1980 to 1990+ njooni hapa tukutane

sindesunde

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
358
346
Habari zenu Wahenga wenzangu, nataka tujikumbushe kipindi cha nyuma kidogo kwa yale machache tunayo kumbuka ila mtanisamehe kwa uwandishi wangu usio mzuri! Napenda tukumbushane ktk mambo mbalimbali ikiwa usafiri maeneno vituko vya zama hizo.

Naanzaia mkoa wa nikikumbuka miaka 1980+ upende wa usafiri haswa daladala ilikuwa vituko tupu maana unakuta daladala inaanzia k/koo au posta inaishia magomeni mapipa sio kama amekatisha ruti hapana ndio ruti yake hiyo!

Nyingine zilikuwa zinaishia manzese msufini nyingine ubungo maji kulikuwa hakuna daladala ya kimara mbezi kutokea town hapo bila kusahau ruti ya manzese to mabibo mwisho. manzese to sinza kwa remi. ubungo to buguruni. ubungo to mwenge via chuo kikuu kulikuwa hakuna ya moja kwa moja. Mwenge to kawe. magoni to dri cinema.kariakoo mikocheni b.karikoo to uwanja ndege au mombasa.

Sasa masi yalikuwa zama hizo nawakumbusha baazi yao DAU LA MNYONGE lilikua leyland cd ubungo/posta.WAGOSI WAKAYA isuzu pua la ng,ombe ubungo/posta. CONCOD benzi buguni/ubungo.ADVANTURE leyland temeke posta. kumbuka kipindi hicho karikoo kulkua hakupatikani basi za kwenda mbagala iliwaidi wakazi wa huko wapande mbasi mpaka temeke ndio wapande ya mbagala tena yapo yalikua yanaishia kizuiani na rangi 3.wakazi wa tegeta na viunga vyake watakua wanaikumbuka SOZA COM isuzu mwenge/tegeta ikifika saa 1 usiku usafiri uliku hakuna wa kurudi mwenge lami mwisho lugalo.

Bagamoyo chuma kilikuwa kinakimbia sana kilikua kinaitwa cassanova ktk pepe huku nyuma waliandika nausifu mtwangio hii chombo ilikua TATA nyingine nayo ilikua moto chini AMIT leyland cd hii ilikua wakati inapanda pale kerege ilikua mpaka raha maana ilikua inalalamika kama nyuki ila madeva wa zamani walijua kuchea gia sana maana huyu wa AMIT alikua anatisha kwa kuchezea gia maana mpaka abiria wanapandwa na mzuka!iHiyo ndio kipindi watu wa kusini wakikumbuka wanaweza kulia sana kutokana na ubovu wa barabara na ambayo ilikua unaweza toka dar unakwenda lindi ukamaliza ata wiki 3 njiani mto rufiji ulikua tatizo ukiondoa ukorofi wa barabara kuanzia ikwirir mpaka lindi.

Miaka hiyo kulikuwa na chuma kinaishia ikwilili SIMBA WANYIKA leyland flani hivi ndogo.BABA NI BABA boss wake alikua anaitwa jamar.bila ya kuwatupa ndugu zetu wa muhoro walikua na basi lao pendwa la mwana mama mmoja kibonge alikua anaishi mitaa ya clubu ya yanga hapon alikua anaitwa fatu shaha huyu mamaa alikua mbabe sana na alikua anasimamia mwenyewe masi yake ya MKARAMO BUS.

Sasa tunarudi kwa ndugu zetu wa kusini walikua na basi linaitwa BORN COAST hii ilikua mkonde aonekane mjanja na ametoka town lazima apande hii ndinga ilikua leyland victori lkn pamoja na ujanja wo wote mto ruiji uliwamaliza sana ndugu zetu wapo alio poteza maisha kwa kuzama na kivuko kile ch zamani na wapo walipoteza mali kwa kusombwa na maji ila kuna jambo moja tamu sana pale rufiji walikua wanafanya biashara sana kivuko kinapozingua.

Na wanaume wa kusini walikua na pesa walikua wanawazalisha sana wadada wa pale rufiji kwakua ulikua unaweza kua pale zaidi ya wiiki unasubili kuvuka na wa dada wa kusini walipa ujauzito sana pale maana anaweza kukwama akiwa hana akibwa basi masela wa kirufiji wanaruka nao tu wazee wanakuambia mechi ilitoka 0-0 baada ya daraja kuisha vizazi vilichanganyikana!Balaa unaweza kuvuka rufiji ila kwenda huko kusini ilikua unaweza ukaenda ata na mguu ukaunga baiskeli na treka wenyewe walikua wanayaita tele utasikia nimepanda tela au ukutane na chuma cha mgerumani ndio alikua mbabe wahuko zamani benzi double diff au bedford tk wenyewe utasikia nimepanda ngongongo kwa sababu lori likirusha wao wakawa wanaita hvvyo.

