2016 Masihi alipoyakanyaga kwa Dkt. Mashairi ya Chekacheka

Jul 3, 2022
47
81
Do not outshine your master!Naam kamwe ''usimzidi Bwana wako."

Katika nchi za watu weusi kama mkaa,rangi ya majabali yaliyoijenga Ulaya na Amerika yote wakiwaacha wato to, wazee na viwete katika bara la giza, Kuna aina yao ya uongozi.

Naam kila ukikaribia wasaa wa kuachia kiti cha enzi vimbwanga huanza!Masihi anaeondoka huanza kujiongezea urefu wa kimo chake kwa mkono.

1.Atahakikisha MANENO MACHACHE NGUMI NYINGI wapo upande wake.

2.Kitabu chenye nguvu japo hakisemi Wala hakisikii ila wino uliomo ndani yake hueshimiwa,kinaongezewa kurasa kadhaa au kinarekebishwa baadhi ya Aya ili mradi tu kiendane na matakwa ya Masihi mlafi!

3.Jeneza la serikali hukaa mkao wa kuwafunika wenye midomo ya moto!Ukileta falsafa za Abraham Lincoln ardhi inakumeza.

Lakini huu utaratibu haupo katika nchi ya BLACK AFRICAN.Hapa Masihi wake hukiheshimu sana KITABU!Muda wa kuachia kiti cha enzi na kwenda kulea wajukuu hua wanaondoka kistaarabu tu lakini huacha vinyago vyao.

Mwaka Fulani, LODILOFA aliekua akienda kulea wajukuu alishindwa kuacha kinyago chake kwa sababu kuna watu ndani ya chama chake waliojipa umuhimu walimzidi kete wakati wa mchakato wa kumtafuta mwakilishi wa chama katika uchaguzi,Watu hawa waliongozwa na Godfather kutoka mitaa ya Wala mikate kwa tikiti kama brekifasti yao.
Mitaa ambayo mtoto wa miaka 9 anavaa kiatu namba 50 na shati la mtu mzima!Mitaa ambayo Kuna msanii wake anashindana na ex wake kula bata!Hii nchi bhana.

LODILOFA akachagua kua mpole na kuwaacha Godfather na genge lake watwae kiti cha enzi huku nyuma akijipanga!Uchaguzi ukaja Mashairi ya chekacheka akaingia kitini mwa enzi baada ya kukitafuta kwa kivumbi na jasho tangu miaka ya 1990s, walalahoi na wavuja jasho waka-enjoy maisha, huyu Mashairi ya chekacheka alikua na tabia za ukipata kula na wanao maana mitaa imekulea kwa hiyo watu walikula na kusaza, vyombo vya hatari vikambatiza majina kama yote ilihali hakua mtu wa Nazareth.

Wakati wake wa kwenda kulea wajukuu ulipowadia nae alitaka kuweka kinyago chake akadunda!Naam LODILOFA alitakakuweka heshima na yeye! Mashairi ya chekacheka akaridhia kinyonge sana kukubaliana na LODILOFA kumpa kiti MASIHI.

Do not outshine your master!

Hiyo ndio Sheria ya kupata nguvu lakini MASIHI alikua mapuuza na akapuuza!Naam akapewa kiti cha enzi na kuapa kukulinda kitabu.

Kuna mambo matatu Si walalahoi Wala Wainjilisti na vyombo vya hatari hawakuyajua kabisa!Wakashindwa kukaa KITAALAMU.Likawa ni kosa kubwa kwao!

1.Midomo ya moto marufuku!
2.Nyimbo za kristo na Tenzi za rohoni ni lazima ili ulambe maokoto.
3. Yeye akienda kushoto wewe marufuku kwenda kulia.

Haya mambo matatu yalileta maafa sana pale BLACK AFRICAN!Ilifika wakati habari za Wainjilisti hazikupatikana kirahisi ni kwa sababu Wainjilisti walikataa kuinba Tenzi za rohoni na nyimbo za kristo.Mashairi ya chekacheka alikua na tabia ya kumpa maujiko MASIHI kiasi alisikika akisema ''.......nimewaletea chuma!"

