2020: CCM tumteue Mama Samia kugombea Urais

Habari za jioni wakuu..

Kama kichwa cha habari kinavyojionesha mimi naona hii miaka mitano imemtosha kabisa raisi wetu Mh.JOHN POMBE MAGUFULI na ningependa MAMA SAMIA SULUHU apokee kijiti cha kuongoza hili taifa.
Maana nimeangalia hali inayoenda nikaona tunahitaji IDEOLOGY mpya ya kuongoza hii nchi na mtu anayeweza kutuvusha ni MAMA SAMIA SULUHU.

Rais Magufuli amejitahidi kwa kiwango chake na inatosha hapa alipofikia..tunamshukuru kwa Uongozi wake.

Ni maoni yangu tu. Siku njema.

Mazee,

Unaelewa maana ya neno "ideology" ? Hususan katika muktadha wa uongozi wa nchi?
 
Nieleweshe..
1. Katika muktadha wa uongozi wa nchi, katika nchi inayoongozwa kidemokrasia kwa chaguzi za vyama vya siasa, "ideology" ni itikadi, ya chama, wote hawa wanafuata itikadi ya chama cha mapinduzi, kwa hiyo, kama unataka kubadili "ideology", badili chama, usibadili mtu. Maana ukibadili mtu, naye atafuata ideology ile ile ya chama.

2.Katika muktadha wa uongozi wa nchi, kwa kanuni ya "collective responsibility", watu wote walio katika serikali inayoongozwa na John Magufuli, wanakubaliana naye.Hivyo, ukimtoa Magufuli na kuaweka hao wengine, wakiendeleza habari za Magufuli, usishangae. Wangekuwa hawakubaliani na Magufuli, kanuni za "collective responsibility" zinawataka wajiuzulu nafasi zao

3. Huyo Mama unayesema afadhali yeye kuliko Magufuli, na yeye anajionesha u Magufuli wake kwa kauli zake kama hizi.
Hizi ni kauli za kijingajinga na ki Magufuli Magufuli, hata sielewi kwa nini unamuona huyu Mama ana afadhali yoyote.

PressReader.com - Journaux du Monde Entier

Samia: Waliohamishia biashara Zambia waendelee kukaa huko

  • Mtanzania
  • 25 Jul 2018
  • Na IBRAHIM YASSIN –TUNDUMA
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyabiashara wa Tanzania waliohamia upande wa mpaka wa wa Zambia uliopo Halmashauri ya Mji wa Tunduma, wilayani Momba mkoani Songwe, waendelee kukaa huko.
Samia aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwaka mjini Tunduma, baada ya Mbunge wa jimbo hilo, Frank Mwakajoka (Chadema) kueleza kuwa dhana ya utawala bora na maelewano kati ya wafanyabiashara na watumishi wa Serikali imetoweka.

Mwakajoka alisema mrundikano wa kodi na unyanyasaji kwa wafanyabiashara ni baadhi ya vikwazo vilivyowakimbiza wafanyabiashara katika masoko ya Tunduma upande wa Tanzania na kuhamia masoko ya Nakonde, Zambi. Akijibu hoja hizo, Samia alisema nchi inaendeshwa kwa sheria na taratibu hivyo haona tatizo kwa wafanyabiashara kuhamia Zambia kwa sababu maeneo mengi ya mipaka jambo hilo ni la kawaida.
Samia aliwataka wafanyabiashara waliohamia upande wa Zambia wabaki huko huko na nafasi zao zichukuliwe na wengine.
“Sioni tatizo wafanyabiashara kuhamia upande wa pili, waliopo ni wengi ambao pia wamekosa nafasi. Waliohama nawataka waendelee kuwa huko nafasi zao za kufanyabiashara huku zitachukuliwa na wengine wenye uzalendo na nchi yao,” alisema Samia.

Aidha, Samia alisema Serikali inakusudia kuondoa msongamano wa magari unaosababisha wafanyabiashara kuchelewa kuvusha mizigo yao katika mpaka huo.

Alisema kero hiyo itaondolewa baada ya kujengwa kwa bandari kavu na kuboresha usafiri wa Reli. Samia alisema Serikali imetenga Sh bilioni moja, kwa ajili ya kujenga eneo la maegesho ya magari katika eneo la Chapwa ili kupunguza msongamano wa magari katika mpaka huo unaokuwa kwa kasi na pia idadi ya watu ikiongezeka.
Alisema Serikali za Tanzania na Zambia zinashirikiana kujenga kituo cha pamoja kitakachopunguza usumbufu kwa wafanyabiashara kuvuka au kuvusha mizigo yao na pia tatizo la wafanyabiashara wanaobadilisha fedha katika mpaka huo linafanyiwa kazi.

