gidlameck
JF-Expert Member
- Jul 8, 2016
- 618
- 532
ile january tu mahusiano yalinichapa kisawasawa ,nikajaribu kulima mvua ikazidi mazao yakaenda na maji, mwezi wa 8 nilipata tuhuma kali ya kutembea na mke wa mtu yule mama hata sijawahi kumsemesha ila nilivyofuatilia kumbe kuna siku rafiki yangu alikuja ninakoishi kunicheki mda huo yule mama anapita mitaa hio jamaa akamwita karibu na home wakaanza kuongea nae aliewaona akatafisiri ni mm mwezi wa 10 uchumi ulinishambulia nikashindwa hata kumpeleka mtoto chuo hili limebaki kama kidonda mpaka sasa 12 hii sioni tumaini lolote mbele yangu kiufupi nimefanikiwa kuona wenzangu wakijenga wakifungua miradi hilo ndio nililofanikiwa mola nipe mwisho mwema. wakumbuke hata wale walioko mahospatalini wakiwa na shida ya afya wape tumaini jipya niwatakie mwisho mwema wa mwaka.