uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. JamiiForums Tanzania LGE2024 Askofu Fredrick Shoo alia na rafu zinazoendelea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Ataja mbinu zinazotumika kuengua Wagombea!

    Dkt. Fredrick Shoo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), hivi leo amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa linaloendelea nchini. Dkt Shoo amesema kumekuwa na makosa mengi katika Ucahguzi huu ikiwemo kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani...
  2. JamiiForums Tanzania PreGE2025 Ni mbinu ya kupata kura?, Utekelezaji wa miradi na miundombinu kipindi cha Uchaguzi: Je, Usalama wa Mazingira na Uendelevu unazingatiwa?

    Muda wa uchaguzi ni kipindi cha kipekee katika mchakato wa kisiasa, ambapo wagombea na vyama vya siasa hutumia kila mbinu kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda kura. Katika mazingira ya Tanzania, utekelezaji wa miradi ya miundombinu na maendeleo wakati wa uchaguzi umejikita kama sehemu muhimu...
  3. JamiiForums Tanzania LGE2024 TAKUKURU Iringa kuanzisha uchunguzi kuhusu wagombea wa serikali za mitaa kujitoa baada ya rushwa

    Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Iringa Imeanzisha Uchunguzi wa Madai ya Uwepo Baadhi ya Wagombea wa Serikali za Mitaa kujitoa Kugombea Baada ya kupewa Rushwa. Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa, Domina Mkama ametoa Kauli Hiyo wakati akizungumzia Utendaji Kazi wa Taasisi...
  4. JamiiForums Tanzania LGE2024 Geita: Wagombea walioenguliwa watuhumiwa kutoa vitisho kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Wakuu Kumbe CCM wakiwatishia wapinzani ni sawa tu lakini Waoinzani wakiwatishia CCM, viongozi wake wanaenda hadi kwenye vyombo vya habari kulialia Hivi karibuni nimemuona Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Yefred Myenzi, akieleza kuwa baadhi ya wagombea ambao majina yao yalikatwa...
  5. JamiiForums Tanzania LGE2024 Benson Kigaila: Yeyote akisema hatukujiandaa na uchaguzi anafanya kazi ya CCM

    "Yeyote akisema hatukujiandaa na uchaguzi, awe Mwanachadema, awe MwanaCCM, awe hana Chama ana shida kati ya hizi mbili mosi; hakuwepo wakati wote wa zoezi hili hivyo hajui anachokizungumza au pili; anafanya kazi ya CCM kwa makusudi kabisa." Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Bara. Kupata...
  6. JamiiForums Tanzania LGE2024 Mkuu wa mkoa Tanga: Wasimamizi wa uchaguzi Tumieni 4R za Rais Samia

    Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian Batilda Burian amewataka viongozi wote ambao wana nafasi za kusimamia michakato ya uchaguzi,kusimamia agizo la kutumia 4R za Rais Samia katika kufanya kazi zao za uchaguzi. Amesema hayo wakati akitoa taarifa za michakato ya uchaguzi ulipofikia kwa...
  7. JamiiForums Tanzania LGE2024 Hujuma Uchaguzi: Mwakajoka atuhumu kuenguliwa kwa Wagombea wa CHADEMA Mikoani

    Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa Frank George Mwakajoka, amesema wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wamekiuka kanuni za uchaguzi kwa kuwaondoa wagombea wa chama hicho bila sababu za msingi. Mwakajoka amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa...
  8. JamiiForums Tanzania LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi akanusha wagombea CHADEMA kuwa na ulemavu

    Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na Msimamizi wa Uchaguzi, Dionis Myinga amekanusha malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wanaotajwa kuwa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti kwa baadhi ya vijiji katika wilaya hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa wameenguliwa baada...
  9. JamiiForums Tanzania LGE2024 Mara waridhishwa na mchakato wa Uchaguzi Serikali za Mitaa, waomba mamlaka ziendelee kufanya kazi nzuri ili haki ipatikane kwa kila mgombea

    Wakuu, Hawa wanamvua nguo Nchimbi aliyesema demokrasia yetu bado changa na hivyo OR TAMISEMI ilegeze kamba kidogo! Watu maefurahia zoezi yeye anataka waonekane wanoko! ==== Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa mkoani Mara wameeleza kuridhishwa na mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu...
  10. JamiiForums Tanzania LGE2024 Kubenea: Hakuna uchaguzi, kuna uchafuzi. Vyama kuendelea kushiriki ni kuhalalisha uhuni, madhara yake yataonekana 2025

    Kupitia andiko hilo la leo, Jumanne Novemba 12.2024 Kubenea ambaye ni mwanahabari nguli nchini na Mkurugenzi wa kampuni ya habari ya Mwanahalisi amedai kuwa kitendo cha vyama vya upinzani nchini kuendelea kushiriki uchaguzi huo ni sawa na kuhalalisha 'uhuni' unaoendelea, na hivyo kutahadharisha...
  11. JamiiForums Tanzania LGE2024 ACT Wazalendo: Wagombea wetu 51,423 wameenguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Chama cha ACT Wazalendo kinatoa Taarifa kwa Umma kuwa wagombea wake 51423 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji wameenguliwa kwa sababu ya udhamini wa chama ngazi ya Kata. Wagombea wetu waliogongewa mihuri ya Kata ambayo ndio ngazi ya udhamini ya ACT Wazalendo wameenguliwa...
  12. JamiiForums Tanzania Serikali inaukaribisha Mlipuko au Vurugu kipindi hiki cha uchaguzi