Unajua Kuna baadhi ya nafasi pale BLACK AFRICAN ni tamu balaa!Ukipata unaweza msahau mkeo.MASIHI alipoipata tu sijui kitu gani kikampeleka kwa Mganga wa Bahinza!?Akarudi na fikra za kujirefushia kimo chake kwa mkono?Fikra za Kuamini Wainjilisti wote mahali pao ni Jeneza la serikali.

Bahati mbaya sana hakua smati katika hii sekta ya ulafi, yeye alikua anakulakula TU!Mganga wa Bahinza aliua na yake!MASIHI alikua hajui Mashairi ya chekacheka na Mganga wake walitibuana nyongo kisa maokoto ya misituni.Naam walikua wanatafutana balaa kushikana uchawi.Masihi hakuyajua hayo sababu alikua Hana ABC za kikachero Kuhusu wapwa hawa katika ulimwengu wa umbea.

Masihi ukiachilia mbali ukipanga wake wa kuongoza wanafunzi wenzake alipokua chuo kikuu cha digrii za mezani, alinyimwa uwezo wa kuwaongoza wenye macho matatu na milango sita ya fahamu wakiongozwa na Mashairi ya chekacheka.

Genesis....
Alipoapa kwa kitabu kilichopigwa kiberiti pale ufaransa na kunyang'anya roho za watu zaidi ya 50M na kilichopitia giza la kiroho lililoisha mwaka 1798,Akawasha matoyota yake pyeeeee!!tiriruriru!!... wiuwiuwiu!! hadi Bahinza kushikana mikono na Mganga ili kupata Siri ya kuusaka utajiri wa kufanya kazi za ukombozi until his soul last in everlasting peace.

Kuna saying zinadai ana damu ya huko!

Alipewa masharti mpaka yakashindwa kubebeka!

Machache na ya msingi ni haya!Manne TU.
1.Jibatize nickname ya kuwaunganisha walalahoi na wavuja jasho ili kila ukipita wakuone umetoka Nazareth.Hii itasaidia wakupende.

2.Wainjilisti marufuku kuingia kanisani tena !
3.Huduma zote za kanisani zifanywe na mashemasi wa imani Moja
4.Mchungaji lazima ajue kudili na mapepo ya makuhani.
5.Mtunzaji, mkusanyaji na mpitiaji wa sadaka za walalahoi kanisani lazima umpe mwanao ili akukatie zaka na sadaka.
6.Hakikisha farisayo ni mwanao ili Wainjilisti waisone namba wakileta midomo ya moto kua kufuati kitabu.

Ukimaliza hayo we fungua KITABU badili aya na kuongeza kurasa then kula maisha!Somo lilikolea Masihi akarudi Black African kutekeleza.

Kwanza akaanza na gia ya kushindwa mapema TU!Alipogombana na MANENO MACHACHE NGUMI NYINGI katika lile tukio la Sept 11.Akafuta imani nao akajenga uswahiba na wavaa SUTI likawa kosa baya sana kimkakati.Akaanza kuwabatiza wanjilisti na washikakamera wanoko!

Mara flani kayeyuka kama barafu, mara huyu kabinywa kengele, sijui yule katobolewa na baruti yaani kazi ya ukombozi, ubatizo na utakaso wa maji mengi ilitukuka sana BLACK AFRICAN.Baada ya kutibuana na MANENO MACHACHE NGUMI NYINGI akaenda mpaka kwa Mashairi ya chekacheka akimnanga na kumpigia vijembe vingi huku akipita na interest zake Moja baada ya nyingine kiasi kwamba Mashairi ya chekacheka akaanza kusumbuliwa na mapepo ya kuurudia ukabwela!

Masihi alikua anapiga injili kwa vitendo kuliko MANENO, Akisikika anaenda kwenye ukaguzi wa wajenzi mkandarasi tumbo joto likipungua tofali au zege kazi anayo!Waumini wakampenda kutoka moyoni na wengine wakampenda kinafki TU ilimrafi wapate maokoto ila Mashairi ya chekacheka alikua anamsonea tu ramani.

Siku ya siku ikaja.....

Mganga alikua na kumbukumbu mbaya sana kumhusu Mashairi ya chekacheka, aliwahi pelekewa suti moja hadi kilingeni kwake maana alikua na tabia za kulala nje ya jumba jeupe yasije mkuta ya mwenzake kushushwa toka angani.Na alikua anajua how smart Mashairi ya chekacheka alivyo, japo na yeye si mtu wa kucheza nae ukimuachia ghetto unakuta dekio tu! Alishawatumia watu radi za kiangazi hadi ughaibuni wakarudi mavumbini na kule misituni alitumia misukule yake kulamba maokoto.

