Heri ya x-mass na mwakampya wapendwa, ndo siku hizo zinayoyoma kuuona mwaka mpya ukifika. Tukumbuke kumuomba Mungu kwani ni bahati nzuri kwa kufika hapa kwani kuna waliolala vitandani kwa kuumwa, ajari na mengine mengi. Kwa mwaka 2013 CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO {CHADEMA} kifanye mambo yafuatayo ili iwe mojawapo ya maandalizi ya kuingia ikuru ya magogoni;
1. Uhamasishaji uzame vijijini kwenye ngazi ya mkoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji, na mashina.
2. wawe na malengo[TARGETS}mfano wanawake na wazee ambao bado hawajafunguka kabisa.
3. matawi yafunguliwe kila siku iendayo kwa Bwana sehemu mbalimbali nchi nzima.
4. vyombo vya habari viongozi wa chadema wasilipuuze kwani ni nguzo muhimu katika kampeni.kauli za maudhi zikomeshwe majukwaani,wajikite zaidi kutoa sera na mikakati ya kuikwamua nchi na umasikini kwa watu
5.wanaotaka kugombea urais,ubunge na madiwani wajulikane ili wananchi wawafahamu mapema.
6.uhamasishaji wa vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kula iwe agenda ya kudumu katika mikutano
yote ya chama kwani vijana wanapiga kelele tu ila hawana kadi za kupigia kura,litiliwe msisitizo zaidi.