2020 CHADEMA watapoteza viti vingi vya Ubunge, upinzani utanyong'onyea, wapigakura watakuwa wachache

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Nasikitika kusema hili. Upinzani hasa kwa chama kikuu cha upinzani CDM kitapoteza viti vya ubunge. Kwenye urais pia watapata asilimia za chini sana.

Pia mwaka 2020 kutakuwa na mwitikio hafifu wa kupiga kura ukilinganisha na mwaka 2015. Wananchi wamekata tamaa na upinzani utazidi kunyong'onyea huku CCM IKIIMARIKA.

Ni habari za kuogofya na za kutisha lakini nmeona niseme na leo tarehe 11/05/2017 iwekwe kumbukumbu hii. Ikiwa CDM watashinda nipigwe BAN YA MAISHA na pia nipo tayari kuhamishwa nchi nipelekwe kokote kule.

Nasisitiza. CDM imepoteza mwelekeo, haina mikakati,haina mipango imekata tamaa. CCM hujipanga wakati wote na kuungana kuupata ushindi kwa hali na mali.

Nchi hii itarudi zama za kale za kati.
 
utabili wa ccm

hii mkoa

arusha
mbeya

hata mlale kwa shetani hamuwezi pata
 
Hahaaa... eti wakuhamishe nchi ueende popote, unashindwa kuhamisha maisha yako na jamaa wanaokuzunguka yawe ya neema, unataka kwenda kuwa mizigo ya watu wengine.
 
Nasikitika kusema hili. Upinzani hasa kwa chama kikuu cha upinzani CDM kitapoteza viti vya ubunge. Kwenye urais pia watapata asilimia za chini sana.

Pia mwaka 2020 kutakuwa na mwitikio hafifu wa kupiga kura ukilinganisha na mwaka 2015. Wananchi wamekata tamaa na upinzani utazidi kunyong'onyea huku CCM IKIIMALIKA.

Ni habari za kuogofya na za kutisha lakini nmeona niseme na leo tarehe 11/05/2017 iwekwe kumbukumbu hii. Ikiwa CDM watashinda nipigwe BAN YA MAISHA na pia nipo tayari kuhamishwa nchi nipelekwe kokote kule.

Nasisitiza. CDM imepoteza mwelekeo, haina mikakati,haina mipango imekata tamaa. CCM hujipanga wakati wote na kuungana kuupata ushindi kwa hali na mali.

Nchi hii itarudi zama za kale za kati.

Unaota au utabiri?
 
Inapoteza vip uelekeo...weka maelezo ya kutosha...sio maneno...we juz tu tumepata wabunge wa east africa...kwa mara ya kwanza...unasema inapoteza...haha...
 
Sio kweli, mimi nilikuwa ccm nimehamia Chadema juzi tu, na watu wengi huku napoishi wanazidi kuhamia Chadema kila kunapokucha.
 
Sijui wewe na nape nani anaijua sana ccm.
Nape anaeona mbali amekwisha toa angalizo kwa ccm we unakuja na ngonjera zako.
Nauzuri umesema mwenyewe kuwa wananchi wengi wamekata tamaa, we unafikili wamekatishwa tamaa na ccm au chadema? Ccm ni mufulisi na itaporomoka zaidi 2020
 
Iwe fair election, tume huru, then uje utoe Mawazo yako hapa, Ccm bila police, tume yenu ya uchaguzi hata kile chama cha bwana Dovutwa kinachukua nchi saa mbili tu asubuhi
 
Back
Top Bottom