VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Huu mwaka ni wa tofauti. Ni mwaka wa kipekee wa kiuchaguzi. Tangu demokrasia ya vyama vingi ianze mwaka 1992 na uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapo 1995, CCM haikuwahi kuwa kwenye mgagaziko kama mwaka huu. 2015 ni kiboko. Hadi sasa, chama chetu pendwa hakina mgombea wa Urais. Ni jambo dogo lakini linalostaajabisha.Haijawahi kutokea. Ni jambo la kuingizwa kwenye kitabu cha Guiness.
Ndani ya CCM,kumetamalaki makundi. Ni kitu cha kawaida chamani. Ndani ya chama wasiotakiwa wanajitakisha kwa nguvu;wanaotakiwa hawataki. Wanaotaka hawana nguvu-ya kifedha na kiushawishi. Patashika nguo kuhanika chamani. Ni mara ya kwanza Tanzania itashuhudia chama tawala-CCM kikiwa na mgombea wa Urais badala ya Rais mtarajiwa. Haijawahi kutokea CCM kuogopa na kuchelewa kumwanika mgombea wake.
Kwa niliyoyashuhudia kanda ya kusini (Lindi, Mtwara na Ruvuma),kanda ya mashariki (Dar es Salaam,Pwani na Morogoro) na sasa kanda ya kaskazini (Tanga, Klmanjaro, Arusha na Manyara), sihofu wala kusita kusema kuwa CCM itakuwa kwenye uzani sawa na wapinzani kwenye mbio za Urais,Ubunge na Udiwani. CCM haitatisha na kuonekana imeshashinda mahali au nafasi fulani.Never!
Nitakapokwenda Dodoma kwenye vikao vya kichama,nitajipa muda wa kuidurusu kanda ya kati (Singida na Dodoma). baadaye kanda ya ziwa na kanda nyinginezo. Nasema tena,ni kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Tanzania, CCM itakuwa na mgombea wa Urais badala ya Rais mtarajiwa. Mambo yamebadilika!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)