2011 UDSM nilinusurika kukamatwa

Baada ya kufukuzwa udsm hakurudi pale alienda kuanza shule upya pale sua nahisi alisomea kati ya kozi zifuatazo sociology, AEA au ualimu.

Na pia alikuwa RAIS wa serikali ya wanafunzi wa SUA ( SUASO)
Alihitimu SUA, udsm alifukuzwa....SUA pia aligombea urais wa chuo Japo hakufanikwa kupata
Ooh ahsante
 
Yeah nikweli mkuu, madogo walisuffer sana
 
Uzi tayari?
 
Kipindi hicho shule nyingi zilikuwa zinakabiliwa na baa la njaa, kama kumbukumbu ziko sawa kipindi hicho wazabuni waligoma kwa sababu serikali ilikuwa haijawalipa kwa muda mrefu, baadhi ya shule zilifikia hatua ya kufungwa kwa ukosefu wa chakula
Kweli kabisa.. nakumbuka mwaka 2008 njaa ilisababisha tukagawiwa chai na maharage Kama dinner kisa shule haikuwa na unga wa kupika ugali...
Ilikuwa shida sana..
 
Kweli kabisa.. nakumbuka mwaka 2008 njaa ilisababisha tukagawiwa chai na maharage Kama dinner kisa shule haikuwa na unga wa kupika ugali...
Ilikuwa shida sana..
Chai na maharage kama dinner bado unasema ilikuwa shida sana?
 
Ndiyo yule pia alimzingua Dr Kawambwa alipokuja pale chini ya shuttle point kusikiliza hoja za wanafunzi,tukaishiwa kupigwa mabomu.......Kumbukumbu kama zipo sawa ni Mwita
Nilichojifunza kwenye wengi poana mengi. Wewe unaweza ukawa unafikiri kua lengo lenu ni moja ila kumbe miongoni mwenu kuna watu wana maelngo tofauti kabisa na maovu. Kusema kweli mgomo wa 2011 ulikua wa mwisho na sidhani kama itakaa kutokea mgomo mwingine tena kwenye vyuo vikuu.
Vijana walifanikiwa kwa asilimia mia moja kwenye mgomo ule japo furaha iligeuka msiba baada ya kusherehekea ushindi kwa kutaka kwenda kutoa kipigo kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) ambapo ilikuja kutafsiriwa kama jaribio la kutaka kupindua serikali ya wanafunzi.

Wakati mwingine najiuliza kama wale wanaosomea uandishi wa habari (Mass communication) matukio kama yale hawawezi hata kuyaandalia habari kwa kina na kuja na kitabu au makala zinazoelezea kwa kina kiini cha tatizo na masimulizi mpaka ilivyoisha na hasara au faida zilizopatikana.

Ila yote kumi tisa yule jamaa aliyejiita alshabab alikua mtu wa tofauti sana (Charismatic leader) kwa waliokuwepo mitaa ya chuo na kufatilia kiundani jamaa alijaliwa uwezo wa kushawishi watu.

jina lake lilikua halifahamiki kwa hiyo hata utawala walipata shida sana kumdhibiti mana hawajui ni nani wala anasoma kozi gani, alisumbua sana.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…