1995 - 2017 RIP Wanamtandao wa CCM

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Kufuatia kwa kutimuliwa kwa viongozi waandamizi wa CCM hiyo dalili tosha kwa chama hicho kimechoka kuwa na makundi ndani ya chama ambao kazi kupigia debe mtu katika nia ya kutwaa madaraka.

Nakumbuka mwaka 2005 jinsi hawa Wanamtandao walivyotumia kila aina ya mbinu ili kuchukua madaraka pamoja na kutoa kashfa mbaya sana dhidi ya mgombea mwenzao Dk Salim Ahamed Salim.

Sasa ni wakati wa wabunge kama kina Bashe wajitafakari upya la sivyo wataonyeshwa milango kama hao wengine waliotimuliwa.

Kwa maamuzi ya mkutano mkuu CCM imeonyesha wanachama wako makini katika kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM kupitia Kamati kuu katika kuleta CCM yenye matumaini.
 
CCM KAMWE haiwezi kuonyesha umakini kwa kuendelea kuwakumbatia wahuni, mafisadi, wala rushwa, majangili, wizi, Bashite etc.

Miezi michache tu iliyopita pale mtaa wa lumumba wamegawana rushwa ya milioni 10 kila mbunge ili wapitishe muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini.
 
Unaota ndugu yangu. Mtandao hauwezi epukika ndani ya CCM. Kilichofanyika mtandao umehamishwa.

Kwa sasa Mwenyekiti anaendelea kuweka ngome yake ambayo kila kitu kitakachoanzishwa na mwenyekiti kwao ni ndiyo mzee. Kundi hili la sasa ni hatari zaidi maana lengo lake kuu si kukitumikia chama bali matumbo yao.
 
CCM KAMWE haiwezi kuonyesha umakini kwa kuendelea kuwakumbatia wahuni, mafisadi, wala rushwa, majangili, wizi, Bashite etc.

Miezi michache tu iliyopita pale mtaa wa lumumba wamegawana rushwa ya milioni 10 kila mbunge ili wapitishe muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini.
Je utaweza kuyathibitisha haya maneno yako ukiwa mahakamani au ndio upayukaji wa usiyoyajua?
 
CCM KAMWE haiwezi kuonyesha umakini kwa kuendelea kuwakumbatia wahuni, mafisadi, wala rushwa, majangili, wizi, Bashite etc.

Miezi michache tu iliyopita pale mtaa wa lumumba wamegawana rushwa ya milioni 10 kila mbunge ili wapitishe muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini.
Wauza madawa ya kulevya na mafisadi wamejibanza chadema
 
Back
Top Bottom