MTAZAMO WA JUMLA
Upo umuhimu wa kuwaeleza wananchi umuhimu wa uchaguzi na athari za khanga na kofia za siku.
Kuwaamsha watambue wanaowachagua si viongozi wa vyama ni wa nchi.
Wananchi wafahamishwe, muda wa wagombea 'kuleta maendeleo nchini au jimboni' umepitwa na wakati.
Maendeleo ni zoezi linaloshirika wananchi, wabunge au Rais ni kiungo.
Wagombea hawana makontena ya maendeleo bandarini.
Wanachotakiwa kueleza ni matatizo waliyo nayo wananchi na watayatatua vipi.
Tumeona wagombea wa CCM wakiorodhesha matatizo ya wananchi, wanayajua kwasababu walikuwa ndani ya mfumo huo wengine kwa miaka 40. Hatutarajii kusikia wakiimba nyimbo za elimu, umasikini, afya n.k.Tunajua hayo ni matatizo yaliyopo nchini siku zote.
Tunataka kuwasikia wakitumia takwimu, vielelezo na namba kutoa suluhu za matatizo yetu.
Miaka 50 ni nchi masikini, watueleza kwanini ni masikini na wanadhani kwa kutumia rasilimali gani ,zinazotoka wapi tunaweza kuondoka kundi hilo
Tunataka kuwasikia wakitueleza, kwanini miaka 50 bajeti ya nchi asilimia 40 ni wafadhili.
Tunafanya nini kuondokana na ufadhili unaouza uhuru wetu na kutufanya dhalili kila tunapotembea duniani
Tunataka watueleze, mmomonyoko wa maadili katika jamii chanzo chake ni nini.
Mivutano ya kidini iliyopo na hii inayozuka ya kikanda chanzo chake nini, watafanya nini kurejesha umoja na mshikamano wa kitaifa. Hatutaki kuwasikia wakilipa masheikh na maaskofu kuwasadia katika kampeni. Tunataka suluhu ya tatizo
Tunataka watueleza, wakisema wanamaliza umasikini, ni kwa hesabu gani, kutoka rasilimali zipi na kwa njia zipi.
Hatutegemei utajiri wao wataugawa kwa wananchi. Tunataka tuone kwa namna jinsi wanavyomalaiza umasiki
Tunataka kuwasikia, wanakbailiana vipi na tatizo la rushwa, ufisadi. Hatutaki kusikia wakilaani maana wanaishi nao kila siku
Tunataka kuwasiki, wakisema wanaendeleza jimbo, ni kwa rasilimali zipi, utaratibu gani na kwa vipi.
Hatutaki wajenge madaraja na shule kwa pesa zao. Hatutaki walete ambulance kwa pesa zao, tunataka tuone sisi kama wananchi tunapangaje, tunachagua vipi na tunatekeleza vipi wao wakiwa viungo.
Kampeni za kuorodhesha matatizo ya wananchi ni za kipuuzi za watu waioijua nchi hii.
Hata wale wanaoijua kama waziri mmoja aliyepo madarakani anayegombea, ambaye miaka 40 yupo serikali, bado hana cha kutuambia, anatuorodheshea matatizo tena kama waziri wa sera na mipango
Kampeni zetu zibadilike, tunataka uhalisia. Mtu akisema atafanya ABC atuonyeshe, hatutaki 'lip service'' miaka 50 inatosha.
Tunataka kama anaongelea uchumi aweke namba, takwimu, vielelezo na ushahidi na si kutuambia atachukua mirahaba ya madini wakati hajui hata madini yaliyopo nchini
Wananchi wachague watu kutokana na mitazamo yao ya kuendeleza taifa na si vyama vyao.
Ukimuona mtu anakuja na ilani au sera za chama ujue hajui tatizo la jimbo lako, hajui tatizo la nchi yako, amebeba makabrasha ili kukuibia tu aendele kulala Dodoma.
Kataeni matapeli hawa wawe wa CCM au Upinzani. Ni matapeli tu waambie wabebe sera warudi nazo kwenye vyama vyao.
Tunataka kiongozi anayeeleza sera zinazoendeana na mazingira aliyosimama