The Alliance for Change and Transparency, sometimes known as the ACT–Wazalendo, is the third-largest political party in Tanzania. It received its permanent registration in May 2014.
Abdul Nondo akutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo Taifa Ndg. Abdul Nondo jana tarehe 03 Disemba 2024, alifanyiwa upasuaji mdogo kwenye unyayo baada ya madakatri wanaomuuguza katika hospitali ya Aga Khan kubaini uwepo wa mivunjiko midogomodogo...
Chama cha ACT Wazalendo kinatoa tamko muda huu kuhusu kutekwa kwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana, Abdul Nondo, nakutelekezwa usiku wa kuamkia leo katika fukwe za Coco Beach, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, Nondo alisaidiwa na dereva wa bodaboda aliyemfikisha katika ofisi...
Ndani ya Muda mfupi wametoa taarifa muhimu ambazo zitasaidia kupatikana kwa mfuasi wao
CHADEMA sasa hivi wangekuwa kwenye media wakitoa matamko kuna kitu wajifunze .
TAARIFA KWA UMMA
UCHAGUZI UBATILISHWE NA KUITISHWA UPYA
TAARIFA YA AWALI YA KAMATI YA UONGOZI TAIFA YA CHAMA CHA ACT WAZALENDO KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI 2024
Kamati ya Uongozi Taifa ya Chama cha ACT Wazalendo imekutana kwenye kikao chake cha dharura jana tarehe...
Bila kuwa mwanachama wa Chadema au ACT Wazalendo, nakiri kwamba Chadema, hawa kina Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Mbowe, na wakati fulani kina Msigwa, Dr. Slaa, Mtikila, Mrema, Dr. Kaborou na wengine, siku zote wamekuwa na nia nzuri sana na nchi yetu. Sina shaka juu ya hilo.
Sasa tatizo ni kwamba...
Chama cha ACT Wazalendo kimesema Wakala wao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, TINGA TOGORO KERANGA kutoka Kata ya Hunyari, Kijiji cha Mariwanda, Kituo cha Kilimani alifanyiwa fujo kwa kunyang'anywa karatasi za Kura na Wakala wa CCM ambaye alizichana baada ya kuona kuwa Wakala wa ACT...
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Geita, Lucas Tibengana amesema kuwa zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa limekumbwa na changamoto kutokana na mfumo wa majina, hali Iliyosababisha baadhi ya wananchi kushindwa kushiriki katika upigaji kura.
Akizungumza katika kituo cha kupigia...
Hali ya upigaji kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji leo tarehe 27, Novemba 2024 mpaka muda huu wa saa 8 kamili mchana.
TUKIO LA SHAMBULIZI
Kwa masikitiko makubwa tunapenda kuujulisha umma kuhusu tukio la kusikitisha lililotokea ambapo Katibu wa Jimbo la Igunga Ndugu...
Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Mtaa wa Mtambani kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Mohammed Mtutuma, ametoa ahadi ya kupambana na unyanyasaji na kuhakikisha heshima ya wananchi inalindwa, ikiwa ni sehemu ya kampeni zake kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024...
Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu , amewataka wananchi wa Kijiji cha Katanda, Kata ya ML. Magharibi, Jimbo la Tunduru Kaskazini, mkoani Ruvuma, kuzingatia vigezo vya uongozi bora badala ya kushikilia itikadi za vyama vya siasa wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Ado ametoa...
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo wa Jimbo la Tunduru Kaskazini mkoani Ruvuma, Yasin Mohamed Mawila, ametoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la udanganyifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Akizungumza Jumapili, Novemba 24, 2024, kwenye mkutano wa kampeni...
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo @ACTwazalendo Bara, Isihaka Mchinjita @MchinjitaIR, amesema kuwa suluhisho la kudumu la kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ni kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho anadai ndicho chanzo cha matatizo hayo.
Akihutubia wakazi wa kijiji cha...
Vyama vya siasa Chadema na ACT Wazalendo vimeungana katika Kata ya Bukuba, Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma, kwa kugawana nafasi za uongozi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Taifa, Abdul...
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema endapo wananchi wakikipa ridhaa chama chake kuongoza vijiji katika maeneo mbalimbali, wataongoza vijiji hivyo kama watakavyoongoza nchi.
Kupata nyuzi za kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread...
Wakuu
Katika tukio la kipekee Afisa wa jeshi la Polisi alijikuta akirekodi sehemu ya mkutano wa kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alipokuwa akiwaombea kura wagombea wa chama chake kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, katika kijiji cha Nyankwi kata ya Busunzu, jimbo la...
Chama cha ACT Wazalendo kimeendelea kuimarisha kampeni zake za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mtakuja, Kata ya Vingunguti, Jimbo la Segerea, Dar es Salaam.
Mkutano huo, uliovutia idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo, uliongozwa na Naibu...
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa, amewaomba wananchi wa Mtaa wa Komesho, Kata ya Msambweni, Jimbo la Tanga Mjini na vijiji vya jirani kuwaamini wagombea wa chama hicho kwa kuwapigia kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Akizungumza...
Wakuu,
Muda mchache baada ya Freeman Mbowe kukamatwa, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo mkoa wa Njombe amezungumza mwanzo mwisho nini hasa kimpelekea mpaka Mwenyekiti huyo kukamatwa.
Soma pia: Freeman Mbowe akamatwa na Jeshi la Polisi akielekea Mbozi mkoani Songwe
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa...
TAARIFA KUTOKA ACT WAZALENDO
Kwa masikitiko makubwa, tumepokea taarifa ya kukamatwa na Polisi kwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo wa Mkoa wa Songwe leo tarehe 22, November, Ndugu Ezekia Elia Zambi bila sababu za msingi zinazojulikana.
Pia soma: LGE2024 - Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro...
Wakuu
Jeshi la Polisi limemzuia mwenyekiti wa Chama cha CHADMA, Taifa, Freeman Mbowe kuzungumza na wananchi wa Mbozi, Mkoani Songwe, na kuwatawanya kwa mabomu wananchi waliokusanyika kumsikiliza mwenyekiti.
Kwa mujibu wa Ratiba eneo hilo lilikuwa na mkutano wa Chama cha ACT wazalendo mchana wa...