20% - Tamaa Mbaya Lyrics - Kweli alistahili tuzo tano .

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Sifa ya moyo tamaa, moyo sifa yake kutamani
Tamaa ya moyo, inaweza kukuweka matatani
Unatamani kuzaa, wakati bado uko shuleni
Tumia akili kukataza, kabla hujawa matatizoni
Ile ndoto ya kitandani, achana nayo
Kama uhanisi labda haiwezekani, kuendana nayo
Unaweza ukaota umejenga angani, angani
kuhifadhi ndoto ya shida gani, wewe.

Chorus --Tuliza moyo wako, kubali mapungufu yakoooo
--Rahisisha mahitaji yako, ongeza kipato chakooo
--Chunga tamaa mbaya, chunga tamaa mbaya x2

Sifa ya macho kuona, kutazama kinachoonekana
Ila sio kila unachokiona, utadhani kupata inawezekana
Nyumbani kuna msichana, njiani utaona wengi wasichana
Bora kuishia kutazama, kuliko kujifanya unaweza sana
Siri ya maisha yako iko kwa muumba, muumba
Alisema mbuzi ni mbuzi hawezi kuwa simba, kuwa simba
Hawezi kuongea, eti anaforce kuimba
Bora kutulia ama kupiga marimba, utasikika pia

Chorus.......

Mwanzo wa safari nakufuata kijana, nakuja na swali unipe jibu la maana
Dunia bila wizi hivi itawezekana, kama haiwezekani siku tukijaonana,
Nitakiweka mbali kisimu changu cha mchina, vijana wote nitawaona hamna maana
Tunarudishana nyuma mambo ya kuibiana, mwenzenu naona noma polisi kupelekana, yeaah.

Chorus......


Masharobaro hebu angalieni hayo mashairi na ujumbe uliomo, halafu muamue kama hakuchukua tuzo tano kwa kuwa anastahili, msisahau Ya nini Malumbano.
 
thanx man,mashairi yametulia.hiyo verse ya mwisho nimeipata vzr now.jamaa alistahili,tumechoka kusikia mapenzi tuuu kila siku
 
Sio Oyoyo oyoyo...............ana ana anaanaado.........................kinyaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom