hivi gesi ina enda dar au bagamoyo?
Kote kote.
Dar ni kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme, majumbani na viwandani (tayari kuna viwanda kama Twiga Cement vinatumia gesi kama nishati). Kwa Bagamoyo, kuna Wachina wameshajenga viwanda tayari, wanahitaji gesi kama nishati ya kuendeshea mitambo yao, mbali na umeme. Viwanda hivi viko upande wa kushoto, kama unakwenda Bagamoyo ukitokea Dar, nadhani ni nyuma kidogo ya eneo linaloitwa Kiromo
ok! nimekupata.navifahamu hivyo viwanda.sasa mbona watu wanaongea kama inaenda bagamoyo nyumbani kwa kikwete?Kote kote.
Dar ni kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme, majumbani na viwandani (tayari kuna viwanda kama Twiga Cement vinatumia gesi kama nishati). Kwa Bagamoyo, kuna Wachina wameshajenga viwanda tayari, wanahitaji gesi kama nishati ya kuendeshea mitambo yao, mbali na umeme. Viwanda hivi viko upande wa kushoto, kama unakwenda Bagamoyo ukitokea Dar, nadhani ni nyuma kidogo ya eneo linaloitwa Kiromo
ok! nimekupata.navifahamu hivyo viwanda.sasa mbona watu wanaongea kama inaenda bagamoyo nyumbani kwa kikwete?
Umerithi mikoba ya sheikh Yahya?!Ndugu Wana JF,
Kwa hali ya upepo wa kisiasa unavyokwenda ndani ya CCM kuanzia Januari Mwaka huu wa 2013 ni wazi kuwa CCM sasa inaelekea kuanza kwa makundi mbali mbali yatakayofanya chama sikivu kirudi tena Dodoma na Kuvunja makundi kama wataweza kutokana na matamko yafuatayo.
GESI YA MTWARA NA MATAMKO:
Mbunge wa Mtwara Mjini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara na nk.:
wao wako tayari kupoteza nyazifa zao kwa kutokubali gesi kwenda Dar/Bagamoyo
Mwenyekiti CCM taifa, Makamu Mwenyekiti na Naibu waziri Mawasiliano, Waziri wa Nishati na Madini na nk.:
hawa wako tayari kutumia nafasi zao kushinikiza gesi kusafirishwa mapaka Dar/Bagamoyo
Kwa kuwa wanaobishana wote ni wanachama wa CCM ni wazi kuwa wapo wanaofuata matakwa ya wananchi na wengine wanaofuata matakwa ya Mkuu wa nchi hivyo basi hali hii italeta pande mbili la wafia wananchi na wafia mkuu wa nchi.
URAISI KWA TIKETI YA CCM 2015 NA MATAMKO
Salaamu za EL mwaka mpya kwa Watanzania:
salamu za maamuzi magumu zilizotolewa baada ya kikao cha EL na Shelukindo, Chenge, Mgeja na Serukamba, na baadae kufuatiwa na kauli ya uamuzi mgumu wa shelukindo wa kumpigania EL kumrithi JK ni kirusi kingine ambacho kinawaambia wanamtandao wa EL wachukue maamuzi magumu ya kuweka bayana ni nani wako nao wa kupeperusha bendera ya CCM 2015. kwa hali hii 2013 ni mwanzo wa mapande yatakayozaliwa CCM kwa wawania uraisi tena kwa vijembe vya hali ya juu.
yaliyoandikwa hapo juu ni mtazamo wangu kisiasa na mwenye kupinga au kusapoti kwa hoja au kukashifu, kutukana, kukejeli wote mnakaribishwa maana ndio demokrasia yenyewe.
Umeona; walitaka kukiua CHADEMA sasa yamewageuka. Sawa tumeona mara nyingi migogoro ya CCM huwa inaisha kwa kutulizana na fedha wanazotuibia kwa kuwa wao ni chama tawala na hivyo kutumia nafasi hiyo vile wanavyotaka. Mimi napingana na anayesema wataendelea kutawala kwa mtindo huo. Mbona haya ya watu kutaka rasilimali wazifaidi pia wakazi wa maeneo husika na mambo mengine mengi ya watu kudai haki zao za msingi yanajitokeza sasa, kuliko wakati mwingine wowote? Hii inaonyesha wazi watu kuelimika na kuwa na uelewa wa kutosha juu ya yanayoendelea katika nchi yao. Kwa maana hiyo CCM wasitegemee mteremko 2015 kama walivyozoea kushinda kwa kura za mizengwe. Hii si nchi ya EL au Shelukindo nk.
mtoa mada umenena vyema ila nahauri tusitegemee migogoro ndani ya ccm ndio iwatoe madarakani kama alivyosema mchangiaji mmoja nikweli watakorogana lkn shekeli zikiwekwa mezani wanasahau shida zao kwa muda na kuanza kuimba ccm oyee! Kuwe na mgogoro kusiwe na mgogoro tuhakikisheni ccm 2015 inakuwa chama pinzani.