100$ Loan to Oldman | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

100$ Loan to Oldman

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Inkoskaz, Nov 10, 2010.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Mzee mmoja alienda bank kuomba mkopo wa dola 100,bank manager akwamwambia sharti awe na kitu cha dhamana ambapo kwa mshangao mzee alionyesha gari yake Ferrari yenye thamani kama dola laki tatu hivi..meneja hakuwa na kipingamizi akapokea pia file lenye document halali za gari na kumuelekeza kwa meneja mikopo amshughulikie mara moja na kumueleza kuwa riba ni 10% per month yaani dola kumi.mzee akakamata mkopo na kuondoka akiacha bank manager anaagiza gari lihifadhiwe na kulindwa vizuri kulingana na thamani yake.
  Baada ya mwezi kamili mzee alirejea na kurudisha mkopo na riba ya 10$ lakini bank manager akamuita ofisini kwake kwa mazungumzo zaidi ambapo alimuuliza mzee kuwa amechunguza na kubaini mzee ni mfanyabiashara anayejiweza sasa iweje aende kukopa benki yao kiasi kidogo tu cha fedha?Mzee kwa upole akamuuliza bank manager "Hivi ni wapi hapa mjini unaweza kupaki gari ya thamani kama hiyo yangu kwa usalama bila pressure mwezi mzima kwa ujira wa dola10 tu?"
   
Loading...