TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,622
- 28,697
.......
Hapo kuna hoja zifuatazo. Je, umejadiliwa katika mukatadha wa kimuungano?
Je, kura za mswada kuamua kuhusu mafuta na gesi zimefikiwa kwa kuzingantia 2/3 ya pande husika?
Maswali zaidi, je, iwapo Zanzibar imeondoa katika muungano, wale wabunge wa Zanzibar katika JMT wanajadili nini?
Maana si suala la muungano kwa mujibu wao. Mijadala yao ni sawa na kuita Wakenya wajadili. Ndivyo livyo sasa
Pamoja na hayo, naibu waziri Nchemba ametangaza kuwepo kwa account mbili chini ya BoT.
Tunafahamu BoT ni ya muungano. Sasa account za kupokea mapato na account za kutunza mapato ni za sehemu gani ya muungano?
Je, account hizo zitahusu gesi na mafuta yatakayopataikana Zanzibar?
Kama jibu ni hapana , ni kwanini rasilimali za upande mmoja (Tanganyika) ndizo zichangie JMT?......
Yes hapa kuna tatizo. Hizo ni bodi za Tanzania na hivyo wazanzibar watahitaji ajira tu kwasababu ni shughuli za muungano.Nimepitia ile sheria ya mafuta (Petroleum Act, 2015) kwa haraka, inasomeka hivi kwenye ukurasa wa 29 wa pdf iliyowekwa jamvini na JF.
Establishment of the Board of PURA (Petroleum Upstream RegulatoryAuthority):-
18.-(1) There shall be the Board of PURA to oversee the operation of PURA.
(2) The Board shall consist of five members who are citizens of Tanzania of moral character, proven integrity
and professional competence.
--------------------
Hao wajumbe watano watatoka Tanganyika (Tanzania Bara) ama Zanziber (Tanzania Visiwani) ama watatoka pande zote mbili.?
Kiukweli, kizungumkuti cha katiba ya Zanzibar kilitakiwa kuwekwa sawa, ili mambo haya yapatiwe ufumbuzi kwa wepesi zaidi. Na uharaka huu ndiyo unaozidisha mashaka, juu ya nia ya wale wanaoharakisha masuala haya. Kuna jambo haliko sawa!!!
Yes hapa kuna tatizo. Hizo ni bodi za Tanzania na hivyo wazanzibar watahitaji ajira tu kwasababu ni shughuli za muungano.
Hivyo nafasi za Watanganyika kusimamia rasilimali zao zitageuzwa kua ajira za kisiasa kwa wznz na kupoteza maana nzima.
Kumbuka huko znz hakuna Mtanganyika katika bodi yao.
Anyways, haya ni mambo yanayotakiwa yaangaliwe kwa kina si kukimbiza mswada kibusa bubusa tu
Na hili walitakiwa walione wabunge wa CCM. Inashngaza sana hawaoni haya
Hoja kubwa hapa ni kuwa uchaguzi wa mwaka huu wananchi waamke.
Wanaona jinsi nchi inavyouzwa watu wakipiga makofi. CCM wametufikisha mahali hata vitu vidogo kama hivyo hawawezi kufikiri
Kama wananchi hawaoni haja ya mabadiliko, wawe tayari kuishi na maumivu kwa muda mrefu nchi ikiuzwa na wao wakiwa ni bidhaa
Bongolander , tunadanyika kirahisi.
Siku zote husema,Watanzania ni watu wa ajabu kidogo, ni wazuri wa kulalama na wepesi sana wakusahau
Tunajua kila uchaguzi huambatana na mambo ‘maovu'
Siku za nyuma tumeona ya Kagoda n.k. bado hatuamshi vichwana kujiuliza, hii miswad inayokimbizwa bungeni kukiwa hakuna wabunge si wapinzani tu hata wa CCM ina heri na taifa hili.
Na iweje miaka 10 miswada hiyo ilikuwa chini ya kapeti na sasa inaibuliwa kwa hati za dharura
Huu wa gesi na mafuta una usiri tusioujua. Hili lilikuwa jambo la kitaifa,kwaninii limeharakishwa hivi?
Hata wabunge waliobaki bungeni nakuhakikishia zaidi ya asilimia 70 hawajui miswada hiyo ina nini, imekusudia nini na ina tija gani kwa wananchi
Lakini pia inaweza kutumika katika hoja za uchaguzi. Tunajua matatizo yaliyotokea mikoa ya kusini hadi askari wa jeshi
Upo uwezekano ni njia ya kutafuta hoja wakati wa kampeni
Ni hoja kama hizo tumeona kesi zikichukua miaka 8 kuamlizika kuelekea uchaguzi.
Na sasa zinatumika kuonyesha CCM inachukizwa na rushwa.
Wakati huo huo kuna lundo la rushwa kama za escrow zikimezewa tu, achilia mbali viporo vya ufisaidi visivyo na majibu
Wananchi walitakiwa waunge mkono hoja za wapinzani na upinzani kwa ujumla.
Hakuna litalofanyika katika muundo wa serikali ya sasa au bunge la sasa
Hao wagombea wa CCM hawana jipya. Kila mmoja anasifu mafasnikio ya awamu ya nne.
Halafu anasemaatasimama kidete kupinga rushwa.
Yaani wanakubali rushwa ni tatizo bado wanasifu serikali iliyopo imefanya vema
Tumeangalia madahalo wa JF na Maria Saraungi. Watia nia wanatetea deni la taifa.
Tatizo si kukopa, bali kwanini tunakopa kiasi hicho.
Tunapokopa na pesa kuishia mikononi mwa mafisadi wachache ni kuwabebesha mzigo watu wasiofaidika na mikopo hiyo.
Mfano, misamaha ya kodi peke yake ni Trilioni1, pesa za ufujaji za taarifa ya CAG, wizi na shugguli zisizo na manufaa kwa wananchi. Ni kiasi kikubwa sana
Utashangaa katika udanganyifu huu bado wananchi wanadhani wapo malaika ndani ya CCM wanaoweza kuwa mworabaini
Kenya walisimama nakusema hapana. Leo wametoka kundi la nchi masikini sana.
Tanzania bado tunaaminibaada ya miaka 50 ya umasikini ipo 5 inayokuja na malaika anayesubiriwakutangazwa Dodoma.
Kama hatubadiliki na kujiuliza, miaka 50 ijayo tutakuwa tumesimama hapa hapa
Tusemezane
Mkuu wabunge wetu wengi kweli wanasikitisha. Lakini hata Spika mwenyewe ni wa ajabu, nadhani she is the worst speaker we have ever had, na bunge lenyewe ni bunge ambalo ni ovyo kabisa kuliko yote. NIdhamu hakuna, lakini hata umakini kwa kazi haonekani. Ninachoona ni wapinzani kufanya kazi yao kwa kujitahidi sana, lakini walio wengi ni kama wingi wao umewafanya wabweteke.
Tukiangalia tangu 2005 hadi sasa kwa hali ya kawaida CCM ilitakiwa kuaga, lakini nashangaa kuona uchaguzi wa ndani wa CCM unakuwa na umuhimu hata kuliko mengine yote.
Nakubaliana na wewe watanzania tunatakiwa kusemezana zaidi.
Mkuu kuhusu spika, wengine tulielewa ni tatizo tangu mwanzo.Mkuu wabunge wetu wengi kweli wanasikitisha. Lakini hata Spika mwenyewe ni wa ajabu, nadhani she is the worst speaker we have ever had, na bunge lenyewe ni bunge ambalo ni ovyo kabisa kuliko yote. NIdhamu hakuna, lakini hata umakini kwa kazi haonekani. Ninachoona ni wapinzani kufanya kazi yao kwa kujitahidi sana, lakini walio wengi ni kama wingi wao umewafanya wabweteke.
Tukiangalia tangu 2005 hadi sasa kwa hali ya kawaida CCM ilitakiwa kuaga, lakini nashangaa kuona uchaguzi wa ndani wa CCM unakuwa na umuhimu hata kuliko mengine yote.
Nakubaliana na wewe watanzania tunatakiwa kusemezana zaidi.
Kwa bahat mbaya na nzuri kwa CCM, Wananchi wanapenda amani na utulivu, yaani wanaibiwa kwa escrow wanasema hewala, wakipandishiwa kodi kufidia escrow wanasema hewala, wakipandishiwa umeme wanasema tumwachie mungu ni kazi yake
Leo wenzetu wote majiranii, wanakimbia, sisi tumebaki tumechuchumaa . Wananchi hawaoni hili
Dodoma, kinachotokea wananchi, ni wezi kuchagua mwizi mwenzao. Hofu inapaswa kuwa kwa familia za wezi
Nashangaa eti anayedhulumiwa naye ana hofu, kubwa gani la maadui litapewa kiti.
Watanzania imefika mahali mujiulize, mna matatizo gani
Tusemezane jamani
Na siyo maudhi peke yake, imefikia mahali udanganyifu unafanyika wazi na watu wanakubali.Mkuu Nguruvi hapa tuko pamoja kabisa. Kama utakuwa umenisoma vizuri kwenye mabandiko yangu, huwa nasema Tanzania tumekumbwa na tatizo la Stockholm Syndrome...CCM licha ya maudhi yote na mabaya inayotufanyia, EPA, Richmond, Radar, Escrow etc etc kweli watu wanasimama na kusema kidumu chama cha mapinduzi. Sielewi maana yake nini.
Kweli ukiangalia Kenya, imepiga hatua mara mbili zaidi ya Tanzania, ukiangalia Rwanda pamoja na udogo wake inapiga hatua kuliko TZ, Uganda ukiangalia inajitahidi sana....sisi wenzetu ni burundi tu, nao siku si nyingi watauacha.
Lazima tusemezane ili tuamshane na kuwafanya viongozi wetu walete msukumo wa maendeleo ya nchi, si yao binafsi. Tanzania inatakiwa kuwa ya kwanza, this is what God has given us, we need to take care of Tanzania.
Mkuu , hoja yako imezangatiwa na tunafanyia kaziMkuu Nguruvi3 naomba nichepuke kidogo kutoka uchambuzi wa hotuba ya mkuu wa nchi, can w discuss a little bit kinachomalizikia Dodoma? Pamoja na misukosuko ya Dodoma, CCM sasa wanajinasibu kwamba wako wamoja( wametoka wamoja Dodoma) na kwa kutumia kete ya Mgufuli watawapiga UKAWA sana na kwa kura nyingi. Najiuliza kweli watanzania wanasahau mapema kiasi hicho? Watafanya maamuzi kwa sababu ya mtu na sio kwamba system nzima ya CCM amabayo kwao wanaona ni utata??
Nina hamu sana ya kujua uchaguzi wa mwaka huu pamoja na mazingira ya kiuchaguzi, nione maamuzi ya watanzania yako influenced na jambo gani na je wanaangalia hali halisi ya maisha yao???