    Chama cha upinzani Chadema kwa muda sasa wameshindwa kuunganisha nguvu ya umma dhidi ya serkali. Sasa ni serikali yenyewe imeleta kiwashio cha bomu. Chadema sasa inatakiwa ku detonate na nchi nzima ilipuke. Ni simple sana. Kwa kuwa kuenguliwa kwa wagombea wao ni mkakati, na hata baada ya...
  13. JamiiForums Tanzania Mpasuko Chadema wiki mbili kabla ya Uchaguzi

    Yapo madai kwamba mikutano mwingine ya Chadema inaruhusiwa na Polisi lakini baadaye Polisi wanaizuia kutokana na shinikizo kutoka ndani ya Chadema. Sasa tunakwenda kwenye huu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa: matumaini yangu ni kwamba itakuwa Uchaguzi wa amani. Huu ni Uchaguzi ambao utaonyesha...
  14. JamiiForums Tanzania TOC kufanya uchaguzi Disemba 14, Filbert Bayi Kugombea tena

    Kamati ya Olimpiki Tanzania , wazee wa TOC wanatarajia kufanya uchaguzi tarehe 14/12/2024 eneo lile lile la kila wakati DODOMA HOTEL , Dodoma na wasamizi wa uchaguzi ni watatu tu. Uchaguzi utatanguliwa na uchaguzi wa kamisheni ya wanamichezo. Filbert Bayi bado yuko busy kujipanga na rushwa ili...
  15. R

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Uchaguzi mkuu 2025 tutegemee wagombea wenye sifa kutoka CCM wakienguliwa na wasio na sifa wakipitishwa na kusimamiwa waende bunge bila kupigiwa kura;

    Chama cha siasa katika siasa za vyama vingi ujipima kukubalika kwake kwa kuruhusu wananchi kupiga kura Kwa hali ilivyo sana nchni ni wazi hakuna tena utaratibu wa kupata viongozi kupitia uchaguzi bali viongozi wa kisiasa wanateuliwa na tume ya uchaguzi au wasimamizi wa uchaguzi Ni vigumu...
  16. JamiiForums Tanzania Uchaguzi ujao utakuwa ni wanaume vs wanawake.

    Watawala wetu siku zote na muda wote wanataja wanawake, wanawake, wasichana, wasichana muda wote kwenye mipango yao. Wanaume na wavulana hawasikiki hata kidogo. Kama atajitokeza mgombea mwanaume anaeaminika (sio Lissu) patachimbika. Vijana wa kiume wanavuja damu kwenye mioyo yao. Hawajisikii...
  17. JamiiForums Tanzania LGE2024 Changamoto za uendeshaji wa zoezi la Uchaguzi nchini na hasara inayopatikana kwa taifa

    BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MAMA SAMIA SULUHU HASSAN YAH: CHANGAMOTO ZA UENDESHAJI WA ZOEZI LA UCHAGUZI NCHINI NA HASARA INAYOPATIKANA KWA TAIFA Mheshimiwa Rais, Kwa heshima na taadhima, napenda kuchukua nafasi hii kuandika barua hii ya wazi kwako...
  18. JamiiForums Tanzania Naona dhahiri vyama vingine vya upinzani vimetendewa haki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Tanzania tuna vyama vya siasa takribani 18 kama sijakosea. Vyama ambavyo vimekua vikilalamika tangu wakati wa uandikishaji wapiga kura nawaona CHADEMA, CUF NA ACT. Hii inadhihirisha kwamba wale wala ubwabwa na wenzake wamesimamisha wagombea na hawajakutana na changamoto yoyote. Na inasemekana...
  19. JamiiForums Tanzania LGE2024 Chadema hamkujiandaa na uchaguzi, acheni kulalamika!

    Tangu mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulipoanza, sijaona viongozi wa CHADEMA wakieleza mkakati wa kushiriki na kushinda uchaguzi huo. Badala yake, wamejikita kwenye malalamiko dhidi ya CCM na serikali. Hakuna hata mchakato wa wazi uliotumika kuwapata wagombea ndani ya chama. Walikaa...
  20. JamiiForums Tanzania LGE2024 Madiwani wasusia Baraza kisa matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Mtwara

    Novemba 8, 2024, madiwani 10 wa vyama vya upinzani wa Halmashauri ya Mtwara wamesusia kikao cha Baraza la Madiwani. Hatua hiyo inatokana na kile wanachoeleza kuwa kutokubaliana na maamuzi ya msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri hiyo, ambaye amewaengua baadhi ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…