Weka maoni na ushauri wako kwa CCM

Asante CCM

JF-Expert Member
Jun 22, 2023
346
1,301
Chama cha Mapinduzi ni chama Tawala na kikongwe hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa kuzingatia ukongwe wake pengine ungependa kushauri ama kutoa maoni yako kwa namna ya Chama hicho kiendelee kuboreka na kuyaboresha maisha ya Wananchi?

Zingatia, weka maoni yako kwa lugha ya staha!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
 
Tuanze na huu
JamiiForums-259242959.jpg
 
Wang'ang'anie hapohapo wasitoke, nataka na mimi nije kuingia hapo kwa mda wangu nichote hadi za vitukuu nistaafu mie
 
Wawaondoe wahuni ndani ya chama, japo najua ni kitu kisichowezekana
CCM kama Chama kitaendelea kuwachukulia hatua wale wote watakao kengeuka na miiko ya Chama.

Rejea wakati uliopitia hakika Chama hakikusta kuwachukulia hatua wale wote ima waliofanya ama walikiuka miiko.
 
Wang'ang'anie hapohapo wasitoke, nataka na mimi nije kuingia hapo kwa mda wangu nichote hadi za vitukuu nistaafu mie
Karibu ni kwa ajili ya wewe uje kujiunga kwa minajili ya kuwatumikia Wananchi.
 
Ni Chama pekee chenye uwezo wa kubadilisha siasa za Afrika mashariki au Barani

Ni Chama kinachohitaji mabadiliko kama sio mapinduzi ya haraka kuenda na wakati na Siasa(siasa za nyakati) za Barani na Duniani

Ni Chama pekee kisichowashirikisha wananchi na NChi katika maamuzi yanayohitaji jumuishi ya na Ushirikiano wa, sauti moja.

CCM wanakiburi wameanza kupuuza Wananchi wake tena.
 
Chama cha Mapinduzi ni chama Tawala na kikongwe hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa kuzingatia ukongwe wake pengine ungependa kushauri ama kutoa maoni yako kwa namna ya Chama hicho kiendelee kuboreka na kuyaboresha maisha ya Wananchi?

Zingatia, weka maoni yako kwa lugha ya staha!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
Anzeni kutafuta mtanganyika kwa nafasi ya urais 2025 la sivyo mmeliwa.
 
Ni chama cha hovyo sana, chama ni kile chenye sauti juu ya mgombea wake yaani Rais, Rais anapovurunda chama kiwe na uwezo wa kumwambia hapa umekosea na ukiendelea kukosea tutakuweka pembeni Ref: ANC south Africa na kwingineko, duniani kote chama utakiwa kuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom