2013: Ungependa CHADEMA wafanye nini zaidi?

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
0
Ewee mpenda mabadiliko,

Mwaka 2013 ungependa Chadema wafanyenini zaidi kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla?
 

davytzee

Member
Nov 25, 2012
62
0
waonyeshe Umoja/Ushirikiano na mshikamano baina ya viongozi wa kubwa wa chama!!



HAPPY NEW YEAR
 

Bukutonaga

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
246
195
Wahakikishe wanaunda jeshi imara kuanzia Vitongoji/Mitaa,Vijiji,kata, wilaya na Mikoa ila mhimu zaidi ni vitongoji hapo watashinda kwa kishindo tena ushindi wa tsunami
 

mwalimu maskini

Senior Member
Feb 21, 2012
169
0
waonyeshe Umoja/Ushirikiano na mshikamano baina ya viongozi wa kubwa wa chama!!



HAPPY NEW YEAR
na kama kuna ambao hawashikamani hata wakishikwa,hawashiriki hata kama wanausika, wanaamini kwenye ndoto na malengo yao zaidi kuliko ukobozi wa nchi yetu na wengine wanadhihaki our misheni("kile ninachoitwa ukombozi wa pili" by mchange) unasemaje?
 

2c2

Member
Nov 5, 2009
98
0
Wajitahidi kuwa wanazungumza lugha moja kuanzia viongozi hadi wanachama porojo za kugombea vyeo waache,
 

dada jane

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
565
0
Wajiimarishe vijijini hasa mikoa ya pembezoni. Wawe makini na matamko yanayotolewa na viongozi wa ccm e.g mwigulu, nape ambayo ni kandamizi kwa wafanyakazi ili kuwatishia. Wajitahidi kutoa msaada wa kisheria kwani mwaka 2010 na mwaka huu kuna wafanyakazi wamefukuzwa kazi kisa anaoneka shabiki wa cdm. Rejea matamko ya Chemba juzi mailioja.
 

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,098
2,000
Waasi wa kundi haramu la Masalia wa Pindua Mbowe Group-PM7 wafukuzwe bila kuonewa huruma.
 

Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,945
1,500
Wakuu, happy new year. Chadema is my favoured political party. Hivyo ningependa wafanye yafuatayo 2013.
1) Wazidishe m4c kuelekea vijijini-walenge makundi maalum ya hakina mama, wazee...

2) Juhudi za usajiri wanachama wapya ziongezwe (kadi hazionekani au hazitoshi)

3) Chama kishinikize mabadiriko ya kupata tume huru ya uchaguzi hata kama mabadiriko ya katiba yatakuwa bado.

4) propaganda za uzushi na zisizo na mashiko zijibiwe kwa ustaha na kwa coverage kubwa ktk vyombo vya habari-

5) chama kisisitize mwendelezo wa amani na kiwe tayari kuonesha vimelea kutoka ccm vinavyoweza kuvurugs amani kwa kisingizio cha vyama vingine

6) Matumizi ya vyombo vya habari yaongezwe, youtube, sms ....na media za chama....

7) chama kianze mapema kutafuta wagombea ubunge, urais...na kuwaandaa-semina za uongozi

8) Chama kiendeleee kuwaandaa watanzania kwa mabadiriko...zaidi ujuzi na jinsi ya kurinda kura zao.
 

mtendaji wa kijiji

JF-Expert Member
Jul 3, 2012
533
195
1. Mijini sasa wanajulikana waende vijijini wakawafungue macho Wa Tz wafungue misingi, matawi na viongozi huko vijijini.

2. Wanaohtaji kadi ni wengi sana hivyo kadi ziwenyingi pamoja na Katiba ya chama na miongozo mingine.

3. Wabunge wawatetee wananchi bungeni kwa kasi ambayo haijawah kutokea, hili litafanikiwa kwa kukaa karibu na wananchi, kufanya tafiti.

4. Kuhakikisha makundi yote yanayo daiwa kuwepo yana vunjwa.

5. Kuibua hoja ambazo hazikupatiwa majawabu na bunge kama RICHMOND.

6. Kujenga mtandao mzuri wa kuwasiliana na wanachama.

7. Kuanzisha MEDIA za Chama.

8.Kutoipa nafasi ya kupumua ccm kwa kila namna
 

hayaland

JF-Expert Member
May 4, 2012
661
500
Heri ya x-mass na mwakampya wapendwa, ndo siku hizo zinayoyoma kuuona mwaka mpya ukifika. Tukumbuke kumuomba Mungu kwani ni bahati nzuri kwa kufika hapa kwani kuna waliolala vitandani kwa kuumwa, ajari na mengine mengi. Kwa mwaka 2013 CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO {CHADEMA} kifanye mambo yafuatayo ili iwe mojawapo ya maandalizi ya kuingia ikuru ya magogoni;

1. Uhamasishaji uzame vijijini kwenye ngazi ya mkoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji, na mashina.

2. wawe na malengo[TARGETS}mfano wanawake na wazee ambao bado hawajafunguka kabisa.

3. matawi yafunguliwe kila siku iendayo kwa Bwana sehemu mbalimbali nchi nzima.

4. vyombo vya habari viongozi wa chadema wasilipuuze kwani ni nguzo muhimu katika kampeni.kauli za maudhi zikomeshwe majukwaani,wajikite zaidi kutoa sera na mikakati ya kuikwamua nchi na umasikini kwa watu

5.wanaotaka kugombea urais,ubunge na madiwani wajulikane ili wananchi wawafahamu mapema.

6.uhamasishaji wa vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kula iwe agenda ya kudumu katika mikutano
yote ya chama kwani vijana wanapiga kelele tu ila hawana kadi za kupigia kura,litiliwe msisitizo zaidi.
 

paulk

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
240
195
mwaka 2013
1.waache kuhamasisha maandamano yasiyo na tija ambayo yataendelea kumwaga damu za watanzania.
2. waache siasa za chuki na vitisho kwani hazisaidii kukuza chama.
3.waache lugha za kupingana wenyewe kwa wenyewe kwani hiyo ni dalili ya kushindwa.
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
5,484
2,000
Wasijaribu kumsema Mkapa vibaya kwani watanzania wengi wanaamini yeye ni binadamu na alifanya mengi twayaona mfano lami Mwanza to Dar,maji Kahama Shinyanga, kudhibiti mfumuko wa bei nk.Wengi tunaamini CCM ndiyo adui yetu mkubwa ingawa tunawaheshimu wachache km Mwakyembe,Magufuli nk
 

Tumaini Makene

Verified Member
Jan 6, 2012
2,620
1,500
Wasijaribu kumsema Mkapa vibaya kwani watanzania wengi wanaamini yeye ni binadamu na alifanya mengi twayaona mfano lami Mwanza to Dar,maji Kahama Shinyanga, kudhibiti mfumuko wa bei nk.Wengi tunaamini CCM ndiyo adui yetu mkubwa ingawa tunawaheshimu wachache km Mwakyembe,Magufuli nk
We have no exceptional with fisadis and Chidodo. Naona unataka kurudisha nyuma mapambano dhidi ua ufisadi. Unajua Mkapa ni namba ngapi katika List of shame. Vipi nyumba za umma?!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom