2020 Dr. Magufuli kusoma Urais

2020 Dr. Magufuli kusoma Urais

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
643
Reaction score
1,603
2020 MAGUFULI KUKOMA URAIS

"Rais Magufuli ni bingwa wa kuvuruga. Amevuruga demokrasia. Amevuruga haki za watu. Na sasa anavuruga kwa kasi uchumi wa nchi. Tunatuma salamu kwake. Mwaka 2020 will be certainly the end of Magufuli's presidency. Mwaka 2020 ndio mwisho wa Magufuli kuwa Rais wa Tanzania. Watanzania sio wajinga kiasi hicho. Watanzania wa sasa tuna akili, tumesoma na tuna uelewa. Hatutamuacha Ikulu mtu anayevuruga nchi"
......

Yeremia Kulwa Maganja,
Kaimu Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo.
Kijiji cha Makande,
Kata ya Lukumbule,
Wilaya ya Tunduru.
Tarehe 10 Novemba 2017.
 
Umeona alivyovurugwa Uganda? Ndio maana anaogopa maswali ya waandishi wa nje.....amezoea waandishi wa bahasha hawa wetu wanauliza direct....pale ameulizwa swali M7 akaona oohhhapa huyu kanjanja wa lugha amesikia neno la mwisho akarirudia takuwa shida.....akawa anamsaidia....amemsaidia sana....maana amevurugwa akakubali anabaka haki za binadamu
 
Kwa tume ipi? Acha kutupa matumaini hewa. Tena msipokuwa makini anaweza asitoke hata 2025. Huwezi kuwa jeuri namna hii ukatoka kizembe zembe. Kina M7 wanapenda sana kupumzika lakini atawaambia nini Dr. Besigye wakishika nchi
 
Unadhani mtu kuachia urais ni rahisi kama kwenda haja kubwa, Hakuna rais hapa nchini atakubali atawale awamu moja labda apende yeye.
 
Ila tuacheni utani bila tume huru ya uchaguzi CCM itatawala Nchi hii mpaka kiama
 
we mpuuzi pambana kwanza na viongozi wanaowakimbia ndo uoengelee habari za rais wetu kipenz cha wanyonge watanzania tunamuamini na tunampenda na tutamchagua
Kipenzi cha wanyonge gani au wale wa Kimara wanaolala nje waliobomolewa nyumba zao.
 
NILIKUWA NAONGEA NA AUNT YANGU MMOJA KWENYE CM ANASEMA HALI NGUMU. NIKAMWAMBIA VUMILIA, NI MIAKA MIWILI SASA! AKASTUKA AKASEMA KUMBE JPM ANA MIAKA MIWILI! ALIDHANI MINNE ETI.

HAHAHAHA JPM KAZA BABA WATU WAISOME NAMBA EFFECTIVE
 
Siasa ya Tz bado sana, wale wanaotaka Mhe raisi atoke mhula ujao wakimaanisha ameshindwa kuendesha nchi ukiwauliza wao wana mikakati gani ya kuendeleza nchi hakuna la maana, kazi yao ni kutafuta wapi mheshimiwa amekosea kusema basi ndio wanashikilia hapo hapo mwezi mzima, likipita wanasubiri akosee tena wapate pa kusemea.........cha ajabu kuna watu wana dhamana ya kuongoza majimbo yao, hakuna la maana wanalofanya kwa wananchi kimaendeleo ila wanataka wapewe nchi ili wafanye cha maana .....kwa kweli huwa siwaelewi kabisa.😕😕
 
Back
Top Bottom