1980 to 1990+ njooni hapa tukutane

1980 to 1990+ njooni hapa tukutane

Wahenga fungukeni tukumbushane mengineyo jamani
Ha ha ha mkuu MWENGE-POSTA km gari yako sio pamba na haina mziki mnene hio ruti utoboi na hata abiria wenyewe hawapandi ilikuwa ruti ya mabrazameni na masister duu
 
Sema mkuu wewe utakuwa muhenga hasa tena mtoto katikati ya JIJI umenifulsisha aisee kweli ilikuwa vituko kuna kama luti ya BUGURUNI ROZANA to MAGOMENI MAPIPA aisee ilikuwa shida
Mtaan tulikuwa tunakaa na TAJIRI wa kiarabu anaitwa BORN CITY alikuwa na mabasi yake yameandikwa hvyo sikumbuki yalikuwa yanaenda mkoa gani ila jamaa ndo alowapoteza KOMANDO YOSSO siku walipovamia kwake ndo ukawa mwisho wao
Enzi za mchiriku mnanda tulikua tunalipia kiingilio pale ccm manzese
 
wazee wa manzese tiptop uzuri njooni hapa tuliokua tunangalia video pale elenest ccm mnzese kipindi ambacho kulikua na mcheza karate maarufu satana au mpenda sifa huyu jamaa alikua anakera sana kwa unevu ila siku alivyongia kwa wachina uraiki ndio aliacha ujinga hiv bado yupo satana jamani
 
umenukumbusha mbali sana uhenga mwenzangu tulikua tunakuja airport tunaingia kwenda kucheki ndege hakuna kizuwizi mnakaa kule juu mnacheki madege tu
TULIKUWA TUNAPANDA HAPO AIRPORT KIULAINI KABISA. siku hizi hakuna hiyo mambo. naona wameziba pote
 
Osama umebadilisha dunia. Wazungu wanasema 'stupid action needs stupid reaction'
Hiv kabla ya Osama kugundulika gaidi gaidi alikua nani maana sipati picha kama Osama alizaliwa ktk familia tajiri kwa nini awe gaidi ila habari za upande mmoja uwa siziamini!
 
Kipindi hiyo kuona lori pale mtongani au rangi 3 linapakia abiria kwenda kusini usiulize kawaida tu
 
Back
Top Bottom