2018 isikupite pasipo kufanya huu uwekezaji

2018 isikupite pasipo kufanya huu uwekezaji

Mkuu kama umepevuka fuatilia living forever, NLD, Flame nk..ilikuwa ni biashara hio hio ya nertwork marketing leo wako wapi vijana wengi waliingia kwa msisimko hakuna walichokipata zaidi ya kuishi kwa matumaini.

Shangazi yangu mimi ndiyo alikuwa coordinator wa living forever Tanzania alituhamasisha wachache waliongia hakuna hata mmoja aliyepata walichukuwa wanahubiri yeye mwenyewe mpka leo choka mbaya ndoto za utajiri alizokuwa nazo na kutuaminisha naona zimeyeyuka.

Mara nyingi watu wanaojiigiza kwenye hizi busness wanakuwa over ambitions kwelikweli eti kuna wati wametajirika huko uganda huwa hawasemi tanzania wanatoleaga mfano uganda wakijua hatuwezi fuatilia.

Mimi nawatia moyo jamani tuchape kazi nunua mzigo au hiduma uza direct sell hizi biashara za ujanja ujanja siyo nzuri.
Mkuu compasation plan ya AIM global ni tofauti na hizo za forever living. Ndio maana RRobert kiyosaki ameandika kwamba network markerting ni biashara nzuri ambayo ukiifanya unakuwa financially free lakini anasisitiza yafuatayo wakati wakuchagua kampuni ya kufanya nayo kazi
.*angalia compasation plan: Je kampuni inakuhitaji wewe tu ndo ulete watu. Je kuna spill over . mfano kwenye alliance kazi yako kubwa unayoifanya ni kuleta watu wawili tu kwenye biashara hao wawili wakileta bado utaendelea kulipwa hata kama walioko chini yako hujawaleta wewe
Halafu pia haikuitaji kuuza products na kurejesha faida kwenye kampuni
*angalia product je products ni muhimu kwa jamii products za alliance ni muhimu sana kwa jamii kwa upande wa afya
*angalia members waliomo je wamenufaika na kampuni: Pale nimekutolea mfano wa watu wa Uganda kwani kampuni imeanzia Uganda ndo ikaja Tz maana ndo kuna watu wengi ambao wameishatengeneza timu kubwa. Lakini kwa upande wa watanzania wapo watanzania kwa hiki kipindi cha miezi kumi na moja toka kampuni iingie nchini wengi wameweza kununua magari. Kila baada ya mwezi kwenye timu yangu lazima awepo mtu wa kununua gari
Mimi mwakani lazima ninunue yangu
 
Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wanajamii forum .
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha mwishoni mwa mwaka 2017.

Kama ilivyo kawaida ya wajasiriamali ni lazima ufanye tathimini juu ya miradi/bishara uliyoifanya katika kipindi chote cha mwaka mmoja pamoja na kuweka malengo ya mwaka mwingine mpya

Sasa katika kuweka mipango yako kama mjasiriamali Mimi ninakushauri usikose kuweka mpango wa kufanya uwekezaji katika kampuni ya AIM global.

AIM global ni kampuni inayojihusisha na kusambaza bidhaa zake kupitia mfumo wa biashara ya mtandao.
Kwa wale ambao wameisha soma vitabu vya ujasiriamali kama cha The business of 21st century, the cashflow quadrant n.k wanaelewa kwa sababu kwanini ufanye biashara ya mtandao na si vinginevyo.
Yapo makampuni mengi yanayofanya biashara ya mtandao lakini zifuatazo baadhi ya sababu kwamba kwanini ufanye networking pamoja na AIM global:-

1.Nguvu ya watu wawili:-kama ilivyokawaida katika biashara ya mtandao ni kuwaleta watu katika biashara. Sasa katika kampuni ya AIM global utahitaji kuleta watu wawili tu na kuweza kutengeneza timu kubwa ya watu walioko chini yako watakao kuwa wanakufanyia kazi.
Pengine ikitokea hujapata mtu wa kumuingiza kwenye biashara
Mtu aliyeko juu yako anakuwekea

