08/02/2011 CHADEMA Walkout: MSTARI UMECHORWA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

08/02/2011 CHADEMA Walkout: MSTARI UMECHORWA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Feb 9, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jana tarehe 08/02/2011 ni siku ambayo mimi na familia yangu tulifurahia jambo lililotokea Katika Bunge. Ni Jambo linaloumiza lakini ni jambo ambalo linafariji na Kutia hasira vile vile. Naona kuna watu humu ndani wanataka kutuaminisha kwamba kwamba eti wananchi zaidi ya milioni mbili ( 2,600,000) walioichagua CHADEMA wamekasirishwa na Kitendo kilichotokea jana. Mimi nawatakia kila la kheri wale wote wanaoamini hivyo.

  Kwa wengi tukio la Jana limeanza kuonesha MSTARI, MSTARI ambao ni Muhimu katika Mapambano yeyote ile, hata katika vita ili ushinde ni lazima Umtambue Adui yako. Vivyo katika Siasa kama unataka Upate Support ya wapiga Kura, ili wapiga kura wakuunge mkono ni Lazima Uchore MSTARI, MSTARI utakonesha kwa uwazi kabisa Pande Mbili.

  Pande Hizo mbili ni zile za Watetezi wa Wananchi na Watetezi wa Mafisadi

  MSTARI UMECHORWA
   
 2. S

  Selungo JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli "MSTARI UMECHORWA". Kwa wale wanaojidanganya kwamba, kitendo cha wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya kupinga hitimisho la maamuzi ya kutengua kanuni kimewaondolea heshima kwa Watanzania wananjidanganya. Kwa mtanzania yeyote yule ambaye amechoshwa na maisha haya ya umasikini uliokithiri, rushwa isiyopimika, ukosefu wa huduma muhimu kwa wananchi, elimu mbovu, ukandamizwaji wa demokrasia wa waziwazi, ufujaji wa mali za umma, wizi, ubinafsi na mengine mengi yanayo fanana na haya, atakubaliana kwa 100% na wabunge wa CHADEMA kuonyesha hisia zao za kupinga haya yote kwa kutoka nja ya bunge.

  Si jambo linalo hitaji kuwa na digrii kuyajua haya yote. Hata ambaye hawahi kwenda shule anaelewa wazi kwamba kwa hali ya serikali zinazoongozwa na sisiemu hazina nia ya thati ya kuleta maendelo ya kweli kwa watanzania zaidi ya kulinda maslahi yao, na hasa waliopo madarakani. Na vilevile kuwakandamiza Watanzania kwa njia yoyote ile ili mradi maslahi yao yanakuwa salama.

  Ki ukweli kitendo kilicho fanywa na wabunge wa CHADEMA kwetu sisi wananchi tunaohitaji kuondoshwa hapa tulipo, kwetu sisi tunawapongeza na kuwaona ni mashujaa wetu wa leo na kesho katika kumtetea mtanzania ambaye kila kukicha hali yake kijamii na kiuchumi inazidi kudidimia. Huku tukishuhudia kila anayepata nafasi ya kuingia kwenye mifereji ya sisiemu moja kwa moja ubinafsi unakuwa ndiyo sera kwake.

  Ni kweli MSTARI UMECHORWA unaoonyesha kipi chama cha kweli kilichoweka mbele maslahi ya Watanzania.

  Tunawapa hongera wabunge wa CHADEMA na tunawaunga mkono kwa nguvu zote. Kilichobaki tunawaomba mrudi lwa watanzania mkawaeleze nini kilicho tekea huku mkiwashita wazandiki na mahafidhina kwa kutotanguliza maslahi ya watanzania mbele.
   
 3. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Yah mstari umechorwa sasa waanze kushusha mavitu bungeni
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yanayotokea sasa yanampa kila mtu kuanza kukiangalia CHADEMA upya hata kama alikuwa anakipuuzia.

  Jana yalinikuta niko mahali napasha kidogo na mzee mmoja aliniuliza swali dogo tu" Hivi kwa nini CHADEMA tu?...CCM wakiongea wanakisema CHADEMA, CUF na wapinzani wengine wote wanaiongelea CHADEMA hii maana yake nini?" Nikamwambia ni KWA SABABU NI UPINZANI RASMI TANZANIA
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nitakumbuka daima maneno yako haya mkuu maana ndio ukweli wa yooooooooooooooooote yanayotokea katika siasa za Tanzania.
   
 6. mwanaharakati m

  mwanaharakati m Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MSITARI UMECHORWA, CHADEMA ndiyo chama pekee cha upinzani.....NCCR,CUF,UDP na TLP wameamua kujiunga na sisiemu ili wawe wanapigiwa makofi bungeni...lakini adhabu yao wataipata kwenye sanduku la kura 2015:clap2:
   
Loading...