16 weeks pregnancy

16 weeks pregnancy

nzilani

Member
Joined
Feb 22, 2013
Posts
12
Reaction score
0
Hi to all JF Members.
Nina Mimba ya wiki 16.Ila kutokana na hali yangu kiafya kwa sasa(Kuugua sana) daktari wangu ananishauri kuwa niitoe la sivyo naweza kufa mimi endapo tatizo litaongezeka.Swali ni kuwa Je ni salama kutoa mimba ya wiki 16???Na ni wapi sehemu inayoaminika(Hospital au sehemu nyingine ile) ambayo naweza kwenda kuitoa???
Naombeni ushauri wenu tafadhali.
 
huyo dakatari alipaswa akutoe hiyo mimba kama ni lazima kufanya hivyo, otherwise ninachokiona ni kuwa wewe ndio unataka kuitoa mimba coz haiwezekani Dr akushauri utoe hiyo mimba halaf eti utafute pa kutolea huyo ni doctor kanjanja. Kumbuka utoaji wa mimba una madhara makubwa kwa afya zenu wadada ukiacha kuwa ni dhambi maana Mungu hamumuogopi siku hizi.
 
Bora umwambie ww
 
huyo doctor aliyeshauri utoe hajakuelekeza pa kutolea? au unataka ushee na sisi dhambi yako?
 
ww siyo mwanafunzi kweli unataka watu wakusaidie wap kwa kutoa hiyo mimba???? Arbotion ni zambi ya kuua lkn hata kisheria pia! Km uko Dar njoo amana ulizia daktar wa wazazi!
 
Hi to all JF Members.
Nina Mimba ya wiki 16.Ila kutokana na hali yangu kiafya kwa sasa(Kuugua sana) daktari wangu ananishauri kuwa niitoe la sivyo naweza kufa mimi endapo tatizo litaongezeka.Swali ni kuwa Je ni salama kutoa mimba ya wiki 16???Na ni wapi sehemu inayoaminika(Hospital au sehemu nyingine ile) ambayo naweza kwenda kuitoa???
Naombeni ushauri wenu tafadhali.
Tuambie kwanza tatizo lako lililopelekea daktari akushauri hivyo. Huyo daktari ni wa kada gani (MD, au specialist? - isije kuwa ni clinical officer au AMO)

Ninavyojua mimi kweli kuna medical indications za abortion, lakini ni mpaka jopo la madaktari watatu, wakae wakubaliane na watie sahihi hiyo mimba kutolewa, vinginevyo wewe na daktari wako mtakuwa hatiani.

Kimaadili na kiimani pia siwezi kumshauri mtu atoe mimba unless hiyo mimba ni kweli inatishia uhai wa mama.

Kama hutojali unaweza kutuambia hilo tatizo, la ukiona ni siri sana PM naweza kukupa ushauri wa kukusaidia.
 
Thnx mwathu.
Huyo Dr hana utaalamu wa utoaji japo pia alinielekeza kwa dr mwingine ila dhumuni langu lakuomba ushauri JF ni kwa sababu nina Imani wapo watu wanaojua na wenye utaalamu ambao pia wanaweza kunisaidia.
Hata hivo nimeolewa na sina tatizo na ndoa yangu siwezi kuamua tu kutoa mimba from no where .
 
Tafuta nchi ambayo utoaji wa mimba umehalalishwa, vinginevyo unachezea jinai. Na zaidi sana ungekuwa nchi hizi ambazo mie napiga mabox, wangechunguza kama hata ukitolewa hiyo Mimba afya yako itakuwa salama kivipi, na kama ingekuwa wakati wa kujifungua tayari basi ingekuwa mjadala nani aokolewe kati yako na mtoto. Napita tu, nimeacha mabox nikaona nichangie kidogo.
 
Si mwanafunzi nimemaliza chuo mwaka juzi na nimeshaolewa .
 
ina maana daktari kakushauri halafu kakuacha ukatafute pa kuitolea?
 
Thnx mwathu.
Huyo Dr hana utaalamu wa utoaji japo pia alinielekeza kwa dr mwingine ila dhumuni langu lakuomba ushauri JF ni kwa sababu nina Imani wapo watu wanaojua na wenye utaalamu ambao pia wanaweza kunisaidia.
Hata hivo nimeolewa na sina tatizo na ndoa yangu siwezi kuamua tu kutoa mimba from no where .