Asilimia 75 ya mizigo inayotoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda nje ya nchi inapita kwenye mpaka wa Tunduma.
 
Nina sababu kuu za kwanini mama yetu Suluhu anafaa kumrithi Magufuli,
1. Ni zamu ya kina mama kupata kiongozi,
2. Zanzibar effect, ni miaka sasa hatuna rais wa JMT kutokea zZanzibar
3. Ni muislamu, japo haijaandikwa popote kwamba akitoka mkristo aje muislamu, lakin inapendeza tukipikezana hivo
4. Ana hekima na Busara, akiwa rais haki ya Mungu Tanzania tutakula maisha mema,
5. Hana kariba ya udikteta ,anawasikiliza wananchi, vema sana
6. Ni mpole n.a. mwadilifu, nadhani baada ya Mkali tupate mpole,
Nyerere mkali, Mwinyi Mpole, Mkapa mkali, Kikwete mpole, Magufuli mkali, Samia mpole

Britannica
 
Nyerere mkali, Mwinyi Mpole, Mkapa mkali, Kikwete mpole, Magufuli mkali, Samia mpol
Britannica

Rahisi kusema ila kutenda......?
 
Akitoka huyo mama (kama uliyoyasema yatatokea) bila shaka ndipo atafuata kijana wetu NIKKI WA PILI.
 
Nina sababu kuu za kwanini mama yetu Suluhu anafaa kumrithi Magufuli,
1. Ni zamu ya kina mama kupata kiongozi,
2. Zanzibar effect, ni miaka sasa hatuna rais wa JMT kutokea zZanzibar
3. Ni muislamu, japo haijaandikwa popote kwamba akitoka mkristo aje muislamu, lakin inapendeza tukipikezana hivo
4. Ana hekima na Busara, akiwa rais haki ya Mungu Tanzania tutakula maisha mema,
5. Hana kariba ya udikteta ,anawasikiliza wananchi, vema sana
6. Ni mpole n.a. mwadilifu, nadhani baada ya Mkali tupate mpole,
Nyerere mkali, Mwinyi Mpole, Mkapa mkali, Kikwete mpole, Magufuli mkali, Samia mpole

Britannica
N
 
Habari za jioni wakuu..

Kama kichwa cha habari kinavyojionesha mimi naona hii miaka mitano imemtosha kabisa raisi wetu Mh.JOHN POMBE MAGUFULI na ningependa MAMA SAMIA SULUHU apokee kijiti cha kuongoza hili taifa.
Maana nimeangalia hali inayoenda nikaona tunahitaji IDEOLOGY mpya ya kuongoza hii nchi na mtu anayeweza kutuvusha ni MAMA SAMIA SULUHU.

Rais Magufuli amejitahidi kwa kiwango chake na inatosha hapa alipofikia..tunamshukuru kwa Uongozi wake.

Ni maoni yangu tu. Siku njema.

Ni kweli ila sikupenda mbinu iliyotumika ya kumuingiza Samia Mdarakani kwa mapinduzi ya kimya kimya ndio maana hana nguvu ya kisiasa zaidi ya dola .
Matokeo yake mama hana raha kabisa na hatakija kupata raha maishani mwaka maana siku zinakuja ambapo kila kilichofanyika gizani kitawekwa kwenye mwanga mchana kweupe .
 
Yaan, Kuna comment za wadau humu nimezi soma zilikua mbele ya mudaa...
 
Nina sababu kuu za kwanini mama yetu Suluhu anafaa kumrithi Magufuli,
1. Ni zamu ya kina mama kupata kiongozi,
2. Zanzibar effect, ni miaka sasa hatuna rais wa JMT kutokea zZanzibar
3. Ni muislamu, japo haijaandikwa popote kwamba akitoka mkristo aje muislamu, lakin inapendeza tukipikezana hivo
4. Ana hekima na Busara, akiwa rais haki ya Mungu Tanzania tutakula maisha mema,
5. Hana kariba ya udikteta ,anawasikiliza wananchi, vema sana
6. Ni mpole n.a. mwadilifu, nadhani baada ya Mkali tupate mpole,
Nyerere mkali, Mwinyi Mpole, Mkapa mkali, Kikwete mpole, Magufuli mkali, Samia mpole

Britannica
Vipi bado unao huu mtazamo mpaka sasa?
 
Back
Top Bottom