Ila kwa wale walikua wenye uwezo ndege ziliku za kutosha meli kama MV-CANADIAN MV-MAPINDUZI hii meli ya mapinduzi nakumbuka tulikua tunatoka mtwara miaka hiyo ilipoteza mwelekeo mpaka tukaja kusaidia na vikosi vya ulinzi vya comoro maisha haya!ktk miko ambayo ilikua uhakika wa safar mbeya na iringa maana nakumbuka ilikua tukifika pale mnazi mmoja ktk mataa kama ktk kampuni ya KWACHA BUS hii ndinga tambua ilikua ndio kama leo unyoona SAUL bila kusahau masi ya kitambo na wakozi wa nyanda za juu kusini KAMATA.

Tanga walikua na uhakika wa safari basi zao kali zilikua TAHAFIF.KIZOTA.BEMBEA.RAHALEO.morogoro kama mtakumbuka DAR EXPRESS zilikua fiat 110 SCORASTIKA sikania 82 ilikua hatari sana hii bus.ABOOD leyland cd.Narudi home kaskazini MAPANDE leyland daf hii basi sijui lifungwa nini maana saa 5 kasoro unakuta inachungulia uchira ikitokea dar hapo nyuma unamkuta SHABAHA scania na picha ya saadm husein.

NGORIKA hebu kumbuka ata miaka ya 1990 to 2000 mwanzoni KISWELE TAWAQAL SAIBABA SAFINA.

Ebu njoo tutililike wazee

4.JPG
1243290_Nissan.jpg
47686377_1881460931979820_4635401887238062080_n.jpg
kiswel 2.jpg
kiswele.jpeg
shabaha 1.jpg
shabaha2.jpg
tawaqar.jpg
UDA PHOTO.jpg
 
Kiswele yalipaki sinza mpaka yeharibika kabisa.

Tajiri wa adventure mpaka Leo anayaheshimu yale magari yake aliyounda body pale ilala anasema hata ikipiga mbuyu ni kunyajua na service kidogo chuma inayeya, ila ndo hivyo Mchina mchina tu. Thanks for remainder
 
nikikumbuka arusha ya zamani vifodi mwisho mbaudatu.kuanzia banda mblii jr mwendo wa sendeu tu dunia ikimbia mzee
 
Mimi nimekumbuka sana hiyo MSURE siku za jumapili tunarudi Pugu sekondari toka kuwatembelea ndugu mjini. Nakumbuka ile kona yake ya kulala pale airport ilikuwa burudani. Bila kusahau SHELLA BEACH.
 
Mimi nimekumbuka sana hiyo MSURE siku za jumapili tunarudi Pugu sekondari toka kuwatembelea ndugu mjini. Nakumbuka ile kona yake ya kulala pale airport ilikuwa burudani. Bila kusahau SHELLA BEACH.
Dah mkuu kumbe na wewe unaikumbuka hiyo shella beach ila kumbuka hivi vyuma .SEA NEVER DRY.INTER PROGRAM.TORINO.TANGA LINE. jangwani zilikua bonge la ligi
 
Sema mkuu wewe utakuwa muhenga hasa tena mtoto katikati ya JIJI umenifulsisha aisee kweli ilikuwa vituko kuna kama luti ya BUGURUNI ROZANA to MAGOMENI MAPIPA aisee ilikuwa shida.

Mtaan tulikuwa tunakaa na TAJIRI wa kiarabu anaitwa BORN CITY alikuwa na mabasi yake yameandikwa hvyo sikumbuki yalikuwa yanaenda mkoa gani ila jamaa ndo alowapoteza KOMANDO YOSSO siku walipovamia kwake ndo ukawa mwisho wao
 
Wakazi wa manzese nazani mnakumbuka hiece flani hivi ilikua kali sana ilikua inapiga manzese karikoo inatwa LONG BEACH hii hiace ilikua kali zama zile ila ata leo sijaona kwa hapo dar japo walikuja wakali wengine temeke COPS alikua na hiace kali hizi ndinga kipindi uzipati ktk sikuu safari ya kwenda NDEGE BEACH
 
Back
Top Bottom