pamoja na kunipa jina/cheo hicho, kwa bahati mbaya kwangu hakina maana yoyote kama sikijui!

Kiufupi mkuu wangu 'Ben Bella' ni hivi: Usitegemee kabisa na kufurahia kwamba kuna mtu yeyote toka nje atakayekuja kujufanyia kazi ambayo ni kazi yako wewe, na mimi, na waTanzania wote kwa ujumla wetu.

Hii ni kazi yetu, unataka ukawatafute watu wengine waje wakukomboe wewe, kwa sababu zipi?

Utaniambia huwezi kufanya kazi hiyo kwa vile huna jeshi na mabunduki ambayo waliowateka ndiyo wanayoyatumia kuwanyanyasa, kuwatishia, na wakati mwingine kuwaua kwa kuyatumia hayo mavyombo mliyowakabidhi wayafanyie kazi ya kulinda usalama wa nchi yetu, ..., badala yake wanayatumia kutulenga sisi.

Bila shaka swali unalouliza. tutawezaje sisi raia kukabiliana na haya masilaha bila ya kuwatumia hao 'vinara' wa dunia?

Mimi nakwambia hivi, kama upo kwenye siasa, weka kipaumbele chako kuwaelimisha wananchi. Wape elimu waelewe hatari inayotukabili. Sio lazima uitishe mikutano kuifanya kazi hiyo. Acha hicho kisingizio cha kunyimwa ruhusa ya mikutano.

Kazi zenu wanasiasa mnaolilia watu wa nje waje kuwafanyia kazi kirahisi ili nanyi mpate njia ya kwenda kuwakandamiza waTanzania, hilo lisahaulini. Lazima mtoke jasho, tuone kweli mnao uchungu na nchi yetu.

Njoni huku vijijini, 'mlango kwa mlango', 'jirani kwa jirani', 'klabu ya pombe kwa klabu ya pombe', mke/mme, n.k.; fanyeni kazi. Tuelezeni tujue nchi yetu inakoelekea.

Wakati mkiyafanya haya, 'of course' baadhi yenu mtakuwa mkishirikisha 'Jamii ya Kimataifa', hata hao 'wabae' wa dunia wajue mnahitaji msaada wao katika mambo kadhaa ambayo nyinyi hamna uwezo nayo - kama hayo ya mabunduki; wayazuie hayo mabunduki, na kuhakikisha maandaizi ya kupiga kura yatakuwa huru na haki kwa kila raia atakayeshiriki.

Sasa niambie, hapo shida ipo wapi? Unalilia watu waje wakukomboe, kumbe nyenzo za kujikomboa unazo mwenyewe?

Wanachi wa nchi hii ndio pekee wa kujiletea ukombozi. Wanahitaji tu uongozi utakaosimamia harakati hizo.
 
Back
Top Bottom