Lakini hakumtonya mteja wake kua Mashairi ya chekacheka ni kisiki cha mpingo, akamuacha aking'oe peke'ake.Naam Mganga na mgangwaji Masihi wakachora ramani ya kumrudisha mavumbini Mashairi ya chekacheka.

What a map!?

Mashairi ya chekacheka alionekana ni nzi kwenye togwa za Hawa maswahiba na dawa yake ni Moja TU arudi mavumbini anadhambi nyingi mno.Walijipa kazi ya muumba, vijana wakatoka Bahinza hadi Bandari salama wakapewa hekalu la kufanyia rehearsal za kumuombea muumini aliekata mitaa ya uzimani na kutokomea mautini huku wakitumia darubini kumsomea ramani ya maangamizi Mashairi ya chekacheka.

Mashairi ya chekacheka ni mtu wa kuchukuliwa poa na Waso mjua lakini undava alionao omba usikutane nao.Siku hii akarudi ghetto kutoka shambani vijana kutoka magari wakaingia mzigoni .

Kumbe wasijue Mkata keki na bosi wa MANENO MACHACHE NGUMI NYINGI alimpa mashairi ya chekacheka Kijana makini mikono mia anatupa NGUMI kama cherehani , miguu inachomoka zaidi ya Usain Bolt na alikua anakula lindo kitambo maana taarifa za kuwindwa alikua nazo.

Vijana walipoingia wakakutana nae weeeee!!Kulikua hakuna hadithi marambili za kichwa wakapokonywa uhai katika ardhi ya ugenini maiti zao zikarudishwa nyumbani na ujumbe mmoja TU!

''.....Nawachora tu na mlichokianzisha mjue kukimaliza mnacheza sindimba hakikisheni nikiwawekea mdundiko hampoteani...."

Jaribio la MASIHI kumrudisha mavumbini Mashairi ya chekacheka akisaidiana na Mganga kufeli likapanda mbegu ya uasherati wa kupokonyana pumzi BLACK AFRICAN.

TANZIA likawa neno la kuzoeleka kama salamu....,...........

Watu walianza kupukutishwa!

One by one lawama akatupiwa namba 19, kumbe bhana

Do not outshine your master!!

MASIHI aka gone to glory, akawaacha walalahoi, makuhani na wachungaji na hasira za mkizi!Mtu wao wanamjua lakini haingiliki kizembe nafsi zao wanazitaka wasijepotea kibwege.

Tatizo lao Masihi aliwazoesha kula samaki badala ya kuvua wanapata tabu kweli

......................................…..............…........…..

There is story in every thing
 
Umeulizwa?
Mwache asaidie kufungua Code maana mpaka hapa mwandish alikuwa na kusudi kutueleimisha kilichotokea ila hatujui hata yy amecopy au anaufaham na kilichotokea hivyo sio tena confidential kwa hiyo anavyochambua anasaidia sana na watu kama hawa ndo muhimu
 
Hakuna jipya. Hukuweza leta jambo lenye tija na hata nick names ulizotoa ni za kitoto tu. Ulipaswa umwambie aliyekusimulia aje asimulie vizuri but alete kitu ambacho hatukifahamu.
 
Kumbe kuna timu ilitoka kwa PAKA kuja kumdedisha baba ake TWO-RIZI!
 
Hakuna jipya. Hukuweza leta jambo lenye tija na hata nick names ulizotoa ni za kitoto tu. Ulipaswa umwambie aliyekusimulia aje asimulie vizuri but alete kitu ambacho hatukifahamu.
Uzuri umesoma ndio umegundua sio kitu kipya na aliekusimulia na ulikosoma nakujua.
 
Hakuna jipya. Hukuweza leta jambo lenye tija na hata nick names ulizotoa ni za kitoto tu. Ulipaswa umwambie aliyekusimulia aje asimulie vizuri but alete kitu ambacho hatukifahamu.
Umaskini ni laana ila uafrika +Umaskini..
Hakuna jipya..
Nickname za kitoto..
Ulipaswa...
Una shida flani la ki-hormone
 
Back
Top Bottom