2.Mfumo wa ulipaji kwa siku(milioni 1au 3au 7/siku):-
Kampuni imeweka mfumo mzuri wa kuwalipa wawekezaji wake
Ambapo kwa siku unalipwa pair 16 kwa kila akaunti na kila pair sh 690000 kwa hiyo kwa akaunti moja ni (Tsh 690000X16=Tsh1104000/siku)
Kwa hiyo mtu mwenye akaunti 2=Tsh2mill, 3=3mil, ...na 7=7mil/siku na mtu unaruhusiwa kujiunga kwenye biashara kwa akaunti moja mpaka saba kulingana na uwezo wako

3. Kuuza bidhaa sio lazima:-
Ukinunua package kwa ajili ya kujiunga kwenye biashara haikuhitaji kurudisha kiwango cha pesa. Ukitaka kuuza fedha itakuwa ni ya kwako. Unanunua package kwa 560000 unaweza ukaiuza kwa laki 7.5, ukarejesha hela yako. Lakini kama wewe huna muda wa kuuza unaweza ukatumia hizo bidhaa kwa ajili ya kutibu na kujilinda na magonjwa kama vile kansa, vidonda vya tumbo, kupunguza mafuta mabaya mwilini, matatizo ya figo, kupunguza speed ya uzee, kuongeza kinga ya mwili n.k
Note: mtu yeyote hata kama siyo mgonjwa anatumia bidhaa kwani ni food supliment

4Hakuna viwango vya mwezi unavyotakiwa kuwa navyo ili akaunti yako iendelee kuwa active

5.Hakuna kufufua akaunti(no renewal) :- Ukishajiunga kwenye biashara haikuhitaji kurudia tena kufufua akaunti hata kama umemaliza muda mrefu hujafanya biashara

6.Unaruhusiwa kuanza biashara kwa akaunti zaidi ya moja:- Mtu unaruhusiwa kujiunga na biashara kwa akaunti kuanzia moja mpaka saba kulingana na uwezo wako

MWISHO: nawakaribisha kwenye hii biashara mtu yeyote anaweza kuifanya hata kama ni mfanyakazi kwani haitaji muda sana ni rahisi kufanya part time.
Kampuni imeingia hapa nchini mwaka huu lakini imebadilisha watu wengi kiuchum wapo wengi walionunua magari, viwanja na vitu vingine vya thamani
Kwa ambaye yuko interested unaweza ukanitext whatsapp kwa no. 0757409103 nitakufafanulia zaidi pia nitakudirect kwenye kituo cha semina kulingana na mkoa uliomo
Kwa hapa mjini ukishaona maelezo marefu kuhusiana na kujipatia kipato jua hakuna jingine zaidi ya ulugumi.

Hakuna pesa inapatikana kwa mserereko kihivi Kaka.
Wadanganye wakuwadanganya.
 
Kwani Mimi nimeandika kampuni ya forever au nimeandika AIM global . kila kampuni ina compasation plan yake na ndio maana AIM global the best direct selling company kila mwaka kutokana na compasation plan take nzuri
Mi ningekushauri uchukue ndugu zako na washikaji wako wote afu wambie mtengeneze timu mpige pesa kimya kimya.

Otherwise uniambie Unapaka kuwaingiza watu chaka maana kukaza kwa vyuma naona akina lugumi mnawewesea.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]


Gusa Unase , Naona unataka kutufungulia mwaka na maumivu
 
Mkuu compasation plan ya AIM global ni tofauti na hizo za forever living. Ndio maana RRobert kiyosaki ameandika kwamba network markerting ni biashara nzuri ambayo ukiifanya unakuwa financially free lakini anasisitiza yafuatayo wakati wakuchagua kampuni ya kufanya nayo kazi
.*angalia compasation plan: Je kampuni inakuhitaji wewe tu ndo ulete watu. Je kuna spill over . mfano kwenye alliance kazi yako kubwa unayoifanya ni kuleta watu wawili tu kwenye biashara hao wawili wakileta bado utaendelea kulipwa hata kama walioko chini yako hujawaleta wewe
Halafu pia haikuitaji kuuza products na kurejesha faida kwenye kampuni
*angalia product je products ni muhimu kwa jamii products za alliance ni muhimu sana kwa jamii kwa upande wa afya
*angalia members waliomo je wamenufaika na kampuni: Pale nimekutolea mfano wa watu wa Uganda kwani kampuni imeanzia Uganda ndo ikaja Tz maana ndo kuna watu wengi ambao wameishatengeneza timu kubwa. Lakini kwa upande wa watanzania wapo watanzania kwa hiki kipindi cha miezi kumi na moja toka kampuni iingie nchini wengi wameweza kununua magari. Kila baada ya mwezi kwenye timu yangu lazima awepo mtu wa kununua gari
Mimi mwakani lazima ninunue yangu
 
Networking business hiyo ni sawa na GNLD, FRAME na wale wengine wengine hiyo lakini tano nenda kariakoo tafuta mzigo peleka malinyi kafanye biashara acha na huu ujanja ujanja hauna mwisho mzuri
Mzigo gani kwa mfano
 
Hakika nimegundua kitu kupitia hii thread kuhusu mitazamo ya watu mbalimbali.
Kuhusiana na fursa mbalimbali kama fursa .

Watu wengi wanapenda kufanya conclusion hata kwa kitu wasichokijua. Hawataki kujifunza
Ushauri wangu ni kwamba kabla haujaji fanya uchunguzi
Kabla haujaanza kufanya biashara soma vitabu. Fanya uchunguzi wa kina kwanza ndo uanze, Tafuta ushauri kwa waliofanikiwa katika hiyo biashara.
Utashangaa mtu anaenda kuomba ushauri kwa mtu aliyefail kwenye biashara Fulani. Kamwe hawezi kukupa mbinu atakuambia hailipi.
Hawezi ukaomba ushauri wa jinsi ya kuweza kufaulu kuingia advance kwa mtu aliyefail kamwe atakushauri vibaya
Ukitaka kuomba ushauri omba ushauri kwa mtu aliyefanikiwa
Wapo watu wengi wamefanikiwa katika networking tena katika hizo forever living zenye compasation plan tofauti na ya alliance lakini unakuta mtu anajoin kwenye business ushauri anaomba kwa aliyefail. automatically nawe utafail.
Kampuni inatoa training jinsi ya kufanya biashara mtu haendi training
Kwa hii mitazamo hali ngumu ya maisha itaendelea na kwa waliotiyari kubadilika na kujifunza na kubadirika watafurahia maisha
 
Omuziba hebu tufanye kazi mkuu, achana na hizi mambo. Kirahisi kabisa mtu apate milioni 7 kwa siku? Nawe unayabeba kama yalivyo unayaleta tu humu, hebu tushauriane vitu vya uhalisia jamani tuachane na maigizo haya muda wake ulishapita. Kama hamkuvuna kipindi cha zamani potezea tu mkuu
sure
 
Ovyo kabisa! Sasa ukikutana na huyu aliyeandika utamuonea huruma!

Namba kuzitaja ni rahisi sana, na uongo wa kutisha kabisa.

Hivi mtu mwenye akili timamu uchukue pesa yako na kuingiza kwenye vitu vya kipuuzi ukitarajia kuvuna mamilioni!
 
Kaka siku nyingine fursa kama hizi usilete jf, huku Kuna wajuaji zaidi ya unavyofikiria
 
Mpk upate timu leo? Watu washafumbuka macho kitambo kama na ww unatafuta team ishakuwa ngumu mkuu kajaribu fb
 
Acha niendelee na biashara yangu si kuibiwa wakati naona
571a22f939cf539c65739f7df0b75da1.jpg
b8f0fb7a45bb3a829b7e08473f6b4815.jpg
 
Ukitaka kuendelea na Umaskini mwaka 2018 jiunge na biashara ya mtandao ya kitapeli kama hii.Utaishia kuzunguka na bidhaa kama mmachinga na laki tano yako ulionunulia bidhaa ni afadhali ungefugia hata kuku
 
Back
Top Bottom