Tatizo gani hilo dada mpaka utoe Mimba?anyway,usikubali wala usikate tamaa juu ya hali yako,fika Muhimbili,waone madaktari bingwa wa kina mama,wasikie na wao watasema nin,then nenda Agha Khan,wasikilize pia ma-specialist wa kule,kina Shafiq,Kaguta na wengineo,sikiliza nao watasema nini kisha from there u may decide ku-abort kama ni Lazima or not..!otherwise usikubali kabisa kutoa mimba,ni uuaji na ni dhambi Imagine 16 weeks ur baby hata mikono na miguu ishaanza ku-protude!tulia kwanza usipatwe na papara!
Kwasababu hukueleza wazi tatizo lako la kiafya,please do that first (kuwaona-specialist) before you abort!
 
jee tatizo ni nini?isije ikawa solution sio kutoa.na hilo tatizo mwanzo halikujitokeza mpaka mimba imefikia wiki hizo?maana kwa hizo wiki mtoto tayari anacheza tumboni
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jamani tatizo lenyewe ni appendix ambayo inabidi kufanyiwa small operation kabla haijapasukia tumboni.Kwa sasa kuna dawa ambazo nimepewa nizitumie kwa siku 5 baada ya hapo ndo swala la operation litafuata.Wanadai kufanya operation kwa mjamzito ni hatari!
 
Inaruhusiwa kutoa mimba kama mwanamke yupo hatarini mfano hali yake kama anaweza mama kufa, kama itakuwa properly suggested by some responsible specialist/physician zaidi ya hapo ni big NO.

Hebu tueleze unataka kuto amimba sababu ya matatizo gani yani usipo itow amimba utakufa? kama hufi usikimbilie kutoa mimba bure, na ukijidai kuitoa hio mimba hio...itakuwa ndo ticket ya kukupeleka motoni.
 
Hebu copy hii link na u-paste kwa URL yako kisha usome! pregnancy.about.com/od/conditionscomplications/f/appendectomy.htm

So far uko kwa early second trimester, its safe even kufanya operation na mwanao akaishi. Don't go for abortion,bado nafanya searching na ntakuwekea hapa what literature says about your condition.pole dada!
 
Jamani tatizo lenyewe ni appendix ambayo inabidi kufanyiwa small operation kabla haijapasukia tumboni.Kwa sasa kuna dawa ambazo nimepewa nizitumie kwa siku 5 baada ya hapo ndo swala la operation litafuata.Wanadai kufanya operation kwa mjamzito ni hatari!
Dada pole sana, huyo daktari wako naona ni kati ya wale walipata zero form four waka-fluke wakawa madaktari. Appendicitis kama ni acute ni kweli inahitaji operation ya haraka (ni surgical emergence) asingekupa siku tano, inaweza kupasuka na ukapata madhara makubwa. Kama ni sub-acute appendicitis unaweza kupewa dawa na ikaisha hii huwa haihitaji upasuaji wa haraka unless imeturn into acute au imeshindwa kurespond kwa dawa.

Na operation kwa mama mjamzito si indication ya kutoa mimba. Ni kweli kwamba unapofanyiwa operation kuna uwezekano wa mimba kuharibika especially kama dawa za usingizi zilizotumika zinamadhara ya moja kwa moja kwa mtoto. Lakini kuna chance kubwa ukafanyiwa upasuaji na mimba yako ikaendelea kukua.

Trust me (if you can) nimefanya operation zaidi ya moja kwa mama mjamzito aliyekuwa na tatizo jingine na mimba zao hazikutoka, hivi last week nimemwona mmoja aliyekuja kwa follow-up akiwa na mimba yake ya wiki 36 sasa ana-approach term. Kati ya nilowafanyia operation wawili walikuwa na heterotopic pregnancy (yaani mimba moja imo ndani ya kizazi nyingine nje) na wote wawili mimba zao ziliendelea kukua licha ya operation nilizowafanyia ambazo ni kubwa kwa sababu mimba za nje zilishapasuka. Hii operation yako ni ndogo (kama utafanyiwa) ambayo haihitaji dawa ya usingizi ya muda mrefu wala haina manupulations nyingi, so chance ya kwamba mimba yako haitaharibika ni kubwa.

Nakushauri nenda Muhimbili waone madaktari bingwa wa upasuaji, kwanza wakuangalie na waridhike kwamba kweli ni appendicitis na pili wakushauri aina ya matibabu unayohitaji. Nenda haraka, kama ni appendicitis kweli inahitaji huduma ya haraka, LAKINI HAIHITAJI UTOLEWE MIMBA KABLA HUJATIBIWA.

Ningeshauri wajawazito wote, kama una-access ya specialist (obstetrician/gynaecologist) tafadhali muone yeye kwa ushauri wa uhakika.
 
Nashangaa mie mrembooo, hapa kila mtu anajifanya kuponda wakati rate ya utoaji mimba iko juu kuliko unavyodhania, kila siku foleni marie stopes ya watoa mimba. Sasa swali ni je kama kila mtu ni mpingaji hao watoa mimba ni akina nani sasa?? kaaaazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom