15 kizimbani wakidaiwa kutumia simu kutapeli

15 kizimbani wakidaiwa kutumia simu kutapeli

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
WAKAZI 15 wa wilaya ya Kilombero Morogoro wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutumia laini za watu wengine bila kutoa taarifa.

Washitakiwa hao ni mkulima Meniad Ndiyo (25), dereva bodaboda, Dotto Likumbai (29) , mkulima Abdallah Migoi (26) na mawakala Athumani Roho (28) na Onesmo Ngajela (24) . Walisomewa mashitaka 10 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga wakulima Saidi Sevenjari maarufu ‘Dangote’ (35) na Hasani Njalatango (34) walisomewa mashitaka sita.

Wafanyabiashara Filbert Ngatunga (26), Octavian Lekaleka (26) na madereva wa bodaboda Francis Mhombera (24) na Moses Mhindi (25) walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.

Mawakala Michael Ngalami (21) na Omary Mbena (31), wanakabiliwa na mashitaka saba mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mbando. Dereva wa pikipiki, Rashid Mshamu (23) na wakala Emmanuel Assey (19), wanakabiliwa na mashitaka sita mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashidi Chaungu.

Akisoma mashitaka, Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori alidai kuwa washitakiwa Sevenjari na Njalatango kati ya Januari Mosi na Juni 15, 2020 maeneo mbalimbali wilayani Kilombero, kwa pamoja walikula njama kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Pia alidai mshitakiwa Sevenjari alituma ujumbe mfupi wa maandishi, ukionesha kwamba Sh 300,000 zimepokewa kupitia Airtel money kutoka kwa Antony Ngonyani Juni 22 mwaka huu saa mbili asubuhi, hivyo salio ni 750,000/-.

Dangote anadaiwa alijipatia Sh 2,132,980 kutoka namba mbalimbali kwa kudanganya kwamba fedha hizo, zimetumwa kimakosa arudishiwe. Nyantori alidai Mei 22 mwaka huu maeneo ya Ifakara, kwa kupitia mfumo wa kompyuta mshitakiwa huyo alisambaza ujumbe kuonesha Ngonyani alipokea Sh 300,000 na salio lake ni 750,000 na kwamba fedha hizo zimetumwa kimakosa hivyo arudishiwe.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kushindwa kutoa taarifa kuhusu mabadiliko ya laini ya simu kosa walilolitenda Januari Mosi na Juni 15 mwaka huu maeneo ya Kilombero, na walitumia namba za simu zilizosajiliwa kwa majina ya watu wengine bila kutoa taarifa kwa mtoa huduma. Washitakiwa walikana mashitaka na walirudishwa rumande.

HabariLeo
 
Sijaielewa hii habari vizuri, kwamba imetumwa laki 3 jumla laki 7 na nusu[emoji16] ina maana kwenye account yangu nitakuwa sijui salio liliomo au inakuwaje
 
Kuna watu wao huamini jambo haraka, ile kupkea sms tu kwa sim yake anaamini kilichoandikwa bila kufanya uchunguzi ndio hawo wanaotuma ela kwa matapeli wanaowapigia sim wakijidai mawakala wa mitandao ya sim.
 
Sijaielewa hii habari vizuri, kwamba imetumwa laki 3 jumla laki 7 na nusu[emoji16] ina maana kwenye account yangu nitakuwa sijui salio liliomo au inakuwaje
Hii hata mimi wameshanitumia sana sema nikawashtukia, wanakupigia simu na kujifanya ni huduma kwa wateja na kukwambia kuna hela imetumwa kwako kimakosa...ukisema hujaiona wanakuuliza unakumbuka salio lako la pesa ni kiasi gani, ukitaja wanakwambia subiri sms ikiingia urudishe hizo hela zilizotumwa kimakosa.

Wanachokifanya ni kukutumia sms feki inayokaribia hela yako yote uliyonayo kwenye simu mfano una laki 5 wanaweza kuandika umetumiwa laki nne na tisini jumla salio lako ni 990,000 na kukutaka uirejeshe ile yao! Ukikurupuka kuirudisha tu 490,000 unajikuta salio lako ni Tsh 100 na simu haziiti tena.
 
Sijaielewa hii habari vizuri, kwamba imetumwa laki 3 jumla laki 7 na nusu[emoji16] ina maana kwenye account yangu nitakuwa sijui salio liliomo au inakuwaje
Kila siku wajinga wanazaliwa. Wanazeeka na wengine wanakufa

Hakuna kulaumiana

Viwanda vya utapeli vipo wapi ?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
HUWA NINAJIULIZA SAAANAA. MBONA MIMI NINAPOKEA MESEJ ZA MATAPELI KILA MARA?? NI LINI WAHUSIKA WATACHUKULIWA HATUA? MBONA NAMBA HIZO ZIMEONGEZEKA BAADA YA USAJILI WA VIDOLE KUANZA?!!

SASA KUMBE MAASKARI WANAWATIAGA NGUVUNI. SAFI SANA.
 
Hii hata mimi wameshanitumia sana sema nikawashtukia, wanakupigia simu na kujifanya ni huduma kwa wateja na kukwambia kuna hela imetumwa kwako kimakosa...ukisema hujaiona wanakuuliza unakumbuka salio lako la pesa ni kiasi gani, ukitaja wanakwambia subiri sms ikiingia urudishe hizo hela zilizotumwa kimakosa.
Wanachokifanya ni kukutumia sms feki inayokaribia hela yako yote uliyonayo kwenye simu mfano una laki 5 wanaweza kuandika umetumiwa laki nne na tisini jumla salio lako ni 990,000 na kukutaka uirejeshe ile yao! Ukikurupuka kuirudisha tu 490,000 unajikuta salio lako ni Tsh 100 na simu haziiti tena.
Ni kweli mkuu mimi walinifanyia hivyo hivyo ila nikawashtukia na kuwaambia acheni utapeli basi hiyo mitusi waliyonivurumishia hadi niliona aibu mie
Waazibiwe kabisa hao si watu wazuri
 
Nshapigiwa sim na mmoja kilichoniuzi nawa heki customer service was voda wananiambia hawawezi fanya lolote...hopeless sana
 
Back
Top Bottom