2017 Released and upcoming movies

Dodou

JF-Expert Member
May 4, 2017
494
390
Spider man: Homecoming
>>>> Baada ya matukio ya kwenye Captain America: Civil War, Peter Parker anajaribu kubalance maisha yake ya shule kama mtu wa kawaida na maisha yake ya kupambana na viumbe waharibifu akiwa kama spiderman
Release date: July 7- US
Starring: Tom Holland, Zendaya, ........

The Pirrates of the Caribbean: Dead men tell no tales
>>>>
Katika safari yake ya baharini akitafuta silaha yenye miujiza ya kutuliza na kuondoa majanga yote baharini (the trident) - Captain Jack Sparrow, anatafutwa na anafuatwa na Captain Salazar, mfu hai ambae anataka kumuangamiza kwa kuwa yeye ndie aliesababisha afe na kulaaniwa kuwa mfu hai
Release date: May 26
Starring: Johnny Depp, Javie Bardem, ...........

Transformers:The last knight
>>>> Vita kati ya Transformers na binadamu inaibuka kipindi ambacho Protector na peace maker Optimus Prime(car robot) hayupo,kuwaangamiza transformers,Cade Yeager anatakiwa kuungana na Bumblebee(car robot) na professor wa oxford kutafuta siri za zamani na historia iliyofichika ya kuwepo kwa transformers duniani
Release date: June 21
Starring: Mark Wahlberg, Isabela Moner, ........

Wonder Woman
>>>>
Kabla ya kuwa wonder woman alikuwa ni Diana princess of the Amazons aliefundishwa mafunzo maalumu na ya hali ya juu ya vita mpaka alipokutana na Rubani wa ndege na kumwelezea juu ya mapigano yanayoendelea huko nje, nje ya Dunia yake, Diana anashawishika kuwa anaweza kukomesha mapigano hayo, anaondoka nyumbani kwa mara ya kwanza, anapigana vita sambamba na wanaume ili kukomesha vita zote, hatimaye anagundua nguvu zake zote alizonazo na wito wake katika maisha yake
Release: June 2
Starring: Gal Gadot, Chris Pine, .........

Justice League
>>>>
Baada ya matukio ya kwenye Batman v Superman na kuwa inspired na superman kwa kitendo chake cha kujitolea, Bruce Wayne- Batman anashirikiana na Wonder woman kutengeneza Team ya superhumans ikiundwa na Aquaman, Cyborg na Flash ili kuweza kupambana na adui aliejitokeza- Steppenwolf na jeshi lake
Release date: November 17
Starring: Ben Affleck, Gal Gadot, Henry Cavill, .....

xXx: Return of Xander Cage

>>>>
Baada ya Xiang na team yake kufanikiwa kuingia office za CIA NYC na kuiba kifaa kinachoweza kucontroll satellites na kuzifanya zi crash sehemu yoyote ile iliyolengwa, CIA agent Jane Marke anamvizia Xander Cage mwendesha operesheni ya xXx hapo zamani ambae alifake kuwa amekufa ili aishi maisha yake, Jane Marke anamshawishi Xander kurudi kwenye opereshen ili kurudisha kifaa kilichoibiwa kijulikanacho kama Pandora's box. Xander anaikata special forces operative unit aliyopewa ikiongozwa na Donovan na kuamua kuunda team yake mwenyewe na kufanikiwa kumpata Xiang nchini ufilipino ambae anakubali kuwa analo box hilo na kusema kuwa team yake pia ni part ya xXx ambayo iliajiriwa na NSA agent Gibbons aliekufa kwa satellite crash nchini Brazil akiwa na recruit wake mcheza mpira Neymar Jr ambapo walikuwa katika operesheni xXx. Xian anamwambia Xander kuwa wameiba box hilo ili kuzuia matumizi yake mabaya huku mmoja wa team yake akiamini kuwa ni lazima waliangamize box hilo, baada ya kuangamiza box hilo, agent Jane Marke anagundua kuwa halikuwa box lenyewe kutokana na kutokea kwa satellite crash nyingine nchini Urusi na kisha Xander anagundua kuwa box lenyewe lipo mikononi mwa director wa CIA aitwae Anderson, Xander Cage na Xiang wanakimbia na kupigana kuwahi kufika kwa CIA director Anderson na kisha wanaamua kulindana dhidi ya Anderson na watu wake
baada ya Xander Cage kumshutumu- director Anderson anakili kuwa yeye ndie aliesababisha satellite crash iliyomuua Gibbons, Anderson anauawa na Xander's teammate na Xiang anakamatwa na CIA. Xander anachukua box analirudisha mikononi mwa Jane Marke, Jane Marke anatangaza kuwa operesheni ya xXx imefungwa kisha anampiga risasi Xander Cage ili aweze kubaki na siri na box hilo na pia anatuma kundi la wauaji ili waweze kuwaua teammates wengine waliosalia ambao wanapigana kwa msaada wa xXx operative wa zamani- Darius.
Xander Cage anapona kutokana na bullet proof aliyokuwa ameivaa,anaungana na Xiang kupigana na Donovan na watu wake pamoja na Jane Marke ,Jane Marke anatuma satellite ili iweze kucrash mahali ambapo teammates wengine wanapigana. Xiang anafanikiwa kumuua Jane Marke na kuchukua box japo anashindwa kuizuia satellite kutokuanguka, Xander akiwa ndani ya ndege anaziba njia ya satellite ambayo inagonga ndege huku yeye akiruka kutoka ndani ya ndege hiyo na kufanikiwa kupona. Xiang anampatia Xander box device ambalo Xander anaamua kuliangamiza na kisha kwenda kwenye mazishi ya Gibbons, Gibbons anamfuata Xander na kujulikana kuwa alifake kifo chake ili kuitengeneza upya program ya xXx ya kwake mwenyewe akianza na Neymar Jr kama recruit wake mpya, Gibbons anampongeza Xander kwa kufanya vizuri na Xander anaamua kuendelea katika kazi na kuwa yupo tayari kwa mission nyingine.

Released date: Jan 20
Starrings: Vin Diesel, Deepika Padukone, Nina Dobrev, ..........

Ntaendelea na zingine
 
Back
Top Bottom